Pages

 

Thursday, May 31, 2012

OKWI ANA THAMANI YA SHILINGI BILIONI 2-SIMBA

0 comments
 Klabu ya Simba imewataka baadhi ya timu kuacha tabia ya kutaka
kutangaza kuwa wanamchukua mchezaji Emmanuel Okwi wakati wakijua ni mchezaji halali wa klabu hiyo.
 
Ofisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga, alisema kuwa kuna baadhi ya watu wameanza kutumia jina la Okwi kama njia ya kupata uongozi au kuonekana bora katika klabu zao huku zikiwa hazijawahi hata siku moja kufanya maongezi na klabu ya Simba.
 
Alisema kama kuna klabu inataka kumsajili mchezaji huyo ifuate utaratibu wa kuongea na viongozi wake kwa kuwa mchezaji huyo bado ni mali ya Simba.

Aliongeza kuwa kama kuna  klabu inataka imsajili Okwi inatakiwa kutumia zaidi ya bilioni 2 ili iweze kumchukua.
 

Alisema mchezaji huyo anatakiwa katika barani  Ulaya na iwapo kuna timu Tanzania inauwezo wa kutoa fedha hiyo, klabu ya Simba ipo tayari kumuuza kwa pesa hiyo.
"Tupo tayari kumuuza.Na kama kuna klabu hapa nchini ina bilioni 2, sisi tunamuachia, kwa kuwa bado mchezaji wetu na anaendelea kuitumikia klabu yetu ya Simba kwa zaidi ya miaka miwili"alisema Kamwaga.
Klabu ya Yanga kupitia wadau wake ilitangaza nia yake ya kumchukua mchezaji huyo raia wa Uganda kwa ajili ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao.

0 comments:

Post a Comment

 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797