Taswira kubwa kabisa ya uso wa mwezi kwa 2012 itaonekana Jumamosi hii.Kwa mujibu wa wataalam wa mambo ya anga za mbali mwezi utaonekana kuwa karibu zaidi usiku wa tarehe 5 mwezi huu na kwa sababu
tukio linatokea wakati mwezi umekomaa (fullmoon) unategemewa kuonekana kwa ukubwa zaidi kuliko wakati wowote mwaka huu
Inasemekana mwezi utasogea umbali wa maili 221 802(km.356 955)kutoka kwenye sayari yetu na kuwafanya watazamaji wauone ukiwa kwenye umbo kubwa na wa kung`aa sana.Mwezi huwa unasogea karibu na dunia mara kwa mara ndani ya mwaka lakini tukio la Jumamosi hii utasogea zaidi kwa asilimia 3 na hii husababishwa na njia (orbit)inayopita mwezi kutokuwa na umbo la duara kamili.Wataalam hao wanasema kuwa usiku huo mwezi utangaa mara 16 zaidi na kwamba ingawaje tukio hili lisilokuwa la kawaida litawashangaza wengi lakini hakuna haja ya kuwa na hofu,kwani mwezi kusogea kidogo hakuna madhara.Wanasema iwapo mwezi ungesogea karibu sana na dunia basi ingezua hali ya matetemeko ya ardhi na kuathiri mwenendo wa bahari
Kwa mara ya mwisho mwezi ulisogea tarehe19 machi mwaka jana.Inashauriwa kwa wale wanaotaka kuuona mwezi kwa wale wanaotaka kuuona mwezi kwa umbo kubwa zaidi wavizie wakati unachomoza au wakati unazama
0 comments:
Post a Comment