Pages

 

Monday, May 21, 2012

IKWIRIRI YAGEUKA UWANJA WA VITA,MMOJA AFARIKI DUNIA

0 comments
  HALI  siyo shwari Ikwiriri wilayani Rufiji, baada ya watu wasiojulikana kuvamia nyumba ya Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD), kuivunja na kuharibu mali huku wengine wakichoma moto magari na nyumba za wananchi

Taarifa zinasema kuwa, vurugu hizo ziliibuka usiku wa kuamkia juzi kutokana na mapigano kati ya wakulima na wafugaji eneo hilo.

.
Vurugu hizo zilizosababisha kuigeuza Ikwiriri uwanja mdogo wa vita zimetokana na wananchi wenye hasira kali ambao walikuwa wanapinga mauaji ya mkulima Shamte Tawangala (60) mkazi wa Ikwiriri aliyeuawa kwa kupigwa na fimbo na vijana jamii ya wafugaji waliokuwa wakichunga ng'ombe katika shamba lake.
Kamanda Mangu alisema kuwa chanzo cha mauaji hao kinaelezwa kuwa ni wachungaji hao kutaka kulishia mifugo yao kwenye shamba la mahindi la Tawangala, na alipojaribu kuwakataza walianza kumshambulia kwa fimbo maeneo mbalimbali ya mwili wake hadi kufariki dunia.

 Habari zinadai kuwa, mapambano kati ya polisi na wananchi  yalizuka baada ya watu kuamua kuingia barabarani kupinga kukamatwa kwa wenzao zaidi ya 20, na pia kukaidi kutimizwa kwa ombi lao la kutaka waachiwe huru.


Akizungumzia kukamatwa kwa wananchi hao, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ernest Mangu alisema watuhumiwa hao walitiwa mbaroni juzi wakati wa vurugu kati ya wakulima na wafugaji ambazo zilidumu kwa zaidi ya saa sita kupinga mauaji ya mkulima yaliyofanywa na wafugaji ambao walikimbia baada ya tukio hilo.
Kamanda Mangu alisema kuwa kabla ya watuhumiwa hao kufikishwa mahakamani juzi asubuhi, zilizuka vurugu nyingine zilizofanywa na wananchi ambao walikuwa wakishinikiza kuachiwa wenzao waliokuwa wamekamatwa.
“Ni kweli leo (juzi) asubuhi muda wa saa tatu wananchi walianza tena vurugu kushinikiza wenzao waliokamatwa na polisi waachiwe, walianza kwa kuchoma matairi, lakini vurugu hizo hazikuchukua muda mrefu kwa kuwa askari wa kutuliza ghasia tunao, na waliweza kuzima vurugu hizo na zoezi la wenzao kufikishwa mahakamani likafanyika kama lilivyopangwa,”alisema Mangu.
Aidha, alisema kuwa katika vurugu hizo wapo ambao wamekamatwa, lakini idadi yao haijajulikana kwa kuwa wako kwenye mahojiano na polisi na watakapobainika watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.


Mangu alisema  walikuwa wanashikilia watu 50 kwa tuhuma za kufanya vurugu, ikiwamo kufunga barabara na kuharibu mali kadhaa.
Alisema wanaoshikiliwa siyo wafugaji wala wakulima, hivyo kama kuna taarifa za kuwapo ulipizaji kisasi siyo sahihi kwani kati ya makundi hayo hakuna kundi lililochukuliwa zaidi ya vijana wa mjini waliokuwa wakifanya vurugu.

“Sisi hatujawakamata wafugaji au wakulima, katika operesheni ilikuwa ya kukamata watu waliokuwa wakifanya vurugu ndiyo tunaowashikilia, sasa ukisema kuna madai ya wafugaji kutaka kulipiza kisasi hapo nashangaa kwa maana mbili, kwanza siku ya fujo hakuna hata mfugaji mmoja aliyelipiza kisasi kwa mkulima,”alisema Mangu na kuongeza:

 “Kweli wafugaji walionyesha kutii walau sheria kwa sababu, licha ya baadhi ya watu kudai wakulima wanawashambulia, wao walikuwa hawajajibu mashambulizi ndiyo maana vurugu hizi tumeweza kufanikiwa kuzizima mapema, lakini kama wafugaji nao wangeenda kuwapiga wakulima hapo sasa kazi ingekuwa ngumu.”   
 MILIO ya mabomu ya machozi na vita ya mawe baina ya askari wa Jeshi la Polisi na wananchi, viliendelea kwa siku mbili, ambapo watu 50 wamekamatwa na kufikishwa mahakamani.
Chanzo cha habari hii kilishuhudia mapambano baina ya polisi waliokuwa wakiwatupia mabomu ya machozi wananchi walioonekana mbele yao, ambao nao katika kujibu mapigo waliwashambulia askari hao kwa mawe.
Polisi hao walilazimika kutumia mabomu hayo, na kufanikiwa kuwakamata watu wengi ambao walikuwa wakikimbia bila mpangilio baada ya kuzidiwa na moshi wa mabomu hayo, katika kutuliza ghasia na mapigano yaliyozuka baina ya wakulima na wafugaji yaliyozuka juzi baada ya kuuawa kwa mkulima mmoja na vijana wawili jamii ya wafugaji.


Mmoja wa wakazi wa eneo hilo alisema kuwa, shughuli zote tangu mtaa wa Kaunda hadi eneo la Mwembemhuro kuelekea bonde la Mto Rufiji, zilifungwa na magari yote yalizuiwa kuingia katikati ya mji wa Ikwiriri.

Taarifa kutoka Jeshi la Polisi zimeeleza kuwa, zaidi ya nyumba saba, duka moja na magari kadhaa yaliharibiwa katika tukio hilo.
Mangu alisema kuwa hadi sasa maofsa wa polisi Mkoa wa Pwani wakiwa na helkopta, wameweka kambi katika eneo hilo ili

.

Wakati hayo yakiendelea, watu 49 kutoka jamii ya wafugaji wamehamia na kuishi na familia zao Kituo cha Polisi Ikwiriri, kuepuka vurugu zinazoendelea mitaani ambazo juzi ziliripotiwa kupoteza maisha ya mkulima mmoja.
Ingawa polisi wanasema hali ni shwari, taarifa zilizothibitishwa na watendaji wa chini zinaeleza siyo shwari na wakati wowote vurugu zinaweza kurudi tena.

Katika eneo la Ikwiriri inakopita barabara kuu ya Dar es Salaam- Mtwara,  tangu juzi  biashara ya maziwa iliyokuwa ikifanywa na wake wa wafugaji haikuwapo, inadaiwa wamehofia usalama wao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ernest Mangu,  alisema wanaendelea kufanya doria  ili kujiridhisha.
Pia, Mangu alisema lengo la doria hizo pia ni kuhakikisha kinachosemwa na baadhi ya watu kuwa, kuna dalili za kurejea vurugu iwapo ni kweli au la.

Kuhusu madai ya ofisa mmoja wa jeshi hilo kuhamishwa kituo cha kazi siku hiyo ya tukio, Mangu alisema hana taarifa hizo.

*PICHA YA SATELLITE KWA MSAADA WA GOOGLE GEOEYE

0 comments:

Post a Comment

 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797