Pages

 

Tuesday, May 22, 2012

UJAUZITO WA LULU `WACHOROPOKA`

0 comments

 
Ujauzito wa mwigizaji nyota wa sinema Bongo ambaye yuko  Gereza la Segerea, Dar es Salaam kwa tuhuma ya kuhusika na kifo cha Steven Kanumba, Elizabeth Michael 'Lulu' umedaiwa kutoka.

Kwa mujibu wa taarifa za wachunguzi kupitia chanzo cha habari hizi sababu kubwa ya mimba hiyo kutoka ni kutunga nje ya mfuko wa uzazi hali ambayo ingemletea matatizo Lulu.
Chanzo kilisema bila kuainisha tukio hilo lilitokea lini:
“Nikwambie kitu, unajua wengi wanaamini Lulu ana mimba na hivi karibuini iliandikwa imefikisha miezi mitatu, ilikuwa sahihi, lakini ukweli ni kwamba kwa sasa imetoka.Sababu kubwa ni kwamba afya yake ilidorora, ukiachia ule ugonjwa wa U.T.I alioripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba anao, lakini kingine ni kuwa iligundulika ujazuito wake ulitunga nje ya mfuko wa uzazi ikawa haina jinsi, ikabidi kutolewa na kusafishwa.” 

Kikiendelea kuzungumza kwa umakini mkubwa, chanzo hicho kilidai kuwa  ujauzito huo ni wa tatu kuchoropoka kwa msanii huyo.
“Unajua huu unakuwa ujauzito wa tatu kwa Lulu kutoka. Kwa kweli kama si hivyo angekuwa na mtoto,” kilisema chanzo bila kuweka wazi nyingine mbili zilitoka kwa matatizo gani.
Chanzo hicho kilidai:
 “Kuna wakati Lulu alikwenda China, aliporudi alikuwa na ujauzito, lakini nao ulitoka, inaonekana ana matatizo kidogo kwenye upande wa kizazi,”  .
Kikaendelea:
 “Baada ya hapo, haukupita muda mrefu, akanasa nyingine ya mwanamuziki mmoja wa Bongo Fleva, pia hiyo nayo ikaja kutoka ya tatu ni hii ya Kanumba.”


Mchunguzi ambae alitumwa na chombo kimoja cha habari kwenda Gereza la Segerea ili kukutana na Lulu na kuzungumza naye ameelezea ugumu wa kumpata ‘laivu’ nyota huyo kutokana na ukweli kwamba kuna watu maalum watatu ambao ndio wenye ruhusa ya kumwona mtuhumiwa huyo,na si zaidi ya hao.
Hata hivyo, ‘shushushu’ huyo alifanikiwa kupata fursa ya kumjulia hali mahabusu mwingine aliyepo kwenye gereza hilo na ndipo akapata bahati ya kuonana na Lulu ambaye alionekana kuwa mnyonge.
Baada ya salamu, mchunguzi huyo alimtupia swali Lulu kuhusu afya yake na ya ujauzito alionao ambapo alijibu kwa mkato.
“Nani amekwambia mimi nina mimba?”


Baadhi ya mastaa wa sinema Bongo ambao hawakuwa tayari majina yao kutajwa, walipishana ‘kiswahili’ kuhusu kuwepo au kutokuwepo kwa ujauzito wa Lulu .
Wapo waliodai ujauzito huo ulitoka akiwa gerezani, wengine walidai ulitoka wiki moja kabla ya kifo cha Kanumba lakini wapo waliodai bado anao.
Staa wa kiume: 

“Lulu hana ujauzito, ulitoka. Ninavyojua mimi, wiki moja kabla ya kifo cha marehemu (Kanumba) ndiyo ulitoka, kwa hiyo hana.”
Staa wa kike:
 “Lulu bado ana mimba ila ni siri sana. Lakini hata nyie wenyewe si mmeona tumbo lile? anao!”
Staa wa kike: 

"Lulu mpaka anaingia kwenye matatizo kwa kifo cha Kanumba alikuwa na kibendi, hawezi kukitoa kwa sasa, maana yuko gerezani.”

Lulu anatarajiwa kufikishwa Mahakama Kuu ya Tanzania Mei 28, mwaka huu ili kujibu tuhuma zinazomkabili juu ya kifo cha Kanumba.

0 comments:

Post a Comment

 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797