Msanii wa kike wa filamu nchini
Elizabeth Michael leo alifikishwa tena katika mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu,Dar Es Salaam kwa ajili ya kusomewa kesi mauaji
inayomkabili.Elizabeth anahusishwa na kifo cha msanii mwenzake Steven
Kanumba,baada ya msanii huyo kafariki ghafla wakiwa pamoja usiku wa
Aprili 7 mwaka huu
Mbele ya hakimu wa mahakama hiyo
Bi.Augustina Mmbado,Elizabeth alisomewa tena mashtaka na hakutakiwa
kujibu chochote kuhusiana na kesi hiyo.Hata hivyo mawakili wanne wanao
mtetea Elizabeth waliomba udhuru ambapo wakili Keneth Fungamtama kwa
niaba ya wenzake,aliiomba mahakama itoe udhuru kwa mshtakiwa kesi
ikasikilizwe kwenye mahakama ya watoto,kwani mshtakiwa bado ana umri
mdogo ambao hauruhusu kushtakiwa kwenye mahakama za kawaida, huku
akikabidhi cheti cha kuzaliwa cha mshitakiwa kikionesha kuwa ana umri wa
miaka 17, na pia kesi yake isikilizwe INCAMERA,(faragha)ombi ambalo
mahakama ililikataa kwa kutumia kifungu namba 198 cha sheria,kwa kuwa
mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.Pia mahakama
ilikataa kutambua cheti cha kuzaliwa cha mshitakiwa kwa madai kuwa cheti
kiliandikwa jina la Diana, jina ambalo mshitakiwa hakuwahi
kulitumia.Elizabeth anatetewa na mawakili Keneth Fungamtama,Fulgence
Massawe,Peter Kibatara na Jackline De Melo.
Kesi imehairishwa tena hadi Mei 21 itakapotajwa tena na Elizabeth amerudisha rumande
0 comments:
Post a Comment