Pages

 

Thursday, May 17, 2012

LULU ANAUMWA

0 comments
Elizabeth ` LULU` Michael

Habari  zinaeleza kuwa staa wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amekwaa gonjwa baya akiwa mahabusu katika Gereza la Segerea jijini Dar es Salaam.

Akizungumza  baada ya kuonekana kwenye duka moja  linalouza madawa ya binadamu,  Kinondoni, hivi karibuni, rafiki wa karibu wa Lulu alisema kuwa alikuja kununua dawa za kumpelekea Lulu gerezani kwa kuwa amepatwa na ugonjwa unaomshambulia sehemu nyeti wa Urinary Tract Infections (U.T.I).

“Namchukulia Lizzy (Lulu) dawa, amepata U.T.I, si unajua mazingira ya usafi kwenye vyoo vya gerezani? Ni rahisi sana mtu kupata au kuambukizwa U.T.I kwa sababu ni vyoo vya public (vinavyotumiwa na watu wengi),” alisema rafiki huyo ambaye huwa  gerezani hapo mara kwa mara.

  Lulu  anaendelea vizuri huku hofu kubwa ikiwa kwenye ujauzito wake kuhofiwa usije   kutoka.

Lulu yupo ndani ya mahabusu ya Segerea kwa tuhuma za kuhusika na kifo cha msanii mwenzake Steven Kanumba na atafikishwa tena mahakamani  Jumatatu hii.



0 comments:

Post a Comment

 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797