Pages

 

Tuesday, May 22, 2012

PICHA YA JACOB ZUMA AKIWA UCHI YACHORWA NA KUWEKWA KWENYE MAENESHO,YAZUA UTATA MKUBWA

0 comments
Picha hii inaonesha sehemu ya juu ya mchoro uliopewa jina la `The Spear `ukifananisha taswira ya rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma


Mchoro wa picha inayomkejeli rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ukionesha mfano wa sehemu za siri za rais huyo wa taifa lenye nguvu barani Afrika, umewekwa hadharani kwenye jumba la maonesho ya picha la Goodman huko Johannesburg,Afrika Kusini na kuanzisha mjadala mkali.
Mchoro huo uliopewa jina la `The Spear`ulichorwa na kuwekwa hadharani na msanii wa michoro wa Cape Town, Brett Murray ambae amejitetea kuwa hakuwa na lengo la kumuudhi mtu yeyote ila ni njia yake ya kujieleza kisiasa kwa staili ya ucheshi,kama msanii
Mchoro huo ni sehemu ya michoro iliyo kwenye maonesho ya Murray anayoyaita `Hail to the Thief II`


Katika kuonesha kukerwa na mchoro huo,watu wawili waliingia kwenye jumba hilo na kuuharibu kwa rangi.Mtu mmoja aliweka alama ya X kwa kutumia rangi nyekundu kwenye eneo la kichwa  na sehemu za siri za mchoro huo na mwengine ambae ni kijana mdogo alivurga mchoro kwa kupulizia rangi nyeusi.
Mwandishi wa BBC ambae alikuwa eneo hilo leo asubuhi aliandika kwenye Twitter:


"Mchoro wa Zuma umevurugwa kwa rangi nyeusi.Muhusika kaniambia kuwa mchoro huo ni wa kichokozi.Walinzi wamemvamia na kumkamata...mtu wa pili nae mbaroni"


Mchoro huo ulikuwa unalindwa na kampuni binafsi ya ulinzi wakati wa tukio


Baada ya kutiwa mbaroni watuhumiwa walifikishwa kwenye kituo cha polisi cha Rosebank


Mapema leo wawakilishi wa chama cha ANC walikimbilia mahakama kuu ya Gauteng mjini Johannesburg kufungua pingamizi la kuzuia jumba la Goodman lisitumie mchoro huo wenye urefu wa mita 1.85 kwenye maonesho.Na pia walikwenda kwenye ofisi za City Press kutaka picha za mchoro huo zisiwekwe mtandaoni


Polisi awali walitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuwa  mitaa kadhaa kuzunguka eneo la mahakama kuu itabidi ifungwe  kuruhusu wafuasi wa ANC ambao wangefika hapo kwa maandamano.Walisema mitaa hiyo itakuwa wazi ifikapo saa 9 alasiri ambapo mahakama itakuwa inafunga shughuli zake


Jumuia ya wanawake wa ANC walihimiza wanawake wenzao kuunga mkono uamuzi wa ANC kuandamana hadi mahakamani.Katika taarifa yao walisema:

"Hakuna Mwafrika Kusini yeyote,katika ofisi yoyote anaestaihili kuvunjiwa heshima namna hii na ni mtu aliekosa hekima kichwani mwake tu ndie anaeweza kudiriki kuchora mchoro kama huu.Tunatoa shutuma kali kwa kazi hii (ya Murray) na tutaendelea kuidharau kadri inavyostahili,tukitegemea Brett Murray atachukua fursa hii kujiangalia,heshima na tabia yake kama binadamu"


Chama cha ANC kiliwataka wanachama wake kukusanyika kwa wingi nje ya mahakama kuu leo kutetea utu, heshima na hadhi ya Zuma, rais wa ANC
Gazeti la Times nalo liliripoti leo asubuhim kuwa msemaji wa kanisa la Nazareth Baptist Church,Enoch Mthembu amependekeza Bret Murray apigwe mawe hadi kufa


"Huyu mtu amelitukana taifa zima na anstahili kupigwa mawe hadi afe.Alixchofanya kinaonesha ni jinsi gani alivyolelewa kibaguzi.Sanaa haiungi mkono kuwavunjia heshima binadamu wenzako"


Chama cha ANC kiliwasilisha karatasi za kimahakama kwenye jumba la maonesho na City Press ambazo zilizotolewa na mahakama siku ya Ijumaa
Karatasi hizi zinazuia pande zote mbili kuweka hadharani mchoro na picha za mchoro huo kwenye mitandao yao au mahali pengine popote


Habari kutoka kwenye jumba la maonesho la Goodman zinasema kuwa wamekataa kutii amri ya mahakama ya kuondoa mchoro huo na kusema kuwa mchoro huo watautumia hadi hapo maonesho yatakapokwisha na kuongeza kuwa kazi yao inalindwa na haki yao kikatiba ya uhuru wa kujieleza


Habari zilizopatikana mchana  zinasema kuwa  watuhumiwa waliokamatwa wakiharibu mchoro huo kwenye jumba la maonesho la Goodman asubuhi ya leo ,wametambuliwa kuwa ni profesa wa chuo kikuu na kijana mdogo mwenye umri wa miaka 15


Mwanasheria wajumba hilo Gregg Palmer amesema kuwa watu hao watafunguliwa kesi ya kuharibu mali.


Ripota wa kituo cha Tv cha eNews,Iman Rappetti,ambae alikuwepo leo asubuhi kwenye jumba hilo kuripoti juu ya mchoro huo uliopewa jina la `The Spear` (mkuki),alieleza jinsi alivyokabiliana na profesa aliekuwa akiharibu mchoro.
Amesema kuwa alikuwa karibu kabisa na mchoro huo wakati profesa huyo alipotoa kifaa cha kuhifadhia rangi na kuanza kuchora alama ya X kukatiza sehemu za siri za mchoro huo


Ameelezea jinsi alivyomvuta mkono kumzuia asiharibu mchoro huku akipiga kelele kuomba msaada kutoka kwa wafanyakazi wa jumba hilo


Rappetti alimuelezea mtu huyo kuwa alikuwa wa kawaida tu amevaa koti lililofumwa,lakini hakujua kuwa nyuma yake alisimama kijana mdogo kashika kasha lenye rangi nyeusi tayari kufuata nyayo za profesa.Alipiga kelele kumzuia kijana huyo alipoanza kupakaza rangi nyeusi juu ya mchoro huo


Wafanyakazi wa jumba waliwadhibiti profesa na kijana, kabla ya polisi kufika mara moja na kuwachukua.Wafanyakazi wa hapo walimwambia Rappetti kuwa, awali profesa alijitambulisha kuwa ni wa kabila la Afrikaans,lakini Rappetti ana wasiwasi kuhusu hilo

"Haonekani kama ni Mwaafrikaans"

Umati wa watu na waandishi wa habari walianza kujaa kuzunguka jengo ambalo tayari lilikuwa limeshafungwa.Ndani ya lango kuu la kuingilia walisimama walinzi watatu wa kampuni binafsi huku wameshika silaha za moto na wamevaa jaketi za kuzuia risasi.

0 comments:

Post a Comment

 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797