Pages

 

Saturday, May 5, 2012

MWANASOKA RASHID YEKINI AFARIKI DUNIA

0 comments
Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria Rashid Yekini amefariki dunia jana jioni kwa ugonjwa ambao taarifa zinasema ni wa ajabu, mjini Iraa, jimbo la Kwara,Nigeria.

Yekini alirejea kutoka nje ya nchi katikati ya wiki hii alikokuwa akipata matibabu,mchezaji mwenzake wa zamani Mutiu Adepoju aliwaambia wanahabari

Ndugu wa marehemu Yekini wamesema kuwa Yekini alikuwa akisumbuliwa na maradhi ambayo hawakuyaelewa.Yekini inasemekana alikuwa akiishi maisha ya kawaida sana tangu alipostaafu kucheza soka mwaka 2005 na kurudi Nigeria akitokea kucheza soka ulaya.

Alipokuwa ulaya alichezea timu za Vitoria Setubal yaUreno,Sporting Gijon ya Hispania na Olympiakos ya Ugiriki.Aliporudi Nigeria aliendelea na soka kwa kucheza katika ligi ya nyumbani ,NPL.Aliogopa umaarufu na hakupenda kujiweka mbele ya kamera na kalamu za waandishi wa habari na mara kadhaa alikataa vyeo mbali  mbali alivyopewa katika soka la Nigeria.

Wakati wa pilika pilika za kombe la dunia 2010 alikataa alipoombwa kuwa balozi wa Nigeria katika michuano hiyo na nafasi yake alikabidhiwa golikipa wa zamani wa Nigeria Ike Shorunmu

Mwezi uliopitan mchezaji mwenzake ambae walichezea timu ya taifa pamoja,kiungo Segun Odegbemi alikanusha taarifa juu ya hali mbaya ya afya mbaya Yekini.Na katika makala yake kwenye gazeti moja la nchi hiyo,Odegbemi aliwahakikishi wasomaji wake kuwa amefanya mazungumzo na Yekini na yuko mbioni kurudi katika ulimwerngu wa soka na mradi wa kuendeleza vipaji vya vijana katika soka

Mwandishi wa habari ambaye alifika ilipo nyumba ya Yekini mjini Ibadan, alielezwa kuwa mama wa Yekini ambae ni mtu mzima sana na mke wa pili wa Yekini walifika Ibadan kumchukua wiki mbili zilizopita, baada ya kupata taarifa kutoka kwa majirani kuwa Yekini alikuwa akifanya mambo ya ajabu

Nyumbani kwake kulikuwa kimya wakati huo na hakukuwa na dalili ya kuishi mtu kwani geti lilikuwa limefungwa na uwanjani zilipo nyumba zake nne kila kitu kilionekana ovyo na majani marefu yameota.Magari yake yalikuwa yameondolewa, na wapangaji wa Yekini waliokuwa wakiishi katika nyumba tatu walishahama kwa kile kilichoelezwa kuwa waliondolewa na Yekini mwenyewe.Watu wa kanisa lililopakana na nyumba ya Yekini walisema kuwa hawajamuona Yekini kwa mwezi mzima.

Yekini ambaye mwezi Oktoba angetimiza miaka 49 ya kuzaliwa  aliisaidia Nigeria katika michuano ya kombe la dunia 1994 Marekani.Goli lake ndio lilipeleka Nigeria kwenye hatua ya robo fainali,ikiwa ni mara ya kwanza kwa nchi hiyo kufikia mafanikio hayo.Na alitunukiwa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Afrika
Yekini anazikwa  kijijini kwao Offa leo Jumamosi kwa taratibu zote za kiislam

0 comments:

Post a Comment

 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797