Pages

 

Tuesday, May 15, 2012

MAISHA YA LULU GEREZANI

0 comments
MAISHA ya msanii maarufu ya filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambaye yupo katika Gereza la Segerea, yamebainika
Lulu ambaye anadaiwa kuhusika na kifo cha aliyekuwa msanii maarufu wa filamu, Steven Kanumba ‘The Great’ kilichotokea Aprili 7, mwaka huu, imeelezwa kuwa maisha yake ya mahabusu yanasikitisha.
 Msanii huyo licha ya kuwa analetewa chakula kutoka nyumbani kila siku, huwa anakula baada ya kubembelezwa na baadhi ya mahabusu wenzake.
“Lulu siyo yule mnayemfahamu uraiani, humu gerezani amekuwa mtu wa kusikia kile anachoambiwa na wenzake, amekuwa msikivu sana na hupenda kulala mara kwa mara,” Mtu alie karibu na Lulu mahabusu alisema
Habari zinasema msanii huyo amekuwa akifundishwa aya kwa aya za Biblia na amekuwa mwepesi kushika baadhi ya mistari ya kwenye kitabu hicho kitakatifu kwa Wakristo.
“Bila shaka amekuwa akishika aya kwa kuwa alizoea kushika maneno yaliyokuwa yanaandikwa katika script za michezo ya filamu,” alisema askari mmoja wa magereza .
Alisema kinachosikitisha ni pale anapotembelewa na rafiki zake, kwani wakiondoka Lulu hushinda akilia mchana kutwa.
Aliongeza kuwa hali anayoishi nayo msanii huyo gerezani ni ya kutia huzuni na simanzi na haonekani kuzoea mazingira kama walivyo mahabusu wengine.
Hivi karibuni, ilielezwa kuwa Lulu amekuwa akivaa rosari na kusoma Biblia mara kwa mara kutokana na mafunzo anayopewa na baadhi ya walokole waliofungwa katika gereza hilo.

0 comments:

Post a Comment

 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797