Bingwa wa dunia wa mchezo wa kuogelea Mnorway Alexander Dale Oen amefariki dunia akiwa katika kambi ya mazoezi mjini Flagstaff,Arizona nchini Marekani
Rais wa Shirikisho la Michezo ya Kuogelea la Norway Per Rune Eknes ametangaza kuwa bingwa wa dunia wa michezo hiyo kwa umbali wa mita 100,Mnorway Alexander Dale Oen amefariki dunia jana kwa ugonjwa wa moyo akiwa na umri wa miaka 26.
Muogeleaji huyo alikutwa ameanguka bafuni jana na alikimbzwa katika Hospitali ya Flagstaff ambako ilithibitishwa kuwa tayari alikuwa ameshakufa .Starla Collins msemaji wa hospitali hiyo alitangaza rasmi kifo cha muogeleaji huyo,lakini hakutoa maelezo zaidi
Oen alishinda katika mashindano ya mjini Shanghai mwaka jana,siku tatu tu baada ya Andres Breivik kufanya mauaji ya kinyama ya watu 77 nchini Norway na aliutunukia ushndi huo kwa wahanga wa mauaji hayo huku akiinyooshea kidole bendera ya Norway iliyobandikwa kwenye kofia aliyovaa.
Timu ya Norway itakayoshiriki michezo ya olimpiki imeweka kambi mjini Flagstaff.Wachezaji wengine walisema kuwa kabla ya tukio Dale Oen alifanya mazoezi mepesi tu na kucheza gofu,lakini baadae walipata wasiwasi walipogundua kuwa mwenzao ameshatumia muda mrefu bafuni na walipokwenda kugonga alikuwa hajibu.Walipoingia walimkuta amelala mwili nusu ya mwili ukiwa sakafuni na nusu nyingine kwenye jakuzi.Daktari wa timu alianzakumpatia huduma ya kwanza mara moja kabla gari la wagonjwa halijafika.Oen alikuwa ni moja ya tegemeo la Norway katika michezo ijayo ya olimpiki

0 comments:
Post a Comment