Pages

 

Sunday, May 20, 2012

`DOGO` BOSI WA FACEBOOK,MARK ZUCKERBERG, AFUNGA NDOA KWA STAILI SIKU YA JUMAMOSI

0 comments
Mwanzilishi wa mtandao wa kijamii wa Facebook, Mark Zuckerberg, amefunga ndoa siku ya Jumamosi na rafiki yake wa kike  wa siku nyingi msichana mwenye asili ya China, Priscilla Chan.
Zuckerberg kijana bilionea mwenye umri wa miaka 28 alitangaza rasmi tukio hilo kwa washabiki wake wa Facebook kupitia Timeline yake


Wawili hao walianza mahusiano wakiwa Chuo Kikuu cha Harvard na wamekuwan imara kwa takriban miaka 9 sasa.Walilishana kiapo katika sherehe isiyokuwa kubwa upande wa nyuma wa nyumba yao huko Palo Alto,California.Kitendo hicho kilileta hali ya mshangao kwa wageni waalikwa wasiopungua 100,kwa mujibu wa  jarida la People,kwa kuwa wengi wao walidhani ni sherehe za kuhitimu kwa Priscilla,ambae tarehe 14 mwezi huu alipata shahada ya chuo kikuu ya elimu ya afya ya watoto kutoka Chuo Kikuu cha California cha San Fransisco(UCSF)

Hii ni Historia yake

Inasemekana Zuckerberg ndie aliebuni pete ya Priscilla ambayo ni ya kawaida tu iliyonakshiwa kidogo na chembe chembe za madini ya ruby,hata mavazi aliyovaa yalionekana kuwa `simple`
Add caption
Zuckerberg kijana ambaye anasifika kwa kufanya mambo yake `simple` alitoa taarifa za tukio hilo katika hali ya kawaida sana kwa kubadilisha status ya kwenye Timeline yake kutoka `in relationship` na kuwa `married`,status ambayo watu zaidi ya laki 8 wame `like` kwa masaa 24 iliyokaa mtandaoni.Muda mfupi baadae dada wa Mark aitwae Arielle aliandika katika facebook yake "Balls.Now I`m the only unmarried Zuckerberg." Na bibi harusi Priscilla nae alimuweka Arielle kama `family member` wake mpya

Kijana Mark Zuckerberg ana hisa zenye thamani isiyopungua dola za kimarekani bilioni 20.Kampuni yake ya Facebook ambayo kwa mara ya kwanza kabisa imeingia katika biashara ya hisa,imeanza  katika mnada wao wa kwanza uliofanyika Ijumaa kwenye eneo lao la Facebook Silicon Valley.Mnada wao wa awali haukwenda vyema kama matarajio ya kampuni yalivyokuwa huku kila hisa zikipnda bei kidogo tu kutoka bei ya mnada ya dola 38 kwa hisa na kuuza asilimia 25 tu ya hisa zao zote.Zaidi ya hisa milioni 576 ziliuzwa na kubadili rekodi ya soko la awali la hisa nchini Marekani.Mwaka jana Facebook iliingiza mapato ya dola za kimarekani bilioni 3.7 na kuvuna faida ya dola za kimarekani bilioni 1.Facebook ina watumiaji wamtandao huo wapatao milioni 900 duniani kote


Kuibuka kwa Facebook na kuleta maajabu ya kiutamaduni duniani kulipelekea kutengenezwa kwa filam iitwayo `Social Network` mwaka juzi.Zuckerberg alianzisha mtandao wa Facebook akiwa bwenini katika chuo alichokuwa akisoma cha Havard miaka minane iliyopita.
\
Si Zuckerberg wala Chan ambao wameongezea chochote kwenye facebook zao kuhusu ndoa yao na watu wa habari wamekuwa wakituma e-mail kwa wahusika katika kampuni ya Facebook ili kupata ufafanuzi zaidi,lakini hazijajibiwa.

0 comments:

Post a Comment

 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797