HABARI ZAKISIASA
UTAPATA HABARI MBALIMBALI ZA KISIASA KUTOKA NDANI NA NJE YA NCHI, UKIWA HAPAHAPASAID NUHU
HABARI ZA BURUDANI
UKIWA HAPA UTAPATA HABARI ZOTE ZA BURUDANI KUTOKA KILA KONA YA DUNIA...SAID NUHU
HABARI ZA MICHEZO
UKIWA HAPA UTAPATA HABARI ZA KILA AINA YA MICHEZO, KUANZIA MPIRA WA MIGUU, BASKETBALL, GOLF NKSAID NUHU
HABARI ZA KIMATAIFA
HAPA UTAPATA HABARI ZA KIMATAIFA KUTOKA KILA KONA YA DUNIAMore
Wednesday, May 23, 2012
MLINZI ALIEKUWA ANATETEA MCHORO WA ZUMA USIHARIBIWE AKAMATWA NA KUFUNGULIWA MASHTAKA
![]() |
| Picha za televisheni zikionedsha Lowie Mabozela akishambuliwa |
Kanali Vishnu Naidoo msemaji wa polisi alieleza:
"Amekamatwa muda mfupi uliopita "Picha za televisheni zilimuonesha mlinzi huyo akimpiga kichwa na kumbinua sakafuni mtuhumiwa Lowie Mabokela kijana mdogo aliekuwa akichafua mchoro kwa rangi nyeusi jana Jumanne
Naidoo amesema Mabokela alifungua kesi ya kushambuliwa jana usiku
![]() |
| Mabozela akivuruga rangi nyeusi kwenye mchoro wa Zuma |
![]() |
| Barend la Grange akiweka alama ya X juu ya mchoro |
![]() |
| Kijana Lowie Mabozela |
Unyama aliofanyiwa Mabokelo umezua mjadala na hasira zingine nchini Afrika Kusini
Mtuhumiwa wa pilialieharibu mchoro,Barend la Grange ambae ni profesa hakuonekana kufanyiwa unyama wakati anakamatwa
Jumba la maonesho liliendelea kuwa limefungwa leo Jumatano.Mtuhumiwa mwengine wa tatu alikamatwa akichora ukutani nje ya jengo la maonesho maneno yasemayo`RESPECT`
![]() |
| Barend la Grange |
Watuhumiwa wote watatu wamepewa dhamana baada ya kusomewa mashtaka na mahakama ya Hillbrow
Habari zingine zinasema wenye maonesho wameamua kufunga na kuondoa mchoro wa Zuma na kuupeleka sehemu salama baada ya vitisho kuzidi
Tuesday, May 22, 2012
PICHA YA JACOB ZUMA AKIWA UCHI YACHORWA NA KUWEKWA KWENYE MAENESHO,YAZUA UTATA MKUBWA
![]() |
| Picha hii inaonesha sehemu ya juu ya mchoro uliopewa jina la `The Spear `ukifananisha taswira ya rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma |
Mchoro wa picha inayomkejeli rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ukionesha mfano wa sehemu za siri za rais huyo wa taifa lenye nguvu barani Afrika, umewekwa hadharani kwenye jumba la maonesho ya picha la Goodman huko Johannesburg,Afrika Kusini na kuanzisha mjadala mkali.
Mchoro huo uliopewa jina la `The Spear`ulichorwa na kuwekwa hadharani na msanii wa michoro wa Cape Town, Brett Murray ambae amejitetea kuwa hakuwa na lengo la kumuudhi mtu yeyote ila ni njia yake ya kujieleza kisiasa kwa staili ya ucheshi,kama msanii
Mchoro huo ni sehemu ya michoro iliyo kwenye maonesho ya Murray anayoyaita `Hail to the Thief II`
Katika kuonesha kukerwa na mchoro huo,watu wawili waliingia kwenye jumba hilo na kuuharibu kwa rangi.Mtu mmoja aliweka alama ya X kwa kutumia rangi nyekundu kwenye eneo la kichwa na sehemu za siri za mchoro huo na mwengine ambae ni kijana mdogo alivurga mchoro kwa kupulizia rangi nyeusi.
Mwandishi wa BBC ambae alikuwa eneo hilo leo asubuhi aliandika kwenye Twitter:
"Mchoro wa Zuma umevurugwa kwa rangi nyeusi.Muhusika kaniambia kuwa mchoro huo ni wa kichokozi.Walinzi wamemvamia na kumkamata...mtu wa pili nae mbaroni"
Mchoro huo ulikuwa unalindwa na kampuni binafsi ya ulinzi wakati wa tukio
Baada ya kutiwa mbaroni watuhumiwa walifikishwa kwenye kituo cha polisi cha Rosebank
Mapema leo wawakilishi wa chama cha ANC walikimbilia mahakama kuu ya Gauteng mjini Johannesburg kufungua pingamizi la kuzuia jumba la Goodman lisitumie mchoro huo wenye urefu wa mita 1.85 kwenye maonesho.Na pia walikwenda kwenye ofisi za City Press kutaka picha za mchoro huo zisiwekwe mtandaoni
Polisi awali walitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuwa mitaa kadhaa kuzunguka eneo la mahakama kuu itabidi ifungwe kuruhusu wafuasi wa ANC ambao wangefika hapo kwa maandamano.Walisema mitaa hiyo itakuwa wazi ifikapo saa 9 alasiri ambapo mahakama itakuwa inafunga shughuli zake
Jumuia ya wanawake wa ANC walihimiza wanawake wenzao kuunga mkono uamuzi wa ANC kuandamana hadi mahakamani.Katika taarifa yao walisema:
"Hakuna Mwafrika Kusini yeyote,katika ofisi yoyote anaestaihili kuvunjiwa heshima namna hii na ni mtu aliekosa hekima kichwani mwake tu ndie anaeweza kudiriki kuchora mchoro kama huu.Tunatoa shutuma kali kwa kazi hii (ya Murray) na tutaendelea kuidharau kadri inavyostahili,tukitegemea Brett Murray atachukua fursa hii kujiangalia,heshima na tabia yake kama binadamu"
Chama cha ANC kiliwataka wanachama wake kukusanyika kwa wingi nje ya mahakama kuu leo kutetea utu, heshima na hadhi ya Zuma, rais wa ANC
Gazeti la Times nalo liliripoti leo asubuhim kuwa msemaji wa kanisa la Nazareth Baptist Church,Enoch Mthembu amependekeza Bret Murray apigwe mawe hadi kufa
"Huyu mtu amelitukana taifa zima na anstahili kupigwa mawe hadi afe.Alixchofanya kinaonesha ni jinsi gani alivyolelewa kibaguzi.Sanaa haiungi mkono kuwavunjia heshima binadamu wenzako"
Chama cha ANC kiliwasilisha karatasi za kimahakama kwenye jumba la maonesho na City Press ambazo zilizotolewa na mahakama siku ya Ijumaa
Karatasi hizi zinazuia pande zote mbili kuweka hadharani mchoro na picha za mchoro huo kwenye mitandao yao au mahali pengine popote
Habari kutoka kwenye jumba la maonesho la Goodman zinasema kuwa wamekataa kutii amri ya mahakama ya kuondoa mchoro huo na kusema kuwa mchoro huo watautumia hadi hapo maonesho yatakapokwisha na kuongeza kuwa kazi yao inalindwa na haki yao kikatiba ya uhuru wa kujieleza
Habari zilizopatikana mchana zinasema kuwa watuhumiwa waliokamatwa wakiharibu mchoro huo kwenye jumba la maonesho la Goodman asubuhi ya leo ,wametambuliwa kuwa ni profesa wa chuo kikuu na kijana mdogo mwenye umri wa miaka 15
Mwanasheria wajumba hilo Gregg Palmer amesema kuwa watu hao watafunguliwa kesi ya kuharibu mali.
Ripota wa kituo cha Tv cha eNews,Iman Rappetti,ambae alikuwepo leo asubuhi kwenye jumba hilo kuripoti juu ya mchoro huo uliopewa jina la `The Spear` (mkuki),alieleza jinsi alivyokabiliana na profesa aliekuwa akiharibu mchoro.
Amesema kuwa alikuwa karibu kabisa na mchoro huo wakati profesa huyo alipotoa kifaa cha kuhifadhia rangi na kuanza kuchora alama ya X kukatiza sehemu za siri za mchoro huo
Ameelezea jinsi alivyomvuta mkono kumzuia asiharibu mchoro huku akipiga kelele kuomba msaada kutoka kwa wafanyakazi wa jumba hilo
Rappetti alimuelezea mtu huyo kuwa alikuwa wa kawaida tu amevaa koti lililofumwa,lakini hakujua kuwa nyuma yake alisimama kijana mdogo kashika kasha lenye rangi nyeusi tayari kufuata nyayo za profesa.Alipiga kelele kumzuia kijana huyo alipoanza kupakaza rangi nyeusi juu ya mchoro huo
Wafanyakazi wa jumba waliwadhibiti profesa na kijana, kabla ya polisi kufika mara moja na kuwachukua.Wafanyakazi wa hapo walimwambia Rappetti kuwa, awali profesa alijitambulisha kuwa ni wa kabila la Afrikaans,lakini Rappetti ana wasiwasi kuhusu hilo
"Haonekani kama ni Mwaafrikaans"
Umati wa watu na waandishi wa habari walianza kujaa kuzunguka jengo ambalo tayari lilikuwa limeshafungwa.Ndani ya lango kuu la kuingilia walisimama walinzi watatu wa kampuni binafsi huku wameshika silaha za moto na wamevaa jaketi za kuzuia risasi.
SIRI YA AJALI YA MAFISANGO HII HAPA
Olly Elenga, ni mtoto wa dada yake
Mafisango. Yeye alishuhudia ajali hiyo jijini Dar es Salaam na ndie aliyeikimbiza
maiti ya mchezaji huyo Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam
Katika mazishi yake, watoto wake wote watatu walihudhuria ambao ni David, Patrina na Crespo aliyekuwa anaishi naye Dar es Salaam.
Crespo aliteka umati wa watu katika mazishi hayo kwani kila mmoja alitaka kumsogelea na kumtazama.
"Kilichotokea ni kwamba baada ya Mafisango kurudi Sudan, Jumanne, siku iliyofuata alizima simu kabisa akasema hataki kwenda popote. Akanipa dola 100 nipeleke kwa dada mmoja waliyekutana naye kwenye ndege jana yake kwa ajili ya kukodi gari ile iliyopata ajali, tukapewa na dereva anayeitwa Bozi. Mafisango hakuwahi kumiliki gari jijini Dar es Salaam. Lakini asubuhi ya Jumatano iliyopita (Mei 16) alimpigia simu nyota wa Yanga, Haruna Niyonzima `Fabregas' na kumwita kwake ili wajadili kuhusu mambo ya timu ya taifa ya Rwanda. Fabregas alikuja nyumbani kuanzia asubuhi na wakanywa pombe na baadaye wakaongezeka akina Redondo (Ramadhani Chombo.) "
"Wakakubaliana waende Kinondoni kwa Queen Suzy yaani yule dansa wa bendi ya FM Academia `Wana Ngwasuma', ambaye ana baa yake karibu na Mango Garden, basi ndio wakanywa hapo na baadaye mke wa Redondo, aliyewaandalia chakula akawaita nyumbani kwao ili wakale, walipofika kule wakanywa bia sana, hapo Mafisango alikuwa hapatikani kwenye simu kwani zilikuwa zinatumika simu za Redondo na marafiki wengine aliokuwa nao."
"Tulikaa sana kwa mke wa Redondo mpaka saa tano usiku. Mafisango alishalewa sana, alikuwa hafai akajilaza kitandani hapo kwa mke wa Redondo akawa ananiambia tuwashe gari twende Keko kulala lakini mke wa Redondo akamwambia 'shemeji nina hamu ya kwenda Ngwasuma' waliokuwa kwenye Ukumbi wa Maisha Club, akatuambia twende wote. Mafisango akakubali akamwambia ataenda kumfurahisha kwa heshima yake".
"Tumefika kule ndani tukanywa sana pombe akatuza wanamuziki, tulivyoondoka akang'ang'ania kuendesha gari badala ya yule Bozi (dereva) aliyekuwa anaendesha tangu mchana, tulikuwa watano kwenye gari pamoja na yeye, kila mara Bozi alikuwa anazozana na Mafisango kwa kuwa alikuwa anamwambia mbona Mafisango mbona haendeshi vizuri gari halafu iko kasi na anayumbisha usukani hautulii, yaani ilifika sehemu mpaka tunataka kumshusha yule Bozi, lakini akasema hashuki mpaka ahakikishe tumefika Keko na kupaki gari la bosi wake."
"Tulipofika pale Keko, taa zilituzuia tukasimama, zilipowaka za kijani tukaondoka lakini spidi Mafisango aliyotoka nayo pale ilikuwa kali ghafla tukavuka geti la kwanza la Veta tukaona guta mbele yetu, kwa vile gari ilikuwa kasi ikabidi Mafisango airudishe kulia kwa nguvu kumkwepa yule jamaa halafu baada ya kumpita akairudisha kushoto ndio hapo ikaingia kwenye mtaro ikapanda ikapinduka na nikachanganyikiwa nilipoona kichwa cha Mafisango kimenasa ndani kwenye sehemu ya gia halafu gari imekwisha na yule dada (rafiki wa mke wa Redondo) aliyekuwa amekaa naye mbele naye akawa kabanwa ikabidi nimtoe. "
"Pia nikamtoa na Mafisango akiwa anavuja damu na wakati huo alishafariki. Nikasimamisha taxi nikamkimbiza Muhimbili kufika pale wakanihakikisha kwamba amekufa sikuamini."
"Lakini Mafisango aliumia sana na kama si pombe aliyokunywa asingekufa."
Katika mazishi yake, watoto wake wote watatu walihudhuria ambao ni David, Patrina na Crespo aliyekuwa anaishi naye Dar es Salaam.
Crespo aliteka umati wa watu katika mazishi hayo kwani kila mmoja alitaka kumsogelea na kumtazama.
`BOBAN` AANGUKA NA KUPOTEZA FAHAMU `AIRPORT`
| BOBAN akilia kwa uchungu siku aliyokufa Mafisango |
Tukio hilo lilitokea jana Jumatatu wakati Boban akiwa anajiandaa kurudi Dar es Salaam baada ya kuhudhuria mazishi ya Patrick Mafisango aliyefariki Alhamisi iliyopita kwa ajali ya gari iliyotokea jijini Dar es Salaam.
Hali ya Boban ilibadilika ghafla akiwa uwanjani hapo na akashindwa kuona mbele kabla ya kulegea na kuanguka.
Madaktari wa uwanja huo walitumia zaidi ya saa 1:30 kumtibu Boban kabla hajarejea katika hali ya kawaida huku bado akiwa na simanzi kubwa kutokana na kifo cha Mafisango.
Boban alimwambia Mwandishi wa michezo wa gazeti la Mwanaspoti katika uwanja huo wa ndege wa Kinshasa,
"Nilimkumbuka sana Mafisango, wakati nikitafakari, nikaona ninalegea, nikashindwa kuona kitu chochote mbele na nikaanguka,"a
Daktari aliyemuhudumia Boban alisema
"Alikuwa na hali mbaya sana, mapigo ya moyo yalikuwa chini, yangeweza kuondoa maisha yake."
Licha ya kupata matibabu hayo, Boban pia alipewa kahawa kwa lengo la kuinua mapigo yake ya moyo.
Boban ambaye alikuwa rafiki mkubwa wa Mafisango ikiwa ni pamoja na kulala chumba kimoja wanapokuwa kambini Simba, aliwakilisha wachezaji wengine wa klabu hiyo katika msiba huo mjini Kinshasa.
Mwili wa Mafisango aliyekuwa akicheza nafasi ya kiungo enzi za uhai wake, ulizikwa katika makaburi ya Kinkole nje kidogo ya Kinshasa juzi Jumapili kuhitimisha safari yake ya miaka 32 ya uhai wake duniani.
Msimu huu akiwa na Simba alifunga mabao 12 akiwa ndiye kiungo pekee aliyefunga mabao mengi katika Ligi Kuu Bara alikofunga mabao 11. Jingine alifunga katika Kombe la Shirikisho.
Katika ajali yake iliyotokea eneo la Veta, Chang'ombe wakati akirejea kutoka klabu ya Maisha, alikuwa na rafiki zake ambao walipata majeraha madogo
UJAUZITO WA LULU `WACHOROPOKA`

Ujauzito wa mwigizaji nyota wa sinema Bongo ambaye yuko Gereza la Segerea, Dar es Salaam kwa tuhuma ya kuhusika na kifo cha Steven Kanumba, Elizabeth Michael 'Lulu' umedaiwa kutoka.
Kwa mujibu wa taarifa za wachunguzi kupitia chanzo cha habari hizi sababu kubwa ya mimba hiyo kutoka ni kutunga nje ya mfuko wa uzazi hali ambayo ingemletea matatizo Lulu.Chanzo kilisema bila kuainisha tukio hilo lilitokea lini:
“Nikwambie kitu, unajua wengi wanaamini Lulu ana mimba na hivi karibuini iliandikwa imefikisha miezi mitatu, ilikuwa sahihi, lakini ukweli ni kwamba kwa sasa imetoka.Sababu kubwa ni kwamba afya yake ilidorora, ukiachia ule ugonjwa wa U.T.I alioripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba anao, lakini kingine ni kuwa iligundulika ujazuito wake ulitunga nje ya mfuko wa uzazi ikawa haina jinsi, ikabidi kutolewa na kusafishwa.”
Kikiendelea kuzungumza kwa umakini mkubwa, chanzo hicho kilidai kuwa ujauzito huo ni wa tatu kuchoropoka kwa msanii huyo.
“Unajua huu unakuwa ujauzito wa tatu kwa Lulu kutoka. Kwa kweli kama si hivyo angekuwa na mtoto,” kilisema chanzo bila kuweka wazi nyingine mbili zilitoka kwa matatizo gani.
Chanzo hicho kilidai:
“Kuna wakati Lulu alikwenda China, aliporudi alikuwa na ujauzito, lakini nao ulitoka, inaonekana ana matatizo kidogo kwenye upande wa kizazi,” .Kikaendelea:
“Baada ya hapo, haukupita muda mrefu, akanasa nyingine ya mwanamuziki mmoja wa Bongo Fleva, pia hiyo nayo ikaja kutoka ya tatu ni hii ya Kanumba.”
Mchunguzi ambae alitumwa na chombo kimoja cha habari kwenda Gereza la Segerea ili kukutana na Lulu na kuzungumza naye ameelezea ugumu wa kumpata ‘laivu’ nyota huyo kutokana na ukweli kwamba kuna watu maalum watatu ambao ndio wenye ruhusa ya kumwona mtuhumiwa huyo,na si zaidi ya hao.
Hata hivyo, ‘shushushu’ huyo alifanikiwa kupata fursa ya kumjulia hali mahabusu mwingine aliyepo kwenye gereza hilo na ndipo akapata bahati ya kuonana na Lulu ambaye alionekana kuwa mnyonge.
Baada ya salamu, mchunguzi huyo alimtupia swali Lulu kuhusu afya yake na ya ujauzito alionao ambapo alijibu kwa mkato.
“Nani amekwambia mimi nina mimba?”
Baadhi ya mastaa wa sinema Bongo ambao hawakuwa tayari majina yao kutajwa, walipishana ‘kiswahili’ kuhusu kuwepo au kutokuwepo kwa ujauzito wa Lulu .
Wapo waliodai ujauzito huo ulitoka akiwa gerezani, wengine walidai ulitoka wiki moja kabla ya kifo cha Kanumba lakini wapo waliodai bado anao.
Staa wa kiume:
“Lulu hana ujauzito, ulitoka. Ninavyojua mimi, wiki moja kabla ya kifo cha marehemu (Kanumba) ndiyo ulitoka, kwa hiyo hana.”Staa wa kike:
“Lulu bado ana mimba ila ni siri sana. Lakini hata nyie wenyewe si mmeona tumbo lile? anao!”Staa wa kike:
Lulu anatarajiwa kufikishwa Mahakama Kuu ya Tanzania Mei 28, mwaka huu ili kujibu tuhuma zinazomkabili juu ya kifo cha Kanumba.
CHANZO:GLOBAL PUBLISHERS
Monday, May 21, 2012
IKWIRIRI YAGEUKA UWANJA WA VITA,MMOJA AFARIKI DUNIA
HALI siyo shwari Ikwiriri wilayani Rufiji, baada ya watu
wasiojulikana kuvamia nyumba ya Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD), kuivunja na
kuharibu mali huku wengine wakichoma moto magari na nyumba za wananchi
Taarifa zinasema kuwa, vurugu hizo ziliibuka usiku wa kuamkia juzi kutokana na mapigano kati ya wakulima na wafugaji eneo hilo.
.
Vurugu hizo zilizosababisha kuigeuza Ikwiriri uwanja mdogo wa vita zimetokana na wananchi wenye hasira kali ambao walikuwa wanapinga mauaji ya mkulima Shamte Tawangala (60) mkazi wa Ikwiriri aliyeuawa kwa kupigwa na fimbo na vijana jamii ya wafugaji waliokuwa wakichunga ng'ombe katika shamba lake.
Kamanda Mangu alisema kuwa chanzo cha mauaji hao kinaelezwa kuwa ni wachungaji hao kutaka kulishia mifugo yao kwenye shamba la mahindi la Tawangala, na alipojaribu kuwakataza walianza kumshambulia kwa fimbo maeneo mbalimbali ya mwili wake hadi kufariki dunia.
Habari zinadai kuwa, mapambano kati ya polisi na wananchi yalizuka baada ya watu kuamua kuingia barabarani kupinga kukamatwa kwa wenzao zaidi ya 20, na pia kukaidi kutimizwa kwa ombi lao la kutaka waachiwe huru.
Akizungumzia kukamatwa kwa wananchi hao, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ernest Mangu alisema watuhumiwa hao walitiwa mbaroni juzi wakati wa vurugu kati ya wakulima na wafugaji ambazo zilidumu kwa zaidi ya saa sita kupinga mauaji ya mkulima yaliyofanywa na wafugaji ambao walikimbia baada ya tukio hilo.
Kamanda Mangu alisema kuwa kabla ya watuhumiwa hao kufikishwa mahakamani juzi asubuhi, zilizuka vurugu nyingine zilizofanywa na wananchi ambao walikuwa wakishinikiza kuachiwa wenzao waliokuwa wamekamatwa.
Mangu alisema walikuwa wanashikilia watu 50 kwa tuhuma za kufanya vurugu, ikiwamo kufunga barabara na kuharibu mali kadhaa.
Alisema wanaoshikiliwa siyo wafugaji wala wakulima, hivyo kama kuna taarifa za kuwapo ulipizaji kisasi siyo sahihi kwani kati ya makundi hayo hakuna kundi lililochukuliwa zaidi ya vijana wa mjini waliokuwa wakifanya vurugu.
Chanzo cha habari hii kilishuhudia mapambano baina ya polisi waliokuwa wakiwatupia mabomu ya machozi wananchi walioonekana mbele yao, ambao nao katika kujibu mapigo waliwashambulia askari hao kwa mawe.
Polisi hao walilazimika kutumia mabomu hayo, na kufanikiwa kuwakamata watu wengi ambao walikuwa wakikimbia bila mpangilio baada ya kuzidiwa na moshi wa mabomu hayo, katika kutuliza ghasia na mapigano yaliyozuka baina ya wakulima na wafugaji yaliyozuka juzi baada ya kuuawa kwa mkulima mmoja na vijana wawili jamii ya wafugaji.
Mmoja wa wakazi wa eneo hilo alisema kuwa, shughuli zote tangu mtaa wa Kaunda hadi eneo la Mwembemhuro kuelekea bonde la Mto Rufiji, zilifungwa na magari yote yalizuiwa kuingia katikati ya mji wa Ikwiriri.
Taarifa kutoka Jeshi la Polisi zimeeleza kuwa, zaidi ya nyumba saba, duka moja na magari kadhaa yaliharibiwa katika tukio hilo.
Mangu alisema kuwa hadi sasa maofsa wa polisi Mkoa wa Pwani wakiwa na helkopta, wameweka kambi katika eneo hilo ili
.
Wakati hayo yakiendelea, watu 49 kutoka jamii ya wafugaji wamehamia na kuishi na familia zao Kituo cha Polisi Ikwiriri, kuepuka vurugu zinazoendelea mitaani ambazo juzi ziliripotiwa kupoteza maisha ya mkulima mmoja.
Ingawa polisi wanasema hali ni shwari, taarifa zilizothibitishwa na watendaji wa chini zinaeleza siyo shwari na wakati wowote vurugu zinaweza kurudi tena.
Katika eneo la Ikwiriri inakopita barabara kuu ya Dar es Salaam- Mtwara, tangu juzi biashara ya maziwa iliyokuwa ikifanywa na wake wa wafugaji haikuwapo, inadaiwa wamehofia usalama wao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ernest Mangu, alisema wanaendelea kufanya doria ili kujiridhisha.
Pia, Mangu alisema lengo la doria hizo pia ni kuhakikisha kinachosemwa na baadhi ya watu kuwa, kuna dalili za kurejea vurugu iwapo ni kweli au la.
Kuhusu madai ya ofisa mmoja wa jeshi hilo kuhamishwa kituo cha kazi siku hiyo ya tukio, Mangu alisema hana taarifa hizo.
*PICHA YA SATELLITE KWA MSAADA WA GOOGLE GEOEYE

“Ni kweli leo (juzi) asubuhi muda wa saa tatu wananchi walianza tena vurugu kushinikiza wenzao waliokamatwa na polisi waachiwe, walianza kwa kuchoma matairi, lakini vurugu hizo hazikuchukua muda mrefu kwa kuwa askari wa kutuliza ghasia tunao, na waliweza kuzima vurugu hizo na zoezi la wenzao kufikishwa mahakamani likafanyika kama lilivyopangwa,”alisema Mangu.Aidha, alisema kuwa katika vurugu hizo wapo ambao wamekamatwa, lakini idadi yao haijajulikana kwa kuwa wako kwenye mahojiano na polisi na watakapobainika watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.
Mangu alisema walikuwa wanashikilia watu 50 kwa tuhuma za kufanya vurugu, ikiwamo kufunga barabara na kuharibu mali kadhaa.
Alisema wanaoshikiliwa siyo wafugaji wala wakulima, hivyo kama kuna taarifa za kuwapo ulipizaji kisasi siyo sahihi kwani kati ya makundi hayo hakuna kundi lililochukuliwa zaidi ya vijana wa mjini waliokuwa wakifanya vurugu.
“Sisi hatujawakamata wafugaji au wakulima, katika operesheni ilikuwa ya kukamata watu waliokuwa wakifanya vurugu ndiyo tunaowashikilia, sasa ukisema kuna madai ya wafugaji kutaka kulipiza kisasi hapo nashangaa kwa maana mbili, kwanza siku ya fujo hakuna hata mfugaji mmoja aliyelipiza kisasi kwa mkulima,”alisema Mangu na kuongeza:
“Kweli wafugaji walionyesha kutii walau sheria kwa sababu, licha ya baadhi ya watu kudai wakulima wanawashambulia, wao walikuwa hawajajibu mashambulizi ndiyo maana vurugu hizi tumeweza kufanikiwa kuzizima mapema, lakini kama wafugaji nao wangeenda kuwapiga wakulima hapo sasa kazi ingekuwa ngumu.”MILIO ya mabomu ya machozi na vita ya mawe baina ya askari wa Jeshi la Polisi na wananchi, viliendelea kwa siku mbili, ambapo watu 50 wamekamatwa na kufikishwa mahakamani.
Chanzo cha habari hii kilishuhudia mapambano baina ya polisi waliokuwa wakiwatupia mabomu ya machozi wananchi walioonekana mbele yao, ambao nao katika kujibu mapigo waliwashambulia askari hao kwa mawe.
Polisi hao walilazimika kutumia mabomu hayo, na kufanikiwa kuwakamata watu wengi ambao walikuwa wakikimbia bila mpangilio baada ya kuzidiwa na moshi wa mabomu hayo, katika kutuliza ghasia na mapigano yaliyozuka baina ya wakulima na wafugaji yaliyozuka juzi baada ya kuuawa kwa mkulima mmoja na vijana wawili jamii ya wafugaji.
Mmoja wa wakazi wa eneo hilo alisema kuwa, shughuli zote tangu mtaa wa Kaunda hadi eneo la Mwembemhuro kuelekea bonde la Mto Rufiji, zilifungwa na magari yote yalizuiwa kuingia katikati ya mji wa Ikwiriri.
Taarifa kutoka Jeshi la Polisi zimeeleza kuwa, zaidi ya nyumba saba, duka moja na magari kadhaa yaliharibiwa katika tukio hilo.
Mangu alisema kuwa hadi sasa maofsa wa polisi Mkoa wa Pwani wakiwa na helkopta, wameweka kambi katika eneo hilo ili
.
Wakati hayo yakiendelea, watu 49 kutoka jamii ya wafugaji wamehamia na kuishi na familia zao Kituo cha Polisi Ikwiriri, kuepuka vurugu zinazoendelea mitaani ambazo juzi ziliripotiwa kupoteza maisha ya mkulima mmoja.
Ingawa polisi wanasema hali ni shwari, taarifa zilizothibitishwa na watendaji wa chini zinaeleza siyo shwari na wakati wowote vurugu zinaweza kurudi tena.
Katika eneo la Ikwiriri inakopita barabara kuu ya Dar es Salaam- Mtwara, tangu juzi biashara ya maziwa iliyokuwa ikifanywa na wake wa wafugaji haikuwapo, inadaiwa wamehofia usalama wao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ernest Mangu, alisema wanaendelea kufanya doria ili kujiridhisha.
Pia, Mangu alisema lengo la doria hizo pia ni kuhakikisha kinachosemwa na baadhi ya watu kuwa, kuna dalili za kurejea vurugu iwapo ni kweli au la.
Kuhusu madai ya ofisa mmoja wa jeshi hilo kuhamishwa kituo cha kazi siku hiyo ya tukio, Mangu alisema hana taarifa hizo.
*PICHA YA SATELLITE KWA MSAADA WA GOOGLE GEOEYE
Sunday, May 20, 2012
`DOGO` BOSI WA FACEBOOK,MARK ZUCKERBERG, AFUNGA NDOA KWA STAILI SIKU YA JUMAMOSI
Mwanzilishi wa mtandao wa kijamii wa Facebook, Mark Zuckerberg, amefunga ndoa siku ya Jumamosi na rafiki yake wa kike wa siku nyingi msichana mwenye asili ya China, Priscilla Chan.
Zuckerberg kijana bilionea mwenye umri wa miaka 28 alitangaza rasmi tukio hilo kwa washabiki wake wa Facebook kupitia Timeline yake
Wawili hao walianza mahusiano wakiwa Chuo Kikuu cha Harvard na wamekuwan imara kwa takriban miaka 9 sasa.Walilishana kiapo katika sherehe isiyokuwa kubwa upande wa nyuma wa nyumba yao huko Palo Alto,California.Kitendo hicho kilileta hali ya mshangao kwa wageni waalikwa wasiopungua 100,kwa mujibu wa jarida la People,kwa kuwa wengi wao walidhani ni sherehe za kuhitimu kwa Priscilla,ambae tarehe 14 mwezi huu alipata shahada ya chuo kikuu ya elimu ya afya ya watoto kutoka Chuo Kikuu cha California cha San Fransisco(UCSF)
Inasemekana Zuckerberg ndie aliebuni pete ya Priscilla ambayo ni ya kawaida tu iliyonakshiwa kidogo na chembe chembe za madini ya ruby,hata mavazi aliyovaa yalionekana kuwa `simple`
Zuckerberg kijana ambaye anasifika kwa kufanya mambo yake `simple` alitoa taarifa za tukio hilo katika hali ya kawaida sana kwa kubadilisha status ya kwenye Timeline yake kutoka `in relationship` na kuwa `married`,status ambayo watu zaidi ya laki 8 wame `like` kwa masaa 24 iliyokaa mtandaoni.Muda mfupi baadae dada wa Mark aitwae Arielle aliandika katika facebook yake "Balls.Now I`m the only unmarried Zuckerberg." Na bibi harusi Priscilla nae alimuweka Arielle kama `family member` wake mpya
Kijana Mark Zuckerberg ana hisa zenye thamani isiyopungua dola za kimarekani bilioni 20.Kampuni yake ya Facebook ambayo kwa mara ya kwanza kabisa imeingia katika biashara ya hisa,imeanza katika mnada wao wa kwanza uliofanyika Ijumaa kwenye eneo lao la Facebook Silicon Valley.Mnada wao wa awali haukwenda vyema kama matarajio ya kampuni yalivyokuwa huku kila hisa zikipnda bei kidogo tu kutoka bei ya mnada ya dola 38 kwa hisa na kuuza asilimia 25 tu ya hisa zao zote.Zaidi ya hisa milioni 576 ziliuzwa na kubadili rekodi ya soko la awali la hisa nchini Marekani.Mwaka jana Facebook iliingiza mapato ya dola za kimarekani bilioni 3.7 na kuvuna faida ya dola za kimarekani bilioni 1.Facebook ina watumiaji wamtandao huo wapatao milioni 900 duniani kote
Kuibuka kwa Facebook na kuleta maajabu ya kiutamaduni duniani kulipelekea kutengenezwa kwa filam iitwayo `Social Network` mwaka juzi.Zuckerberg alianzisha mtandao wa Facebook akiwa bwenini katika chuo alichokuwa akisoma cha Havard miaka minane iliyopita.
\
Si Zuckerberg wala Chan ambao wameongezea chochote kwenye facebook zao kuhusu ndoa yao na watu wa habari wamekuwa wakituma e-mail kwa wahusika katika kampuni ya Facebook ili kupata ufafanuzi zaidi,lakini hazijajibiwa.
Zuckerberg kijana bilionea mwenye umri wa miaka 28 alitangaza rasmi tukio hilo kwa washabiki wake wa Facebook kupitia Timeline yake
Wawili hao walianza mahusiano wakiwa Chuo Kikuu cha Harvard na wamekuwan imara kwa takriban miaka 9 sasa.Walilishana kiapo katika sherehe isiyokuwa kubwa upande wa nyuma wa nyumba yao huko Palo Alto,California.Kitendo hicho kilileta hali ya mshangao kwa wageni waalikwa wasiopungua 100,kwa mujibu wa jarida la People,kwa kuwa wengi wao walidhani ni sherehe za kuhitimu kwa Priscilla,ambae tarehe 14 mwezi huu alipata shahada ya chuo kikuu ya elimu ya afya ya watoto kutoka Chuo Kikuu cha California cha San Fransisco(UCSF)
![]() |
| Hii ni Historia yake |
Inasemekana Zuckerberg ndie aliebuni pete ya Priscilla ambayo ni ya kawaida tu iliyonakshiwa kidogo na chembe chembe za madini ya ruby,hata mavazi aliyovaa yalionekana kuwa `simple`
![]() |
| Add caption |
Kijana Mark Zuckerberg ana hisa zenye thamani isiyopungua dola za kimarekani bilioni 20.Kampuni yake ya Facebook ambayo kwa mara ya kwanza kabisa imeingia katika biashara ya hisa,imeanza katika mnada wao wa kwanza uliofanyika Ijumaa kwenye eneo lao la Facebook Silicon Valley.Mnada wao wa awali haukwenda vyema kama matarajio ya kampuni yalivyokuwa huku kila hisa zikipnda bei kidogo tu kutoka bei ya mnada ya dola 38 kwa hisa na kuuza asilimia 25 tu ya hisa zao zote.Zaidi ya hisa milioni 576 ziliuzwa na kubadili rekodi ya soko la awali la hisa nchini Marekani.Mwaka jana Facebook iliingiza mapato ya dola za kimarekani bilioni 3.7 na kuvuna faida ya dola za kimarekani bilioni 1.Facebook ina watumiaji wamtandao huo wapatao milioni 900 duniani kote
Kuibuka kwa Facebook na kuleta maajabu ya kiutamaduni duniani kulipelekea kutengenezwa kwa filam iitwayo `Social Network` mwaka juzi.Zuckerberg alianzisha mtandao wa Facebook akiwa bwenini katika chuo alichokuwa akisoma cha Havard miaka minane iliyopita.
\
Si Zuckerberg wala Chan ambao wameongezea chochote kwenye facebook zao kuhusu ndoa yao na watu wa habari wamekuwa wakituma e-mail kwa wahusika katika kampuni ya Facebook ili kupata ufafanuzi zaidi,lakini hazijajibiwa.
WASTARA AZUNGUMZIA HALI YA MUMEWE NAYE PIA AKIWA AMELAZWA
Mke wa Sajuki (Wastara) ambae yuko India kwa sasa akiwa anamuuguza mumewe (Sajuki) amezungumza kwa mara ya kwanza na mtandao wa millardayo.com kuhusu hali ya sasa ya Sajuki.
Amesema “kwa kweli hali imebadilika na ninategemea kuona hali nzuri zaidi leo (jana) ni siku ya tano toka tumekuja huku India, Sajuki amebadilika sana kwa sababu siku tulipoondoka Tanzania hali yake ilikua mbaya hata rangi alibadilika lakini kwa sasa amerudi kwenye hali ya kawaida”
Kwenye sentensi nyingine, Wastara amesema Sajuki alikua hawezi hata kuongea ukamuelewa, sasa hivi anaongea hata kwa mda wa saa moja kitu ambacho alikua hawezi kabisa na sasa hivi ameweza kukaa kabisa”
Wastara amesema “changamoto tuliyonayo ni kwamba tunahudumiwa na watu mbalimbali ukiachana na dokta, hawajui kiingereza sasa unaweza kukuta unahitaji kitu lakini hamuelewani, kitu kingine ni swala la chakula, chakula ni kipya kwetu wote wawili huku ni Asia wana vyakula vyao”
Kuhusu Ugonjwa wa Sajuki, Wastara amesema walivyoondoka Tanzania walijua wanakwenda India na Sajuki atatibiwa ugonjwa unaomsumbua moja kwa moja lakini kabla ya kufanyiwa chochote ikagundulika kwamba alikua na tatizo la pumzi hivyo haikuwezekana kutibiwa ugonjwa wake kwa sababu inatakiwa kabla ya kufanyiwa opareshen anatakiwa kuwa kwenye hali ya kawaida, kwa hiyo ametibiwa kwanza tatizo la pumzi ili aweze kuhema vizuri ndio aanze kutibiwa ugonjwa wake”
Kwa kumalizia Wastara amesema “mimi pia nilipofika tu India nilikua mdhaifu, nilipoteza Network zote ikabidi nilazwe kwa sababu nilikua hoi, hapa yenyewe nimelazwa lakini naendelea vizuri
SOURCE:millardiayo.com
Subscribe to:
Posts (Atom)