Pages

 

Thursday, May 3, 2012

BIG BROTHER AFRICA HEWANI JUMAPILI, WASHIRIKI HAWA HAPA, RAPPER `PREZZO` WA KENYA NAYE NDANI YA MJENGO!

0 comments
Hii ndio logo ya gemu msimu huu wa 7
Lile shindano maarufu la kwenye televisheni duniani kwa upande wa Afrika, BIG BROTHER AFRICA,linaanza rasmi siku ya Jumapili tarehe 6 huko nchini Afrika Kusini.Shindano hilo linalorushwa na kampuni ya televisheni ya kulipia (PPV) ya DSTV kupitia chaneli maalum namba 198 na Africa Magic (chaneli namba114) litaanza kuwa hewani  siku hiyo  kuanzia  majira ya saa 3.00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki,huku washiriki wa shindano hilo linalopendwa kwa kiwango kikubwa na vijana,wakitangazwa na kuoneshwa jinsi wanavyoingia ndani ya jumba la Big Brother lililopo katika eneo la  Hendrik Verwoerd Drive, Randburg 2194, South Africa.Jumba la 
Sebule inavyoonekana
Chumba cha kulala washiriki
Sehemu ya kujiswafi aka bafuni and chooni
Big Brother Africa likiwa limeng`arishwa na kunakshiwa upya,litakuwa ni suprise kwa watazamaji kwani Big Brother mwenyewe ameahidi hivyo.Shindano la mwaka huu ni shindano la saba tangu mashindano hayo yaanze mwaka mwaka 2003, huku safari hii likiwa limebatizwa jina la `BIG BROTHER STARGAME.`na washiriki wataitwa `STARMATES `Kawaida nchi 12 hushiriki kwenye kinyang`anyiro hicho lakini safari hii zimeongezwa nchi mbili ambazo ni Liberia na Sierra Leone,nchi zingine ni Angola,Botswana,Ghana ,Kenya,Malawi,Namibia,Nigeria,Afrika Kusini,Tanzania,Uganda ,Zambia ,Zimbabwe,Ethiopia na Msumbiji
Hii ni` batch` ya washiriki maarufu (CELEBRITIES)watakaoingia mjengoni msimu huu

Shindano la mwaka huu ni wazi kuwa litawatia watazamaji homa,kwa sababu tofauti na mashindano yaliyopita safari hii kila mshiriki anatakiwa aingie kwenye jumba akiwa na mwenza ,mpenzi,rafiki,jirani au mama.Kuna suprise nyingi ambazo zimeandaliwa na Biggy na mojawapo ni uwepo wa majumba mawili...UPVILLE na DOWNVILLE.Mshindi atajiondokea na kitita cha dola 300 000 za kimarekani ambazo ni sawa na zaidi ya Tshs. 475 milioni.Kama kawaida ya suprise za Biggy, mwaka jana wakati shindano linaisha Jumapili ya Julai 31 walipatikana washindi wawili, Karen Igo msichana aliekuwa na umri wa miaka 27 kutoka Nigeria ambae alipata dola 200 000 na Wendall Parson mvulana aliyekuwa na umri wa miaka 23 kutoka Zimbabwe ambae nae alipata  dola za kimarekani 200 000


Tayari washiriki saba ambao ni kundi la waburudishaji maarufu barani Afrika (CELEBRITIES) wameshathibitishwa kushiriki huku washiriki wengine wakiendelea kutajwa kila siku zinavyosogea.Waliotajwa ni
Mampi (Zambia)
Roki (Zimbabwe)
Prezzo(Kenya)
Mchekeshaji Derrick ambae atakwenda kwa jina la DKB ( Ghana, miaka 26)

•Msanii wa muziki wa rap Prezzo ambae atakwenda kwa jina hilo hilo Prezzo (Kenya, miaka 32)

•Mwimbaji Martha ambae ataitwa Lady May ( Namibia, miaka 25)

•Mwanamuziki wa pop Suzan ambae ataitwa Goldie ( Nigeria, miaka (28)

•Mwanamitindo na mfanyabiashara,Babalwa ataenda na jina la Barbz ( South Africa, miaka 34)

Barbz (Afrika Kusini)
•Mwananuziki wa R&B Mampi atakaekwenda na jina lake hilo Mampi  (Zambia, miaka25)

•Mwanamuziki wakike Rockford ambae ataitwa Roki ( Zimbabwe,miaka 27)
Eazzy(Ghana ,hajathibitishwa)
Keita (Ghana,hajathibitishwa)
Pia kuna habari ambazo hazijathibitishwa kuwa mwana muziki wa kike wa Ghana Eazzy pamoja na mwanamitindo na mbunifu wa mavazi Keita wataungana na DKB kuiwakilisha Ghana.Tetesi zinasema kuwa Eazzy na Keita wanaingia kama wapenzi na DKB kama msanii maarufu(CELEBRITY) 
DKB ( Ghana)


Goldie(Nigeria)
Rapper J Cole atapamba ufunguzi
Kundi la Mulla kutoka Kenya
Lady May(Namibia)


Ufunguzi wa mwaka huu hapo Jumapili utapambwa na wasanii mbalimbali akiwemo mwanamuziki  J.Cole kutoka Marekani anaeletwa na kampuni ya burudani ya One Entertainment ya Los Angeles,ambayo mwaka jana ilifanikisha ujio wa Busta Rhymes kwenye Big Brother `Amplified.`Habari zinasema kuwa J.Cole atapanda jukwaani kuwasindikiza washiriki na nyimbo tatu,`Can`t Get Enough,Nobody`s Perfect na Work Out` Pia wasanii wengine watakao perform kama Mulla kutoka Kenya na wengine.
IK Osakioduwa wa Nigeria
Kama kawaida IK Osakioduwa atakuwa kilingeni kuendesha mambo.Kwa wale ambao watakuwa mbali na Tv zao wanaweza kuona  shindano hili kupitia mtandaoni kwa link hii:www.africamagic.tv/bigbrother

0 comments:

Post a Comment

 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797