Pages

 

Monday, August 11, 2014

HASIRA ZAMFANYA VAN GAAL KURUDI UHOLANZI

0 comments
Baada ya Kocha wa Manchester United Louis Van Gaal  kuchukizwa na kitendo cha kukosa windo lake alilokuwa amelitolea macho muda mrefu,anajiandaa kufunga safari kuelekea Uholanzi kutafuta njia mpya ya kujifariji kwa kuvamia Klabu ya Ajax nchini humo

Manchester United wanajiandaa kutoa ofa ya kitita cha pauni 15 milioni kumnasa beki Daley Blind,baada ya kutoka kapa kwenye mbio za kumuwania Thomas Vermaelen,gazeti la Mirror nchini Uingereza limeripoti leo.
LVG anasemekana kumuwekea kipaumbele Varmaelen katika muda huu mchache uliobaki wa dirisha la usajili,lakini jana wababe wa Catalan waliitangazia dunia kuwa wameshamnasa beki huyo raia wa Ubelgiji aliyetimka kutoka Arsenal.

Akiwa anachukizwa na vigingi anavyokutana navyo kwenye usajili,Van Gaal bado hajakata tamaa,kiasi kwamba yuko tayari kufanya uvamizi kwenye klabu ya Ajax,kumnasa Blind

.Daley Danny Blind ambaye ni mtoto wa Danny Blind, kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Uholanzi,alijizolea sifa wakati wa michuano ya Kombe la Dunia nchini Brazil kwa uwezo wake wa kuzuia na kusaidia mashambulizi tangu mechi yao ya kwanza dhidi ya Spain,alipotoa krosi murua ilyozaa bao safi la kusawazisha la Van Persie Blind ana uwezo wa kucheza nafasi  tofauti ,hasa beki wa kati au kiungo wa kati. ingawaje anajisikia poa kukaba upande wa kushoto

Kiasi cha pauni milioni 15 zitawekwa mezani siku chache zijazo kwa ajili ya nyota huyo wa Kiholanzi mwenye umri wa miaka 24 na imedokezwa kuwa Ajax,wamesalimu amri kumpoteza mchezaji wao huyo muhimu,baada ya Blind mwenyewe kuonesha nia ya kutaka kuondoka.

Aliwahi kusema"Unategemea nifanye nini Van Gaal atakaponihitaji Manchester United?Inabidi nitafakari.
Kombe la Dunia limeniongezea heshima kama mchezaji na nilishaweka bayana kuwa kama kuna watu watakuja na ofa nzuri nitawasikiliza."




Read more...

Friday, August 2, 2013

NANDO ALITAKA KUJIUA

0 comments
 
Siku  chache zilizopita mwakilishi wa Tanzania kwenye shindano la Big Brother Africa 8 (The Chase) Nando alitimuliwa kutoka kwenye jumba linalowahifadhi washiriki wa shindano hilo kwakile kilichoonekana kutishia usalama wa mshiriki mwenzake Elikem,mwakilishi wa Ghana.
Habari mpya hivi sasa ni juu ya `tweet` ya mshiriki huyo juu ya jaribio lake la kutaka kujiua mwaka 2011
Hii inaonesha kuwa Nando amepitia kwenye utoto wenye misukosuko na juzi kati alikiri kuwahi kutumia tiba maalum ya kupambana na matatizo aliyokuwanayo.Labda pengine njia hizi za maisha ndio zilizojenga tabia yake ya ukorofi
Tukio hilo la kujaribu kujiua lilipelekea mwaka mmoja baadae aanzishe ukurasa wa Facebook aliouita L.O.V.E ambao ameufanya maalum kwa watu waliopitia masukosuko ya kimaisha kujadiliana.

Read more...

HIVI NDIVYO AKINA MASOGANGE WALIVYOPITA UWANJA WA NDEGE DAR

0 comments

CHANZO CHA HABARI:GAZETI LA MTANZANIA
TUKIO la wasichana wawili wa Tanzania waliokamatwa na dawa za kulevya Afrika Kusini, limechukua sura mpya baada ya kujulikana kwamba, siku ambayo watuhumiwa hao walisafiri kupitia Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Dar es Salaam, mbwa wanaohakiki usalama wa mizigo hawakuwapo. 
 
Chanzo chetu cha habari kiliiambia MTAZANIA, kwamba pamoja na uwepo wa kitengo cha kudhibiti dawa za kulevya uwanjani hapo, kitengo hicho kina kasoro kadhaa zinazotakiwa kurekebishwa.

“Mimi niko hapa, najua kila kinachoendelea, nakwambia siku hiyo ambayo wale wasichana walipitisha dawa hizo, hapakuwa na mbwa wa kunusa, naamini kama mbwa wangek
uwapo, lazima siri ingefichuka,” kilisema chanzo hicho.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, katika viwanja vya ndege kuna vitengo vingi vikiwamo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Idara ya Uhamiaji na askari polisi ambapo kila kitengo kina majukumu yake.
“Kwa hiyo, ninachotaka kukwambia ni kwamba, jukumu la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) ambayo baadhi ya watu wanasema inachangia kupitisha dawa za kulevya, haihusiki kwa sababu jukumu lake kuu ni kuzuia vitu vinavyohatarisha usalama wa ndege na abiria.

“Kuhusu uzito wa mizigo na malipo, hilo linafanywa na shirika la ndege husika na baada ya shughuli zote kufanyika, mizigo hukaguliwa kwa mashine na kunuswa na mbwa kabla ya safari kuanza,” kilisema chanzo hicho.

Pamoja na hayo, utata mwingine juu ya hali ya usalama na uwajibikaji wa watumishi wa uwanja huo wa ndege umejionyesha kupitia nyaraka zilizopatikana.

Uchunguzi uliofanywa na MTANZANIA kwa siku kadhaa sasa, umebaini dawa hizo kilo 150 aina ya Crystal Methamphetamine zenye thamani ya Sh bilioni 6.8 zilizokamatwa na wasichana hao, zilimhusisha pia mshirika wao kibiashara aliyefahamika kwa jina la Mangunga ambaye majina yake matatu tunayo.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo, wasichana hao, Agness Gerald (25) na Melisa Edward (24) walisafiri ndege moja na Mangunga wakitoka Dar es Salaam kwenda Afrika Kusini.

Nyaraka hizo zinaonyesha kwamba, wakati Manguga na wasichana hao wakisafiri na ndege ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA), namba SA 189, Julai 5 mwaka huu, walikuwa na mabegi tisa.

Nyaraka hizo zinaonyesha jina la Agness Gerald, kwamba ndiye aliyelipia mabegi hayo, lakini katika sehemu inayotakiwa kuandikwa barua pepe, imeandikwa barua pepe ya Mangunga inayosomeka, Nmangunga@Gmail.com.

Mabegi hayo, yalikuwa na kilo 150 za dawa za kulevya lakini kila mmoja alitakiwa kusafiri na kifurushi cha kilo 20 na hivyo kutakiwa kuwa na kilo 60 wote kwa pamoja.

Baada ya kila mmoja kuwa na kilo 20, zilibaki kilo 90 ambazo walizilipia Dola za Marekani 94 badala ya Dola 450.

Nyaraka zinaendelea kuonyesha kuwa, Mangunga, Agness na Merisa wakati wa safari yao walikaa kiti kimoja kilichokuwa na namba tofauti.

Agness alikaa kiti namba 23B, Mangunga alikaa kiti namba 23D na Melisa alikaa namba 23A.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Suleiman Suleiman, alipotakiwa kutoa ufafanuzi juu taarifa hizo, alikataa kulizungumzia kwa undani na kusema hana majibu kwa kuwa suala hilo liko katika uchunguzi.

Agness na Melisa, walikamatwa Julai 5 mwaka huu katika Uwanja wa Ndege wa Oliver Thambo nchini Afrika Kusini wakiwa na dawa za kulevya.

Wakati wanakamatwa, walikuwa na mabegi sita kati ya tisa waliyokuwa nayo wakati wanapanda ndege jijini Dar es Salaam.

Inasemekana mabegi matatu yaliondoka na Mangunga ambaye hadi sasa hajul
Read more...

Sunday, July 28, 2013

CHELSEA INAMTAKA MTOTO WA DAVIS MOSHA

0 comments
Edgar Davis Mosha mtoto wa mfanyabiashara tajiri na maarufu boss wa kampuni ya DELINA, Bwana Davis Mosha amehojiwa na VOA (Voice of America). Edgar na baba yake wametua kwa kishindo nchini Marekani wakitokea Uingereza ambapo Edgar amepeperusha vyema bendera ya Tanzania kwa kuitwa  kufanya majaribio na klabu ya Chelsea ya Uingereza..


  





Read more...

WATANZANIA WALIOKAMATWA NA MADAWA HONG KONG WATUMA WARAKA MZITO..WATAJA WAHUSIKA WAKUU..WAMO VIGOGO NA WAFANYABIASHARA MAARUFU

0 comments
WATANZANIA walio gerezani nchini Hong Kong kwa makosa ya kukutwa wakisafirisha madawa hatari ya kulevya,wametuma waraka mzito kwa wananchi wenzao kuelezea  mambo mengi ambayo wananchi wa kawaida hawayajui kuhusu biashara hiyo inayopigwa vita duniani kote,na pia wamewataja wahusika ambao ndio wamiliki wakuu wa biashara hiyo waraka wenyewe ni huu hapa chini..usome kwa makini:


Read more...

Friday, July 26, 2013

VYAMA VYA USHIRIKA NI MAGENGE YA WEZI-KIKWETE

0 comments
Rais Kikwete
Bukoba. Rais Jakaya Kikwete, amesema baadhi ya vyama vya ushirika nchini vina mkusanyiko wa wezi wanaokula fedha za wananchi bila hata kunawa.
Kikwete aliyasema hayo juzi jioni alipokuwa akizungumza na wananchi baada ya kufungua jengo la kitega uchumi la Chama cha Ushirika cha Mkoa wa Kagera (KCU), mjini Bukoba.
“Acheni kuwa wachuuzi tu wa kununua na kuuza mazao ya wananchi na badala yake mjiingize katika shughuli za uwekezaji na maendeleo ya kwelikweli ya wanachama wenu,” alinena Rais.
“Hapa Kagera ni kitovu cha ushirika na KCU ni kitovu cha kuboresha na kuleta usasa katika shughuli za ushirika. Siyo kama vyama vingine ambavyo ni mkusanyiko wa wezi wanaokula waziwazi mchana bila hata aibu ….wanakula bila kunawa,” alisisitiza.
Rais Kikwete alisema huko nyuma Serikali ilifanya uamuzi wa kulipa madeni yote ya ushirika nchini ili kuvipunguzia vyama mzigo wa kujiendesha.
Alisema hata hivyo sasa vyama hivyohivyo, vimeanza kujitumbukiza tena katika madeni na kwamba hiyo inatokana na kukosa viongozi waaminifu na waadilifu.
Kabla ya kuzindua jengo hilo, Rais Kikwete aliweka jiwe la msingi kwenye upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Bukoba ambao unapanuliwa ili kuufanya kuwa wa kisasa. Kazi hiyo itagharimu Sh21.015 bilioni, itakapokamilika.
Mradi huo wa upanuzi wa uwanja ulianza Februari mwaka jana na unatarajiwa kukamilika Februari mwakani.
Upanuzi huo ukikamilika uwanja huo utakuwa na uwezo wa kuhudumia wasafiri 500,000 kwa mwaka sawa na wasafiri 150 kwa saa.
Uwanja huo umekuwa ukilalamiwa kuwa ndiyo kikwazo cha kukosekana kwa huduma za uhakika za usafiri wa anga kati ya Kagera na mikoa mingine nchini.
Kwa sasa wananchi wengi wa mkoa huo wanaosafiri lwa ndege, wamekuwa wakiishia katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza na baadaye kusafiri kwa meli.
Read more...

HUU NI WARAKA MZITO KWA WATANZANIA KUTOKA KWA KALA JEREMIAH KUHUSU LOWASSA

0 comments
Msanii wa Hip hop Kala Jeremiah

TANGAZO KWA UMMA

MIMI KALA JEREMIAH NILIKUWA MSANII WA KWANZA TANZANIA KUMSEMA MHESHIMIWA EDWARD LOWASA KUPITIA WIMBO WANGU UITWAO WIMBO WA TAIFA BAADA YA MHESHIMIWA KUKUMBWA NA KASHFA YA UFISADI WA RICHMOND.KWA KIPINDI KILE KILA MMOJA WETU ALIHAMAKI SANA NA KUONA KWELI MZEE WA WATU NI FISADI.KWENYE WIMBO HUO KUNA MISTARI NILISEMA. mi siyo mwana siasa sisubiri tume ichunguze nistaafu ka Lowasa.

KWA KUWA MIMI NI MZURI SANA KWENYE KUFANYA UCHUNGUZI BINAFSI NILITUMIA MUDA MWINGI SANA KULICHUNGUZA SWALA HILI LA KASHFA HII NA BAADAE NILIGUNDUA KUWA NI SWALA LA KISIASA.NA YALIKUWA NI MAPITO AMBAYO MWANADAMU YOYOTE HUPEWA MUDA WA KUPITIA MAGUMU ILI KUPIMWA IMANI YAKE KWA MUNGU.

BAADA YA KUGUNDUA HAYO MWAKA JANA NILITENGENEZA WIMBO UNAOITWA AZIMIO LA ARUSHA AMBAO UPO KWENYE ALBUM YANGU YA PASAKA AMBAYO IKO SOKONI TOKEA MWAKA JANA. KATIKA WIMBO HUO WA AZIMIO LA ARUSHA NILIANDIKA MISTARI IFUATAYO. walipiga dili waka msakizia lowasa ili kuficha siri kali.NILIANDIKA MSTARI HUU BAADA YA KUFANYA UCHUNGUZI NA KUJIRIDHISHA KUWA MHESHIMIWA NI KIONGOZI BORA SANA NA HASA KWA UAMUZI WAKE WA KUJIUZULU BILA SHINIKIZO KUBWA NA WAKATI KWA NAFASI ALIYOKUWA NAYO YA UWAZIRI MKUU ALIKUWA NA UWEZO WA KUGOMA KUJIUZULU NA HASA KWA KUWA HAKUWA FISADI KAMA ILIVYOSEMWA.

MWEZI WA TATU MWISHONI MWAKA HUU NILITOA WIMBO UNAOKWENDA KWA JINA LA KARIBU DAR AMBAKO NILISEMA dar es salam ingekuwa nchi Rais angekuwa Lowasa huku watu washashtukia kuna mchezo kwenye siasa HAPA NILIKUWA NAMAANISHA KUWA WATU WENGI WANAOISHI DAR WANAWAHI KUJUA MAMBO YA WANASIASA KWA KUWA WANASIASA WANAISHI HUKU LAKINI PIA WATAFITI WENGI WA MAMBO YA KISIASA WANAISHI HUKU KWA HIYO NI RAHISI ZAIDI KUUJUA UKWELI MAPEMA.

NAAMINI KUONDOKA KWA LOWASA KWENYE UWAZIRI MKUU KUMEZOROTESHA MAENDELEO YA TAIFA KWA KIASI FLANI

NDUGU ZANGU WATANZANIA NI WAZI KUWA LOWASA NI JEMBE TENA JEMBE LA KAZI KUMBUKENI BILA LOWASA KUSINGEKUWA NA SHULE ZA KATA TANZANIA,NA ANGEENDELEA KUWEPO MADARAKANI ALIKUWA NA MPANGO WA KUANZA MCHAKATO WA ZAHANATI ZA KATA.IKUMBUKWE PIA LOWASA NDIYE ALIYESIMAMIA UJENZI WA CHUO CHA UDOM TENA KWA PESA ZA KITANZANIA BILA KUOMBAOMBA VIMIKOPO.

MRADI WA MAJI KUTOKA MWANZA KWENDA SHINYANGA NI KAZI YA LOWASA. ZIPO KAZI NYINGI AMBAZO NIKIZITAJA ZOTE NAWEZA KUJAZA UKURASA.NACHOJARIBU KUSEMA HAPA NI KWA KUWA MIMI NI MSANII NA NI KIOO CHA JAMII NINGEOMBA WEWE MWANAJAMII CHUKUA HATUA YA KUFANYA UCHUNGUZI BINAFSI KUHUSU LOWASA.BILA KUFUATA MKUMBO WA KISIASA NAAMINI UTAKUBALIANA NA MIMI KUWA LOWASA NI JEMBE.

MIMI HUWA NAPENDA KUSOMA VITABU VYA WANAHARAKATI NA KUNA KITABU KIMOJA NILIKIPITIA CHA MWANAHARAKATI KUTOKA ITALY AITWAE NICCOLO MACHIAVELLI AMBAYE ALIZALIWA MWAKA 1469 NA KUFARIKI 1527. KATIKA ENZI ZA UHAI WAKE ALIWAHI KUANDIKA VITABU KADHAA LAKINI KATI YA VITABU HIVYO KITABU KIITWACHO THE PRINCE NDICHO KILIMPA HESHIMA KUBWA SANA KWA KUWA ALIIKOSOA SERIKALI YA KIFALME YA KIPINDI HICHO KITU AMBACHO HAKIKUWA RAHISI KWA MTU KUFANYA HASA IKIKUMBUKWA KUWA ENZI ZA UFALME ZILIKUWA ENZI ZA UBABE. KATIKA MANENO KUTOKA KWENYE KITABU HICHO AMBAYO NINGE PENDA KUKUSHIRIKISHA WEWE NDUGU YANGU MTANZANIA NI MANENO YAFUATAYO MACHIAVELLI ALIANDIKA HIVI. kuna kipindi ambacho mataifa yanapita katika vipindi vigumu. na kwa kipindi hicho kigumu mataifa hayo yatahitaji sana kupata kiongozi mwenye kuweza kuchukua maamuzi magumu,na ambaye hatakuwa chini ya sauti ya mtu mwingine, na ambaye ataweza kuyatekeleza maamuzi magumu kwa haraka hata kama ni kwa kuwaumiza wachache ili wengi wawe huru.atakayekuwa tayari kutekeleza jambo baya ili likapita na kusahaulika na atakayetekeleza mambo mazuri kwa muda mrefu na yakaendlea kukumbukwa.kiongozi huyo atatakiwa kuchagua kuogopwa ama kupendwa lakini ni bora akachagua kuogopwa lakini akitenda haki kwa wananchi husika.HAYO NI BAADHI YA MANENO ALIYOANDIKA MACHIAVELLI KWENYE THE PRINCE KITABU AMBACHO KILIMPELEKEA KUITWA NA MFALME NA KUPEWA NAFASI YA JUU YA UONGOZI KATIKA SERIKALI HIYO YA KIFALME.

KWA MAONI YANGU NADHANI TAIFA LETU LIMEPITIA VIPINDI VIGUMU KADHAA NA KWA MANENO YA BWANA MACHIAVELLI NADHANI KIONGOZI ANAYEFAA AMBAYE ANAWEZA AKACHUKUA MAAMUZI MAGUMU NA AMBAYE HAWEZI KUWA CHINI YA SAUTI YA MTU MWINGINE NI MHESHIMIWA EDWARD NGOYAI LOWASA.

tafakari chukua hatua
Read more...

Monday, July 22, 2013

ORPHANED GIRL BURNT WITH HOT WATER BY HER KEEPER IN AN ARGUMENT OVER DISAPPEARED PART OF FOOD

0 comments
Dora after after reciving medical treatment

A twelve years old girl,student of Wazo Hill Primary School in Dar Es Salaam,has claimed that she was burnt with hot water by her niece, Saum Masudi.

The little girl whose name is Dora said she faced that kind of atrocity few days ago in the Wazo area where she lives with Saum, her niece, and keeper after the death of her father.

In her account of the tragedy Dora said that in the morning of that day she woke up early and cleaned the house and in that course visited the den where they keep ducks to clean it.


"After finishing with cleanliness I went inside the main house and found thick porridge which was left over since yesterday.I took few slabs off and gave them to ducks in the den,my sister (niece) was asleep at the time.When she woke up,she found  the thick porridge was halved so she demanded to know what happened to the food.I told her that I served some to our ducks.She didn`t believe me,so she pulled me to the den to prove it.At the time we arrive at the den,there was nothing, the food was long been eaten by ducks.She called me a liar,and started to tie my hands and legs together.After that she splashed very hot water around my body."
Dora shows off severity of inflictions she received

She said she was wounded in different parts of her body and she never received instant medical care after that.After few days the wounds started to rot and stink until the day one of her relatives paid a visit and wanted to shave her untidy hair.In the process the relative told her to take off the T-shirt she was wearing so it doesn`t get covered by her falling hair.That`s when the relative came to the horrific scene of stinking wounds.After recovering from her shock of the day, the relative wanted to know what really happened .Dora explained it all and Dora`s keeper fled the house immediatelly.

Dora poses with her helper Kauthari Isack
After the news of her miseries broke it`s boundaries,Dora said a good samaritan Kauthari Isack who was  emotinally touched by Dora`s story took her to the Police station and then to hospital for medical care.Kauthari confirmed that she helped Dora to hospital after becaming emotinally very touched by her story
"I took her firstly to the police station to get Police Form 3 so she could be accepted by medical staff at the hospital, and people at the police station opened a case no.KW/RB/6034/2013.The search for suspect has just begun and they (police) have husband of the suspect to help the search.

The Kinondoni Regional Police Commander ACP Camillius Wambura has confirmed the incident regarding Dora inflictions and of the ongoing searching of the suspect

"I warn all members of the public, that this kind of cruelty can not be tolerated.People should refrain from doing such things, because we have severe punishment in store for this"
Read more...

HUU NI UKATILI MKUBWA..YATIMA AMWAGIWA MAJI YA MOTO,KISA KIPORO CHA UGALI!

0 comments
Mtoto Dora baada ya kupata msaada kutoka kwa msamaria mwema

Mtoto Dora Juma,12, mwanafunzi wa Shule ya Msingi Wazo Hill, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam imedaiwa ameunguzwa kwa maji ya moto na binamu yake aliyetajwa kwa jina la Saum Masud.
Dora ambaye ni yatima alikutwa na dhahama hiyo hivi karibuni eneo la Wazo Dar alikokuwa akiishi na binamu yake huyo kama mlezi wake baada ya kufiwa na baba yake.
Akisimulia tukio hilo Dora alidai kuwa siku ya tukio aliamka asubuhi kufanya usafi wa uwanja nyumbani na akaingia katika banda la bata kwa ajili ya kulisafisha.
“Baada ya kumaliza usafi niliingia ndani na kukuta kiporo cha ugali nikakata kipande nikawapa bata bandani, wakati huo dada (Saum) alikuwa amelala, alipoamka na kukuta kiporo cha ugali kimekatwa aliniuliza nikamueleza nimewapa bata, hakuamini.
“Akaniambia twende bandani kuangalia kama nasema kweli, tulifika tukakuta bata wameula hali iliyomfanya  dada  kutoamini, alinifunga mikono na miguu na kuniunguza kwa maji ya moto sehemu mbalimbali mwilini,” alidai Dora.
Mtoto Dora akionesha alivyounguzwa mgongoni kwa kumwagiwa maji ya moto
Alisema baada ya kufanyiwa unyama huo hakupewa huduma yoyote na kusababisha vidonda kuoza na aliokolewa na ndugu yao mmoja aliyekwenda kuwatembelea na kutaka kumnyoa nywele.
“Aliniambia nivue fulana ili nywele zisinidondokee, nilipovua alishangaa kuona nina vidonda mwilini, nilipomueleza mkasa mzima aliwapigia simu ndugu wengine hali iliyofanya dada Saumu kukimbia na kwenda kusikojulikana,” alidai.
Dora alisema alichukuliwa na msamaria mwema aitwaye Kauthari Issack ambaye aliliambia kuwa kweli alimchukua binti huyo baada ya kuguswa na unyama aliofanyiwa.
Mtoto Dora akiwa na msamaria mwema Kauthari Isack
 “Baada ya kumchukua nilikwenda polisi kupata PF3 ili akatibiwe na anaendelea kutibiwa, askari wakafungua jalada namba  KW/RB/6034/2013 na wakaanza kumsaka mtuhumiwa lakini wakafanikiwa  kumkamata mumewe aitwaye Hamisi Kayanda ili aisaidie polisi,” alisema Kauthari.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni ACP Camillius Wambura amethibitisha mtoto huyo kufanyiwa kitendo hicho na kusakwa mtuhumiwa. “Niwaonye wananchi kwamba ukatili kama huu hauwezi kuvumiliwa, watu wajiepushe nao maana watachukuliwa hatua kali za kisheria,” alionya Kamanda Wambura.
Read more...
 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797