Edgar
Davis Mosha mtoto wa mfanyabiashara tajiri na maarufu boss wa kampuni
ya DELINA, Bwana Davis Mosha amehojiwa na VOA (Voice of America). Edgar na
baba yake wametua kwa kishindo nchini Marekani wakitokea Uingereza
ambapo Edgar amepeperusha vyema bendera ya Tanzania kwa kuitwa kufanya
majaribio na klabu ya Chelsea ya Uingereza..
HABARI ZAKISIASA
UTAPATA HABARI MBALIMBALI ZA KISIASA KUTOKA NDANI NA NJE YA NCHI, UKIWA HAPAHAPASAID NUHU
HABARI ZA BURUDANI
UKIWA HAPA UTAPATA HABARI ZOTE ZA BURUDANI KUTOKA KILA KONA YA DUNIA...SAID NUHU
HABARI ZA MICHEZO
UKIWA HAPA UTAPATA HABARI ZA KILA AINA YA MICHEZO, KUANZIA MPIRA WA MIGUU, BASKETBALL, GOLF NKSAID NUHU
HABARI ZA KIMATAIFA
HAPA UTAPATA HABARI ZA KIMATAIFA KUTOKA KILA KONA YA DUNIAMore
Showing posts with label michezo. Show all posts
Showing posts with label michezo. Show all posts
Sunday, July 28, 2013
Wednesday, July 17, 2013
MKONGWE GEORGE MASATU ALILIA KURUDI SIMBA
ALIYEKUWA mchezaji wa Simba miaka kumi na tano iliyopita George Magere Masatu, amesema kuwa kwa sasa yuko tayari kurejea kwenye timu hiyo.
Masatu hivi sasa amerejea nchini akiwa tayari amestaafu soka lakini ana kadi ya uanachama wa timu hiyo yenye maskani yake Msimbazi jijini Dar es Salaam.
Masatu amesema kuwa yuko tayari kurejea kama kocha na siyo mchezaji tena kama ilivyokuwa awali Masatu alisema kuwa, ana uwezo na uzoefu kufundisha aliyoupatia katika shule ya soka ya Arsenal huko Indonesia alikokuwa akicheza soka la kulipwa kwa zaidi ya miaka mitano.
“Kweli nimerudi nyumbani kuendelea na maisha, lakini ukisema kuhusu Simba mimi ni mwanachama.Na kama wakisema nifanye nao kazi,niko tayari haina shida
“Nimekuwa kocha kwenye shule ya watoto ya Arsenal kule Indonesia kwa zaidi ya miaka mitatu. Ninajua kazi inavyofanyika na wakisema wanataka tufanye kazi, basi tutafanya hivyo,” alisema Masatu aliyekuwa beki kisiki wakati wa enzi zake.
Masatu alianza kufanya vizuri akiwa na Pamba ya Mwanza kabla ya kujiunga na Simba mwanzoni mwa miaka ya 1990.
Pamoja na kuwa na umbo dogo, Masatu alikuwa ndiye beki nyota na imara zaidi wa kati nchini na jina lake halijawahi kushuka chati pamoja na kuwa nje ya Tanzania kwa muda mrefu.
USHINDI WA ARSENAL WAFANYIWA PROPAGANDA ZA KISIASA INDONESIA
![]() |
| Sege Gnaby wa Arsenal akikwepa daruga la mchezaji wa Indonesia, Roby |
Mgombea urais katika uchaguzi wa Rais wa 2014 kupitia Chama cha Great Indonesia Movement Party (Gerindra) Jenerali mstahafu Prabowo Subianto ameutumia mchezo kati ya timu ya taifa ya nchi hiyo na Arsenal kuishambulia serikali iliyo madarakani katika hotuba ya mkutano wa Kampeni za uchaguzi wa Rais wa nchi hiyo wa mwaka 2014
Baada ya timu ya taifa ya Indonesia kupokea kipigo cha goili 7-0 kutoka Gunners mgombea Prabowo aliilaumu serikali kwa kutoisimamia vizuri timu hiyo na kuahidi iwapo ataingia madarakani kama rais wa Indonesia atahakikisha kikosi cha timu ya taifa kinafanya vizuri katika mechi zake
"
Iweje hata timu yetu ya taifa inashindwa kwenye mechi na wachezaji 11 wa ngazi ya klabu.Tutahakikisha tunalipa umuhimu wa pekee suala zima la timu ya taifa.Kwa hiyo ninachofikiri ni kwamba matatizo haya yanasababishwa na udhaifu katika uendeshaji,na uwezo mdogo wa kufikiri.Matatizo katika uongozi.Tunataka Indonesia iwe na timu ya taifa iliyo imara"
Jenerali Prabowo ambaye aliwahi kuwa askari wa kikosi maalum,aliwahi kuwania kiti cha umakamu wa rais 2009 ambapo alibwagwa na mpinzani wake Megawati Sukamoputri.Ni mmoja kati ya wagombea wanaopewa nafasi kubwa ya kuingia ikulu ya nchi hiyo ya mashariki ya mbali 2014
Saturday, July 13, 2013
VITA UWANJA WA TAIFA JIONI YA LEO
LEO, kuanzia saa 9 alasiri,Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, inatinga Uwanja wa Taifa Jijini
Dar es Salaam kucheza na wenzao, Uganda Cranes, kusaka nafasi ya
kucheza Fainali za CHAN, African Nations Championship, zitakachezwa
kuanzia Januari 10 hadi Februari 1, 2014 huko Afrika Kusini.
Mashindano haya yalianza kuchezwa huko
Nchini Ivory Coast Mwaka 2009 na Tanzania ilishiriki Fainali hizo na
yanahusisha Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wanaocheza Ligi za ndani ya
Nchi zao pekee.
Wachezaji wanaocheza Soka nje ya Nchi zao hawaruhusiwi kushiriki.
KUMBUKUMBU:
CHAN 2009
Tanzania walishiriki Fainali za Kwanza
za CHAN Mwaka 2009, wakiwa chini ya Kocha Marcio Maximo, huko Nchini
Ivory Coast wakiwa Kundi A pamoja na Wenyeji Ivory Coast, Zambia na
Senegal na kumaliza Nafasi ya 3.
Katika Mechi hizo za CHAN Tanzania ilifungwa na Senegal 1-0, kuifunga Ivory Coast 1-0 na kutoka sare 1-1 na Zambia.
AFCON 1980
Tanzania haijawahi kufuzu kucheza
Fainali za AFCON tangu Mwaka 1980 walipocheza huko Nchini Nigeria, chini
ya Kocha kutoka Poland Slawomir Wolk, wakiwa Kundi moja na Wenyeji
Nigeria, Egypt na Ivory Coast ambako walifungwa Mechi ya kwanza 3-1 na
Nigeria, 2-1 na Egypt na kutoka 1-1 na Ivory Coast.
Kikosi cha Uganda tayari kipo Nchini
kikiwa na Kocha wao Sredojvic Micho na jana kwenye Mkutano wa Waandishi
wa Habari Kocha huyo alisema Taifa Stars imekuwa ikifanya vizuri tangu
iwe chini ya Kim, na itakuwa na Wachezaji tisa wa Kikosi cha Kwanza
kinachocheza Mechi za Mchujo za Kombe la Dunia wakati kwa upande wake
atakuwa na Wachezaji wawili tu.
Pia Kambi ya Uganda imekuwa ikilalamikia
joto kali la Jiji la Dar es Salaam ambapo wao kwao wamezoea hali ya
wastani wa Nyuzijoto 25 wakati wamekumbana na Joto la zaidi ya Nyuzijoto
30.
Kwenye Mechi ya leo Uganda Cranes
wanatarajiwa kutumia Mfumo wa 4-3-3 kwa mujibu wa Mdau wao mmoja
aliekuwepo wakati Timu hiyo ikifanya Mazoezo wa Uwanja wa Karume, Dar es
Salaam.
VIINGILIO:
-Sh. 5,000 kwa Viti vya rangi ya kijani [Viti 19,648]
-Sh. 7,000 Viti vya rangi ya bluu [Viti 17,045]
-Sh. 10,000 Viti vya rangi ya chungwa [Viti 11,897]
-Sh. 15,000 VIP C [Viti 4,060]
-Sh. 20,000 VIP B [Viti 4,160.]
-Sh. 30,000 VIP A [Viti 748]
TAHADHARI:
Washabiki wanakumbushwa
kutonunua Tiketi mikononi mwa Watu au katika maeneo yasiyohusika ili
kuepuka kununua Tiketi bandia, hivyo kukosa fursa ya kushuhudia mechi
hiyo.
++++++++++++++++++++++++++++++++
Nae Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen,
alisema ni muhimu kwao kushinda Mechi hii ili kujiweka katika mazingira
mazuri kwa ajili ya Marudiano lakini pia alisema Uganda ndiyo
inayoongoza kwa Ubora wa Viwango vya FIFA katika ukanda huu wa Afrika
Mashariki na Kati, na hivyo ni changamoto kwao.
Kim Poulsen pia alisema Wachezaji wake tayari wamejipanga vizuri kwa ajili ya Mechi hiyo.
Hapo Jana, Rais wa TFF, Leodegar Tenga,
aliitembelea Kambi ya Taifa Stars kwenye Hoteli ya Tansoma, Dar es
Salaam na kuwapa moyo Wachezaji kwa kuwaambia kuwa kiwango walichoonesha
kwenye Mechi zilizopita za Mchujo za Kombe la Dunia dhidi ya Morocco na
Ivory Coast kimetoa uhakika wa uwezo wao wa kushindana katika
Mashindano yoyote, kwani tayari wameiva.
Rais Tenga, akiwahimiza Wachezaji
kupigana kwa ajili ya Tanzania, alitamka: “Kiwango mlichoonyesha katika
mechi hizo kila Mtanzania anayewafuatilia amekiona, hivyo hatuna shaka
kuwa mtatuwakilisha vizuri kwenye mechi ya kesho dhidi ya Uganda.”
CHAN 2014
RATIBA
KANDA KASKAZINI
(Timu 2 zitafuzu)
05-07/07/13: Tunisia v Morocco
26-27/07/13: Morocco v Tunisia
Algeria v Libya - Imefutwa
Libya watacheza Fainali huko South Africa baada Algeria kujitoa.
KANDA MAGHARIBI A
(Timu 2 zitafuzu)
Raundi ya Awali
30/11/12-2/12/12 : Liberia 0-1 Mauritania; Guinea 0-0 Sierra Leone
14-16/12/12: Mauritania 2-1 Liberia; Sierra Leone 1-1 Guinea
Mauritania wamepita Jumala ya Bao 3-1
Guinea wamepita kwa Magoli ya Ugenini
Raundi ya 1
05-07/07/13: Senegal v Mauritania; Mali v Guinea
26-27/07/13 : Mauritania v Senegal; Guinea v Mali
KANDA MAGHARIBI B
(Timu 3 zitafuzu)
Raundi ya Awali
30/11-2/12/12/12: Burkina Faso 2-1 Togo
14-16/12/12: Togo 0-1 Burkina Faso
Burkina Faso wamepita Jumla ya Bao 3-1
Raundi ya 1
05-07/07/13: Benin v Ghana; Nigeria v Ivory Coast; Burkina Faso v Niger
26-27/07/13: Ghana v Benin; Ivory Coast v Nigeria; Niger v Burkina Faso
KANDA KATI
(Timu 3 zitafuzu)
Raundi ya Awali
Central African Republic v Congo - cancelled
Congo inasonga baada ya kujitoa Central African Republic
Raundi ya 1
05-07/07/13: Cameroon v Gabon; DR Congo v Congo
26-27/07/13: Gabon v Cameroon; Congo v DR Congo
Washindi watatinga Fainali
Mchujo Raundi ya 1
Watakaofungwa Mechi za Raundi ya 1 watapambana kati ya Tarehe 26-28/07/13 na 09-11/08/13 na Washindi wawili kusonga Fainali.
KANDA KATI MASHARIKI
(Timu 3 zitafuzu)
Raundi ya Awali
14-16/12/12: Burundi 1-0 Kenya; Eritrea v Ethiopia ( Ethiopia wamesonga baada Eritrea kujitoa)
06/01/13: Kenya 0-0 Burundi (Burundi wamesonga Jumla ya Bao 1-0)
Raundi ya 1
05-07/07/13: Burundi v Sudan
12-13/07/13: Ethiopia v Rwanda; Tanzania v Uganda
26-27/07/13: Sudan v Burundi, Rwanda v Ethiopia, Uganda v Tanzania
KANDA KUSINI
(Timu 3 zitafuzu pamoja na Wenyeji South Africa)
Raundi ya Awali
30/11-2/12/12 : Mauritius 2-0 Comoros
14-16/12/12: Comoros 0-0 Mauritius
Mauritius yasonga Jumla ya Bao 2-0
Raundi ya 1
23/06/2013: Swaziland 0-1 Angola
29/06/2013: Angola 1-0 Swaziland
Angola yasonga Jumla ya Bao 2-0
26-7/07/13: Mauritius v Zimbabwe; Mozambique v Namibia; Botswana v Zambia
02-04/08/13: Zimbabwe v Mauritius, Namibia v Mozambique; Zambia v Botswana
Raundi ya 2
26-28/07/13 : Mechi za Kwanza
09-11/08/13: Mechi za Pili
Raundi ya 2
Washindi wawili wa Raundi ya 2 wanaungana na Wenyeji South Africa kucheza Fainali.
Mshindi Mauritius/Zimbabwe v Mshindi Mozambique/Namibia
Botswana/Zambia v Angola
Thursday, July 11, 2013
BREAKING NEWS: ..ROONEY AUMIA MAZOEZINI KURUDISHWA NYUMBANI HARAKA
Klabu ya Manchester United imetoa taarifa za kuumia kwa mshambuliaji wake Wayne Rooney leo na kwamba katika uchunguzi wa scan uliofanyika jioni hii umeonesha kuwa amepata matatizo kwenye misuli ya paja
Kutokana na ugunduzi huo klabu imeamua kumrudisha nyumbani Uingereza kutoka ziarani ,ili kumfanyia uchunguzi wa kina na matibabu yanayostahili
Wednesday, July 10, 2013
HII NDIO AKAUNTI RASMI YA TWITTER ILIYOFUNGULIWA NA KLABU YA MANCHESTER UNITED

BABA MZAZI WA JOHN TERRY NAE ASHITAKIWA KWA UBAGUZI
Gazeti la Daily Mirror leo limebeba habari kuwa baba wa nyota wa timu ya soka ya Chelsea ya Uingereza John Terry amefikishwa mahakamani kwa kile kilichoelezwa kuwa `shambulio lililotokana na ubaguzi` na pia ameshtakiwa kwa kutishia kumuumshambulia mtu mwingine kutokana na hisia za kibaguzi.Makosa yote hayo aliyafanya kwenye tukio moja,ugomvi uliotokea katika mtaa mmoja jijini London.
Mzee Terry mwenye umri wa miaka 59,alitiwa mbaroni Machi 22 mwaka huu baada ya kutokea ugomvi aktika mtaa mmoja uitwao Frenchurch ndani ya jiji la London,nchini Uingereza.
Alisomewa mashtaka yake leo asubuhi katika kituo cha Polisi cha Bishopsgate wakati akiripoti kwenye dhamana aliyopewa.Watu wengine wawili,Tudor Musteata,47, na Stephen Niland wanahusishwa katika kesi hiyo na watafikishwa mahakamani kujibu kesi tarehe 23 mwezi huu katika mahakama ya jiji la London.
Polisi wamethibitisha kuwepo kwa kesi hiyo lakini hawakutoa maelezo zaidi.
Kesi hiyo ya Terry mkubwa imekuja ikiwa ni mwaka tu tangu mtoto wamzee Terry John afutiwe mashtaka mahakamani kutokana na kesi iliyomkabili ya kumtolea lugha ya kibaguzi mchezaji wa Queen`s Park Rangers Anton Ferdinand mdogo wa Rio Ferdinand wa Manchester United

John Terry alikanusha kumtolea lugha hiyo Anton Ferdinand wakati wa mechi kati ya Chelsea na QPR mwaka juzi
Lakini Chama cha Soka cha Soka cha Uingereza kilipingana na maamuzi ya mahakama ya kumtoa hatiani John Terry na kudai kuwa utetezi wa Terry ulikuwa ni wa `kutunga na usioendana na tukio`,wakamfungia mechi nne.Terry hakukata rufaa FA na aliomba radhi kwa kosa lake la kutumia lugha isiyofaa.
Lakini alishutumiwa kwa kutomtaka radhi Anton Ferdinand mwenyewe na Chelsea nao walilaumiwa kwa kuendelea kumuachia Terry unahodha wa timu.
Katika miaka ya nyuma ,2002,John Terry akiwa na wachezaji wengine wawili,alifunguliwa mashataka ya kuvunja amani baada ya kuibua zogo dhidi ya baunsa kwenye klabu ya starehe usiku.Aliondolewa mashtaka baadae.
Mzee Terry mwenye umri wa miaka 59,alitiwa mbaroni Machi 22 mwaka huu baada ya kutokea ugomvi aktika mtaa mmoja uitwao Frenchurch ndani ya jiji la London,nchini Uingereza.
Alisomewa mashtaka yake leo asubuhi katika kituo cha Polisi cha Bishopsgate wakati akiripoti kwenye dhamana aliyopewa.Watu wengine wawili,Tudor Musteata,47, na Stephen Niland wanahusishwa katika kesi hiyo na watafikishwa mahakamani kujibu kesi tarehe 23 mwezi huu katika mahakama ya jiji la London.
Polisi wamethibitisha kuwepo kwa kesi hiyo lakini hawakutoa maelezo zaidi.
Kesi hiyo ya Terry mkubwa imekuja ikiwa ni mwaka tu tangu mtoto wamzee Terry John afutiwe mashtaka mahakamani kutokana na kesi iliyomkabili ya kumtolea lugha ya kibaguzi mchezaji wa Queen`s Park Rangers Anton Ferdinand mdogo wa Rio Ferdinand wa Manchester United

John Terry alikanusha kumtolea lugha hiyo Anton Ferdinand wakati wa mechi kati ya Chelsea na QPR mwaka juzi
Lakini Chama cha Soka cha Soka cha Uingereza kilipingana na maamuzi ya mahakama ya kumtoa hatiani John Terry na kudai kuwa utetezi wa Terry ulikuwa ni wa `kutunga na usioendana na tukio`,wakamfungia mechi nne.Terry hakukata rufaa FA na aliomba radhi kwa kosa lake la kutumia lugha isiyofaa.
Lakini alishutumiwa kwa kutomtaka radhi Anton Ferdinand mwenyewe na Chelsea nao walilaumiwa kwa kuendelea kumuachia Terry unahodha wa timu.
Katika miaka ya nyuma ,2002,John Terry akiwa na wachezaji wengine wawili,alifunguliwa mashataka ya kuvunja amani baada ya kuibua zogo dhidi ya baunsa kwenye klabu ya starehe usiku.Aliondolewa mashtaka baadae.
Monday, July 8, 2013
BAYERN YATANGAZA RASMI MARIO GOMEZ KUJIUNGA NA FIORENTINA
Mabingwa Soka Barani Ulaya kwa ngazi ya vilabu,Bayern Munich imetangaza rasmi kuachana na mshambuliaji Mario Gomez na kwamaba wamefikia makubaliano na timu ya Forentina ya Italia ambao wamekuwa wakimfuatilia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kwa muda sasa.Mchezaji huyo alipokonywa nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza cha Mabingwa hao wa Ujerumani na mshambuliaji mwingine Mario Mandzukic.
Wiki iliyopita Bayern walisema kuwa mpango wa Gomez kwenda Fiorentina umekufa huku ikiripotiwa kuwa Fiorentina hawakuwa tayari kutoa kitita cha euro milioni 20 walizotaka Bayern.
Mkurugenzi wa mawasiliano wa Bayern amesema uhamisho wa mchezaji huyuamabao unatajwa kuwa utakuwa hadi 2017, utasainiwa katika wiki moja au mbili zijazo na katika mkataba wake Gomez anatarajiwa kuvuna kitita cha euro milioni 4 kila msimu Gazeti moja la Italia Gazetta Dello Sport limandika kuwa Fiorentina watatoa euro milioni 15 kumnyakua mchezaji huyo
Mkataba wa Gomez na Bayern ulikuwa unaenda hadi 2016,lakini katika kile kilichoelezwa kukasirishwa kwa fowadi huyo na kitendo cha kutopangwa mechi nyingi za msimu uliopita.Kocha Jupp Heynckes alikuwa akimtumia Mandzukic mara kwa mara.Aliomba auzwe timu nyingine ili apate nafasi ya kucheza na kujihakikishia nafasi ya kwenda Kombe La Dunia Brazil 2014 .
Ingawaje hakupngwa mechi nyingi Gomez alifanikiwa kufikisha idadi ya magoli 19 msimu ulioisha yakiwamo mawili aliyofunga kwenye fainali ya Kombe la Ujerumani
Mchezaji huyo amebatizwa jina la Super Mario,linalotokana na kikaragosi cha kwenye mchezo wa kompyuta.Alijiunga na Bayern Miunich mwaka 2009 akitokea VfB Stuttgart kwa ada ya uhamisha ya euro milioni 35.Ameifungia timu ya taifa ya Ujerumani magoli 25 katika mechi 58 alizocheza.
Wiki iliyopita Bayern walisema kuwa mpango wa Gomez kwenda Fiorentina umekufa huku ikiripotiwa kuwa Fiorentina hawakuwa tayari kutoa kitita cha euro milioni 20 walizotaka Bayern.
Mkurugenzi wa mawasiliano wa Bayern amesema uhamisho wa mchezaji huyuamabao unatajwa kuwa utakuwa hadi 2017, utasainiwa katika wiki moja au mbili zijazo na katika mkataba wake Gomez anatarajiwa kuvuna kitita cha euro milioni 4 kila msimu Gazeti moja la Italia Gazetta Dello Sport limandika kuwa Fiorentina watatoa euro milioni 15 kumnyakua mchezaji huyo
Mkataba wa Gomez na Bayern ulikuwa unaenda hadi 2016,lakini katika kile kilichoelezwa kukasirishwa kwa fowadi huyo na kitendo cha kutopangwa mechi nyingi za msimu uliopita.Kocha Jupp Heynckes alikuwa akimtumia Mandzukic mara kwa mara.Aliomba auzwe timu nyingine ili apate nafasi ya kucheza na kujihakikishia nafasi ya kwenda Kombe La Dunia Brazil 2014 .
Ingawaje hakupngwa mechi nyingi Gomez alifanikiwa kufikisha idadi ya magoli 19 msimu ulioisha yakiwamo mawili aliyofunga kwenye fainali ya Kombe la Ujerumani
Mchezaji huyo amebatizwa jina la Super Mario,linalotokana na kikaragosi cha kwenye mchezo wa kompyuta.Alijiunga na Bayern Miunich mwaka 2009 akitokea VfB Stuttgart kwa ada ya uhamisha ya euro milioni 35.Ameifungia timu ya taifa ya Ujerumani magoli 25 katika mechi 58 alizocheza.
Sunday, July 7, 2013
USAIN BOLT KUCHEZEA MANCHESTER UNITED!
![]() |
| Usain Bolt |
Mwanariadha huyo, ambaye inasemekana ndie binadamu mwenye kasi kuliko wote duniani,atakuwepo katika kikosi kitakachomenyana na timu ya Seville kutoka Hispania,katika dimba la Old Trafford, siku ya tarehe 9 mwezi ujao.
"Matamanio yake sasa yatatimia,Bolt atakuwemo kwenye kikosi na kucheza sambamba na Rio.Utakuwa mchezo wa aina yake,kwa kuwa watu watapendeza kuona kama kasi yake inaweza kwenda na uwezo wake wa kumiliki mpira."Kimeongea chanzo cha ndani ya klabu hiyo.Uteuzi wa Bolt kwenye kikosi hicho unatarajiwa kutangazwa wiki ijayo.
Saturday, July 6, 2013
REFA NA MCHEZAJI WAUAWA KINYAMA BRAZIL
Baada ya kwisha kwa pilikapilika za Kombe la Mabara nchini Brazil,sambamba na vurugu mitaani,huku nchi hiyo kubwa ya Amerika ya Kusini ikikabiliwa na changamoto nyingine ya kuwa mwenyeji wa mashindano yajayo ya Kombe la Dunia 2014,nchi hiyo imeingia kwenye taswira mbaya-kwa mara nyingine-baada ya kuripotiwa kutokea mauaji ya kutisha ya mchezaji na mwamuzi katika mechi mjini Maranhao ,kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Taarifa zinasema kuwa Otávio Jordão da Silva ambae alikuwa mwamuzi wa mechi hiyo na ambae alikuwa akishambuliwa kwa matusi muda wote wa mechi, alichomoa kisu baada kumaliza mechi na kisha kumchoma nacho mchezaji mmoja mwenye umri wa miaka 31 aitwae Josemir Santos na kumsababishia majeraha ambayo hatimae yalisababisha kifo chake.
Ndugu na marafiki wa mchezaji huyo walipogundua kuwa Santos ameshafariki,walilipiza kisasi kwa kumchoma kisu mwamuzi huyo,ambae baadae kundi la watu liliendelea kumpiga,na kummalizia kwa kumkata vipande vipande na kunyofoa kichwa chake kabla hawajakichomeka kwenye mti na kukiweka kama bendera katikati ya uwanja.
Hakuna taarifa zaidi juu ya tukio hilo, lakini picha zilizowekwa mtandaoni na mtandao wa 101GREAT GOALS zimethibitisha kutokea kwa tukio hilo
Taarifa zinasema kuwa Otávio Jordão da Silva ambae alikuwa mwamuzi wa mechi hiyo na ambae alikuwa akishambuliwa kwa matusi muda wote wa mechi, alichomoa kisu baada kumaliza mechi na kisha kumchoma nacho mchezaji mmoja mwenye umri wa miaka 31 aitwae Josemir Santos na kumsababishia majeraha ambayo hatimae yalisababisha kifo chake.
Ndugu na marafiki wa mchezaji huyo walipogundua kuwa Santos ameshafariki,walilipiza kisasi kwa kumchoma kisu mwamuzi huyo,ambae baadae kundi la watu liliendelea kumpiga,na kummalizia kwa kumkata vipande vipande na kunyofoa kichwa chake kabla hawajakichomeka kwenye mti na kukiweka kama bendera katikati ya uwanja.
Hakuna taarifa zaidi juu ya tukio hilo, lakini picha zilizowekwa mtandaoni na mtandao wa 101GREAT GOALS zimethibitisha kutokea kwa tukio hilo
![]() |
| Marehemu Josemir Santos Abreu |
Friday, July 6, 2012
IJUE TEKNOLOJIA MPYA YA GOLINI KWA UFASAHA
![]() |
| Hawk-Eye |
Washabiki wa soka wanaofuatilia kwa makini Ligi Kuu ya
Uingereza Premier League,wataanza kuiona teknolojia ya golini ikitumika kwenye
ligi hiyo ifikapo mwezi Januari mwakani baada ya Bodi ya Kimataifa ya Vyama vya
Soka Ulimwenguni (IFAB) kutia tiki matumizi ya teknolojia hiyo katikati ya
wiki.
IFAB(International FA Board)imeingiza teknolojia hiyo kuwa
moja ya sheria zitakazoendesha mchezo huo,na kufungua ukurasa mpya kabisa
katika historia ya mchezo huo unaopendwa zaidi duniani
Mifumo miwili ya teknolojia hiyo ndio iliyopitishwa na
kuruhusiwa kutumika baada ya majaribio mengi ya kisayansi kuwa
yamefanyika.Mifumo hiyo Hawk-Eye na GoalRef inafanya kazi hivi:
HAWK-EYE.
Ni mfumo unaotegemea kamera,ambao ulitengenezwa na kampuni
ya Uingereza ya Hawkeye,na kununuliwa na kampuni ya Kijapan ya Sony mwaka jana,teknolojia
ambayo kwa muda imekuwa ikisaidia maamuzi kwenye michezo ya kriketi na tennis
Kamera 6 au 7 zenye uwezo wa kupiga picha kwa kasi ya ajabu
zitafungwa pande zote mbili za uwanja na nyingine juu,zitakuwa na kazi ya kufuatilia
mpira kila utakapokwenda ndani ya uwanja,kompyuta yenye uwezo wa kusoma taarifa
kwa usahihi wa hali ya juu itakuwa ikipokea picha kutoka kwenye kamera
hizo,kuzitafsiri kwa kasi na hapo hapo kutuma matokeo kwenye kifaa mfano wa saa
ambacho mwamuzi atavaa mkononi kama kinavyoonekana pichani.
Kitu ambacho badomkinatia shaka ni iwapo kamera hizo
zitafanya kazi kwa ufanisi iwapo mpira utakuwa umekumbatiwa na golikipa katika
jitihada za kuwahi kuokoa.
Ingekuwa jambo zuri iwapo picha zinazotoka kwenye kamera
hizo zingerushwa kwenye `replay`(picha za marudio) za kwenye TV pale unapotokea
utata ili na sisi watazamaji tushuhudie jinsi teknojia hiyo inavyofanya
kazi,lakini bahati mbaya FIFA wamesisitiza kuwa picha hizo hazitaoneshwa, si
kwenye TV za uwanjani tu, hata majumbani!Kitu pekee kitakachofanyika ni mwamuzi
wa mchezo kupewa ishara na kifaa alichovaa iwapo mpira utavuka mstari wa goli.
![]() |
| GoalRef |
GOALREF
Teknolojia hii ina mfumo uliobuniwa kwa ushirikiano wa
wataalam wa Denmark na Ujerumani,na imeundwa kwa mfumo wa sumaku maalum ambayo
inauwezo wa kugundua iwapo mpira utavuka mstari wa goli.
Kamba maalum ndogo
ndogo 3 zenye sumaku zinawekwa kwa ndani kwenye mpira eneo kati ya gozi na
blada na mpira utnapo vuka mstari wa goli sumaku hii iliyo ndani ya mpira hutoa
ishara kwenye vifaa maalum (sensor) vilivyowekwa ndani ya nguzo ya juu na zile
mbili za goli.
Zile sensor zinapopata taarifa kutoka kwenye sumaku huwa
kama zimetekenywa na kutoa aina ya mawimbi ya umeme ambayo bila kuchelewa
hudakwa na kompyuta ambayo nayo hupeleka taarifa kwenye kifaa kama saa
atakachovaa mwamuzi mkononi mwake..yote hayo niliyoyataja hufanyika chini ya
sekunde moja!
Hii teknolojia ya GoalRef inatarajiwa kuwa na gharama kidogo
katika kununua na kuifunga kuliko ile ya Hawk-Eye,lakini kampuni
zinazotengeneza mipira bado zinajishauri iwapo ni sahihi kuweka sumaku ndani ya
mipira yao,ila wataalam wa GoalRef
wanaendelea kutoa ushawishi wa kitaalam kuthibitisha kuwa hakuna tatizo.
…………………JE UNA MAONI GANI MSHABIKI WA SOKA?
Thursday, June 21, 2012
TAARIFA: KAGAWA KUFANYIWA VIPIMO OLD TRAFFORD KESHO
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana,Shinji Kagawa anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya kesho Ijumaa pale Old Trafford ili dili lake la kujiunga na Manchester United kwa paundi milioni 17 liweze kukamilika.
Endapo Kagawa atathibitishwa kuwa fiti,Manchester United watakuwa na jukumu la kumtafutia kibali cha kufanya kazi nchini Uingereza,na baada ya hapo kila kitu kitakuwa kimekamilika.
Lakini, ili kibali kipatikane, Kagawa anatakiwa awe ameshaichezea Japan asilimia 75 ya mechi za kimataifa kwa mwaka uliopita,lakini Kagawa hana sifa hiyo,hivyo basi sifa pekee ambayo Manchester United wanaweza kuitumia kupata kibali ni ile ya kipaji cha ziada,ambayo hata Arsenal waliitumia kwa Miyachi,mchezaji mwingine kutoka Japan.
Shinji Kagawa amaepata mafanikio katika misimu miwili iliyocheza kwenye ligi kuu ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga.Ameichezea Borussia Dortmund mechi 71 na kufunga magoli 29,amechangia magoli 15,amebeba kombe la ligi kuu (Bundesliga) mara mbili na kombe la Ujerumani mara moja.
Thursday, June 14, 2012
HII NDIO BARUA YA ORLANDO PIRATES YA KUMUITA OKWI
Klabu ya Orlando Pirates ya Afrika Kusni
imetuma barua ya kumtaka mchezaji wa Simba Sports Club ya Tanzania, Emmanuel Okwi
kwenda nchini Afrika Kusni kwa ajili ya kufanya majaribio ili kuona kama anaweza
kujiunga na timu hiyo
Barua hiyo inatoa maelekezo kwamba Okwi atapewa majaribio
ya wiki mbili na Orlando Pirates, huku akipewa huduma kuanzia
malazi, matibabu, usafiri pamoja na gharama nyingine zitakazojitokeza wakati akiwa huko.
Ni misimu miwili sasa Orlando wamekuwa wakimfuatilia Okwi
ambaye klabu yake ya sasa, Simba, imeimesema ana thamani ya Tshs Billioni 2.Simba ilifikia hatua ya kutangaza thamani ya mchezaji wao huyo tegemeo,baada ya kuzuka habari mwanzoni mwa mwezi Juni kuwa Yanga wamemsajili mshambuliaji huyo raia wa Uganda.
Tuesday, June 12, 2012
Sunday, June 10, 2012
Thursday, May 31, 2012
OKWI ANA THAMANI YA SHILINGI BILIONI 2-SIMBA
Klabu ya Simba imewataka baadhi ya timu kuacha tabia ya kutaka
kutangaza kuwa wanamchukua mchezaji Emmanuel Okwi wakati wakijua ni mchezaji halali wa klabu hiyo.
Ofisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga, alisema kuwa kuna baadhi ya watu wameanza kutumia jina la Okwi kama njia ya kupata uongozi au kuonekana bora katika klabu zao huku zikiwa hazijawahi hata siku moja kufanya maongezi na klabu ya Simba.
Alisema kama kuna klabu inataka kumsajili mchezaji huyo ifuate utaratibu wa kuongea na viongozi wake kwa kuwa mchezaji huyo bado ni mali ya Simba.
Aliongeza kuwa kama kuna klabu inataka imsajili Okwi inatakiwa kutumia zaidi ya bilioni 2 ili iweze kumchukua.
Alisema mchezaji huyo anatakiwa katika barani Ulaya na iwapo kuna timu Tanzania inauwezo wa kutoa fedha hiyo, klabu ya Simba ipo tayari kumuuza kwa pesa hiyo.
kutangaza kuwa wanamchukua mchezaji Emmanuel Okwi wakati wakijua ni mchezaji halali wa klabu hiyo.
Ofisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga, alisema kuwa kuna baadhi ya watu wameanza kutumia jina la Okwi kama njia ya kupata uongozi au kuonekana bora katika klabu zao huku zikiwa hazijawahi hata siku moja kufanya maongezi na klabu ya Simba.
Alisema kama kuna klabu inataka kumsajili mchezaji huyo ifuate utaratibu wa kuongea na viongozi wake kwa kuwa mchezaji huyo bado ni mali ya Simba.
Aliongeza kuwa kama kuna klabu inataka imsajili Okwi inatakiwa kutumia zaidi ya bilioni 2 ili iweze kumchukua.
Alisema mchezaji huyo anatakiwa katika barani Ulaya na iwapo kuna timu Tanzania inauwezo wa kutoa fedha hiyo, klabu ya Simba ipo tayari kumuuza kwa pesa hiyo.
"Tupo tayari kumuuza.Na kama kuna klabu hapa nchini ina bilioni 2, sisi tunamuachia, kwa kuwa bado mchezaji wetu na anaendelea kuitumikia klabu yetu ya Simba kwa zaidi ya miaka miwili"alisema Kamwaga.Klabu ya Yanga kupitia wadau wake ilitangaza nia yake ya kumchukua mchezaji huyo raia wa Uganda kwa ajili ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao.
Friday, May 25, 2012
SIR ALEX FERGUSON KUSTAAFU MWISHONI MWA MSIMU UJAO
Kocha wa timu ya soka ya Manchester United, Sir Alex Ferguson huenda akaachana na kazi yake ya ukocha mara tu baada ya kuisha kwa msimu wa 2012/2013,kutokana na kuanza kusumbuliwa na matatizo ya kiafya.
Kwa mujibu wa rafiki yake wa karibu ambae pia ni mmiliki wa timu ya Wigan Athletic,Dave Whelan,Ferguson anafikria kuachana na ukocha baada ya kupata matatizo ya kiafya Ijumaa iliyopita,amabapo alipatwa ghafla na ugonjwa wa kutoka damu puani mfululizo bila kuacha na kusababisha akimbizwe Hospitali ya Glasgow
Whelan alikuwa alikiambia kituo cha televisheni cha ESPN:
Kwa mujibu wa rafiki yake wa karibu ambae pia ni mmiliki wa timu ya Wigan Athletic,Dave Whelan,Ferguson anafikria kuachana na ukocha baada ya kupata matatizo ya kiafya Ijumaa iliyopita,amabapo alipatwa ghafla na ugonjwa wa kutoka damu puani mfululizo bila kuacha na kusababisha akimbizwe Hospitali ya Glasgow
Whelan alikuwa alikiambia kituo cha televisheni cha ESPN:
"Baada ya msimu ujao,Sir Alex atabwaga manyanga.Msukumo wa mambo unataka iwe hivyo,hasa unapokuwa uko juu kwa muda mrefu.Umri unapokuwa umeshakwenda inakuwa ngumu kupambana namsukumo wa majukumu,na ipo siku lazima itakuathiri.Sir Alex ni mgumu kukubali kushindwa na najua atataka aendelee na hadi siku atakayodondoka na pia naheshimu mafanikio aliyofikia kama wengine wanavyoheshimu.Najua lengo lake lilikuwa kuendelea kwa miaka miwili au mitatu zaidi,pengine zaidi ya hapo,lakini alipata matatizo kidogo ya kiafya wiki iliyopita,hiyo inaniambia kuwa lazima afikirie kwa kina maamuzi yake na atagundua kuwa hakuna ulazima wa kuendelea kwa miaka mingine mitano na kujiweka katika hatari.Ningependa niseme yeye ni kocha bora kabisa kupata kutokea.Kama ataamua kweli kufunga virago, basi litakuwa ni pigo kubwa katika mchezo wa soka.Nina hakika.Jinsi mafanikio yake yasivyo lingana na ya mtu (kocha) yeyote,jinsi anavyochagua wachezaji kwa usahihi na kupata mavuno zaidi kutoka kwao,inamfanya awe kocha bora kabisa,bora zaidi ya tuliowahi kuwaona"
Tuesday, May 22, 2012
SIRI YA AJALI YA MAFISANGO HII HAPA
Olly Elenga, ni mtoto wa dada yake
Mafisango. Yeye alishuhudia ajali hiyo jijini Dar es Salaam na ndie aliyeikimbiza
maiti ya mchezaji huyo Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam
Katika mazishi yake, watoto wake wote watatu walihudhuria ambao ni David, Patrina na Crespo aliyekuwa anaishi naye Dar es Salaam.
Crespo aliteka umati wa watu katika mazishi hayo kwani kila mmoja alitaka kumsogelea na kumtazama.
"Kilichotokea ni kwamba baada ya Mafisango kurudi Sudan, Jumanne, siku iliyofuata alizima simu kabisa akasema hataki kwenda popote. Akanipa dola 100 nipeleke kwa dada mmoja waliyekutana naye kwenye ndege jana yake kwa ajili ya kukodi gari ile iliyopata ajali, tukapewa na dereva anayeitwa Bozi. Mafisango hakuwahi kumiliki gari jijini Dar es Salaam. Lakini asubuhi ya Jumatano iliyopita (Mei 16) alimpigia simu nyota wa Yanga, Haruna Niyonzima `Fabregas' na kumwita kwake ili wajadili kuhusu mambo ya timu ya taifa ya Rwanda. Fabregas alikuja nyumbani kuanzia asubuhi na wakanywa pombe na baadaye wakaongezeka akina Redondo (Ramadhani Chombo.) "
"Wakakubaliana waende Kinondoni kwa Queen Suzy yaani yule dansa wa bendi ya FM Academia `Wana Ngwasuma', ambaye ana baa yake karibu na Mango Garden, basi ndio wakanywa hapo na baadaye mke wa Redondo, aliyewaandalia chakula akawaita nyumbani kwao ili wakale, walipofika kule wakanywa bia sana, hapo Mafisango alikuwa hapatikani kwenye simu kwani zilikuwa zinatumika simu za Redondo na marafiki wengine aliokuwa nao."
"Tulikaa sana kwa mke wa Redondo mpaka saa tano usiku. Mafisango alishalewa sana, alikuwa hafai akajilaza kitandani hapo kwa mke wa Redondo akawa ananiambia tuwashe gari twende Keko kulala lakini mke wa Redondo akamwambia 'shemeji nina hamu ya kwenda Ngwasuma' waliokuwa kwenye Ukumbi wa Maisha Club, akatuambia twende wote. Mafisango akakubali akamwambia ataenda kumfurahisha kwa heshima yake".
"Tumefika kule ndani tukanywa sana pombe akatuza wanamuziki, tulivyoondoka akang'ang'ania kuendesha gari badala ya yule Bozi (dereva) aliyekuwa anaendesha tangu mchana, tulikuwa watano kwenye gari pamoja na yeye, kila mara Bozi alikuwa anazozana na Mafisango kwa kuwa alikuwa anamwambia mbona Mafisango mbona haendeshi vizuri gari halafu iko kasi na anayumbisha usukani hautulii, yaani ilifika sehemu mpaka tunataka kumshusha yule Bozi, lakini akasema hashuki mpaka ahakikishe tumefika Keko na kupaki gari la bosi wake."
"Tulipofika pale Keko, taa zilituzuia tukasimama, zilipowaka za kijani tukaondoka lakini spidi Mafisango aliyotoka nayo pale ilikuwa kali ghafla tukavuka geti la kwanza la Veta tukaona guta mbele yetu, kwa vile gari ilikuwa kasi ikabidi Mafisango airudishe kulia kwa nguvu kumkwepa yule jamaa halafu baada ya kumpita akairudisha kushoto ndio hapo ikaingia kwenye mtaro ikapanda ikapinduka na nikachanganyikiwa nilipoona kichwa cha Mafisango kimenasa ndani kwenye sehemu ya gia halafu gari imekwisha na yule dada (rafiki wa mke wa Redondo) aliyekuwa amekaa naye mbele naye akawa kabanwa ikabidi nimtoe. "
"Pia nikamtoa na Mafisango akiwa anavuja damu na wakati huo alishafariki. Nikasimamisha taxi nikamkimbiza Muhimbili kufika pale wakanihakikisha kwamba amekufa sikuamini."
"Lakini Mafisango aliumia sana na kama si pombe aliyokunywa asingekufa."
Katika mazishi yake, watoto wake wote watatu walihudhuria ambao ni David, Patrina na Crespo aliyekuwa anaishi naye Dar es Salaam.
Crespo aliteka umati wa watu katika mazishi hayo kwani kila mmoja alitaka kumsogelea na kumtazama.
`BOBAN` AANGUKA NA KUPOTEZA FAHAMU `AIRPORT`
| BOBAN akilia kwa uchungu siku aliyokufa Mafisango |
Tukio hilo lilitokea jana Jumatatu wakati Boban akiwa anajiandaa kurudi Dar es Salaam baada ya kuhudhuria mazishi ya Patrick Mafisango aliyefariki Alhamisi iliyopita kwa ajali ya gari iliyotokea jijini Dar es Salaam.
Hali ya Boban ilibadilika ghafla akiwa uwanjani hapo na akashindwa kuona mbele kabla ya kulegea na kuanguka.
Madaktari wa uwanja huo walitumia zaidi ya saa 1:30 kumtibu Boban kabla hajarejea katika hali ya kawaida huku bado akiwa na simanzi kubwa kutokana na kifo cha Mafisango.
Boban alimwambia Mwandishi wa michezo wa gazeti la Mwanaspoti katika uwanja huo wa ndege wa Kinshasa,
"Nilimkumbuka sana Mafisango, wakati nikitafakari, nikaona ninalegea, nikashindwa kuona kitu chochote mbele na nikaanguka,"a
Daktari aliyemuhudumia Boban alisema
"Alikuwa na hali mbaya sana, mapigo ya moyo yalikuwa chini, yangeweza kuondoa maisha yake."
Licha ya kupata matibabu hayo, Boban pia alipewa kahawa kwa lengo la kuinua mapigo yake ya moyo.
Boban ambaye alikuwa rafiki mkubwa wa Mafisango ikiwa ni pamoja na kulala chumba kimoja wanapokuwa kambini Simba, aliwakilisha wachezaji wengine wa klabu hiyo katika msiba huo mjini Kinshasa.
Mwili wa Mafisango aliyekuwa akicheza nafasi ya kiungo enzi za uhai wake, ulizikwa katika makaburi ya Kinkole nje kidogo ya Kinshasa juzi Jumapili kuhitimisha safari yake ya miaka 32 ya uhai wake duniani.
Msimu huu akiwa na Simba alifunga mabao 12 akiwa ndiye kiungo pekee aliyefunga mabao mengi katika Ligi Kuu Bara alikofunga mabao 11. Jingine alifunga katika Kombe la Shirikisho.
Katika ajali yake iliyotokea eneo la Veta, Chang'ombe wakati akirejea kutoka klabu ya Maisha, alikuwa na rafiki zake ambao walipata majeraha madogo
Thursday, May 17, 2012
MAFISANGO KUAGWA LEO,RAGE AELEZA KILICHOTOKEA
![]() |
| Hili ndio gari alilopata nalo ajali marehemu Mafisango |
Leo Ijumaa watu watapata fursa ya kuuaga mwili wa marehemu Patrick Mafisango kwenye viwanja vya TCC Club Chang'ombe jijini Dar es Salaam. kuanzia saa nne asubuhi (awali ilikuwa imepangwa mwili uagwe katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni) . Taarifa zilizotolewa baadaye na msemaji wa familia zimetaarifu kuwa mwili wa marehemu Patrick utasafirishwa na ndege ya saa kumi tayari kwa kuzikwa katika mji aliozaliwa wa Kinshasa huko nchini Congo DRC (awali taarifa zilizotolewa na meneja wa Simba Nico Nyagawa zilizema mwili wa Mafisango baada ya kuagwa utaondoka na kusafirishwa na ndege ya shirika la KQ kuelekea kwao Rwanda kwa ajili ya kuzikwa).
| Anaelia ni mmoja wamarafiki wa marehemu Mafisango ambao alikuwa nao ndani ya gari |
| Haruna Moshi `BOBAN` akilia kwa uchungu jana msibani |
| BOBAN na wenzake wakiwa msibani |
Ndani ya gari hilo inasemekana alikuwa ameambatana na mdogo wake pamoja na rafiki zake wakirejea kutoka kwenye klabu ya starehe. Patrick aliaga dunia muda mfupi baadaye alipokuwa akiwahishwa hospitalini. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam na maombolezo ya msiba yapo kwenye nyumba iliyopo maeneo ya Keko Toroli jirani na kituo cha Chang’ombe Maduka Mawili (Njia Panda ya Sigara).
Patrick alijiunga kuichezea Simba SC mwaka jana, akitokea timu ya Azam FC aliyojiunga nayo alipohamia nchini Tanzania miaka mitatu iliyopita. Awali alkuwa akiichezea APR ya Rwanda. Video za baadhi ya magoli aliyowahi kufunga zipo youtube.
| Akina mama ambao ni washabiki wa marehemu Mafisango wakilia kwa huzuni msibani jana |
Amefariki siku chache tu baada ya kocha wa timu ta taifa ya Rwanda, Milutin Sredojovik (Micho) kumuita kujumuika katika timu ya Taifa ya nchi hiyo kwa ajili ya maandalizi ya mechi za kuwania kufuzu kucheza kombe la dunia 2014.
Source: http://www.wavuti.com
Subscribe to:
Posts (Atom)
























