Pages

 

Friday, May 4, 2012

RIPOTI ILYOKWENDA SHULE;MADHARA YA KUTUMIA OVYO FACEBOOK HAYA HAPA:

0 comments
Watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii hawajui madhara ya matumizi holela ya mitandao hiyo au hawataki kujihadhari na hatari zinazowakabili,ripoti imetolewa jana mjini Washington katika jarida la taasisi isiyo ya kiserikali, Consumer Reports

Ripoti hiyo inasema watumiaji wapatao 13 milioni wa Marekani hawajui au hawataki kutumia nyenzo za kujiweka salama kwenye mtandao wa facebook.Uchunguzi unaonesha kuwa wamarekani wapatao 4.5 milioni huwa wanaandika kwenye facebook wapi watakwenda na muda gani katika siku fulani na hii ni njia mojawapo ya kuwataarifu watu wabaya wanaoweza kudhuru,na pia kuna idadi nyingine ya wamarekani 4.7 milioni ambao wame `like` page zinazohusu mambo ya afya na tiba na kutoa taarifa za afya zao,bila ya kutambua kuwa kufanya hivyo ni kuyanufaisha makampuni ya bima.

Ripoti inaendelea kudokeza kuwa ni asilimia 37 tu ya watumiaji wa facebook ndio waotumia nyenzo za usalama wa taarifa zao kwenye facebook
"Facebook kwa kweli ni mtandao ambao kwa kiasi kikubwa umebadilisha namna watu wanavyoweza kuwasiliana duniani, na imekuwa huduma ambayo inafanikisha kwa kiwamgo kikubwa usambaaji wa taarifa binafsi za mtumiaji kwa umbali ambao hata mtumiaji mwenyewe hawezi kuamini"
Ripoti hiyo inaendelea kusema kuwa mwaka jana familia zipatazo 7 milioni zinazotumia mtandao wa facebook zimeripotiwa kuingia kwenye matatizo kutokana na facebook,matatizo kama vile watu wengine kuingia kwenye akaunti zao bila wao kujua,kusumbuliwa na kutishwa

"Uchunguzi wetu umegundua mambo ya kustaajabisha ambayo si ya kuyakalia kimya-lakini ni vyema wale wanaotaka kuziweka taarifa zao salama zaidi wajue"
Uchunguzi unaonesha kuwa facebook inakusanya taarifa nyingi za watumiaji pengine bila watuimiaji wenyewe kujua

Mtumiaji atashangaa kufahamishwa kuwa facebook wanakusanya taarifa kila anapoingia kwenye website yenye alama ya `like` bila kujali iwapo amebonyeza  alama au la...au ana akaunti ya facebook, au hata kama haja log in

Wachunguzi hao wamewashauri wamiliki wa facebook kulichukulia suala la usalama wa taarifa za watumiaji kwa umakini kwa kuweka nyenzo zitakazo dhibiti watumiaji wajanja.Pia wametahadharisha kuwa taarifa za watumiaji zinapochukuliwa ni jambo la hatari

Watumiaji walioulizwa mikakati yao katika kuweka salama taarifa zao kwenye facebook walitoa majibu ya kustaajabisha,robo yao huwa wanaweka taarifa  za uongo kwenye akaunti zao za facebook,ikiwa ni pamoja na  majina na tarehe za kuzaliwa

Idadi ya watu waliokiri kutumia taarifa za uongo imeongezeka maradufu ukilinganishwa na miaka miwili ilyopita swali hilo hilo lilipoulizwa,ingawa kisheria kitendo hicho ni kinyume na mkataba wa matumizi ya facebook

Mtandao wa facebook unasubriwa kwa hamu kubwa utakapoingia kwenye soko la hisa kwa mara ya kwanza wiki chache zijazo na kutarajiwa kuuza hisa zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 10,ikiwa ni kiasi kikubwa zaidi kuwahi kuuzwa na kampuni za internet katika soko la hisa la Wall Street

Idadi ya watumiaji wa facebook duniani imeongezeka na kufikia milioni 901 hadi ilipofika robo ya mwaka kwa mujibu wa nyaraka za kampuni hiyo.
Kwa taarifa zaidi tembelea link hii  http://www.consumerreports.org/cro/magazine/2012/06/facebook-your-privacy/index.htm

0 comments:

Post a Comment

 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797