Kikundi cha watu wenye silaha wamemteka,kumuua binti wa albino mwenye umri wa miaka 15 na kisha kuukata kata mwili wake nchini Burundi ikiwa ni tukio la 18 ndani ya miaka minne kutokea nchini humo
Watu wenye ualbino,hali ya kibaiolojia ambayo huzuia kabisa utengenezwaji wa rangi ya ngozi,wamekuwa wakibaguliwa na baadhi ya jamii katika nchi kadhaa za kiafrika
Kutokana na imani za kishirikina zilizotawala katika jamii hizo kwamba albino wana uwezo wa ziada,hupelekea watu hao kuuawa na kisha viungo vyao kuuzwa kwa waganga wa kienyeji
Katika tukio la majuzi kundi la watu waliobeba mikuki,magobole na mapanga walivamia nyumba moja katika eneo lililo karibu na mji mkuu Bujumbura na kumteka msichana mwenye umri wa miaka 15
Kwa mujibu wa maafisa wa serikali,watu hao walimuua binti huyo na kisha kukata mikono na miguu na kutokomea navyo.
Idadi ya maalbino waliouawa kwa staili hiyo imefikia 18 tangu mwaka 2008 na kasi ya mauaji hayo ilpungua baada ya mwezi Agosti 2009 ambapo watu wanane walikamatwa na kufunguliwa mashtaka ya mauaji ya albino
Lakini Kassim Kazungu ambae ni Rais wa kikundi kinachotetea maalbino cha Albinos Sans Frontieres anasema kuwa serikali ya nchi hiyo imeshindwa kulinda maisha ya maalbino nchini humo kwani kila mtu aliehukumiwa kifungo kwa mauaji ya albino ametoroka gerezani.
0 comments:
Post a Comment