Kocha wa timu ya soka ya Manchester United, Sir Alex Ferguson huenda akaachana na kazi yake ya ukocha mara tu baada ya kuisha kwa msimu wa 2012/2013,kutokana na kuanza kusumbuliwa na matatizo ya kiafya.
Kwa mujibu wa rafiki yake wa karibu ambae pia ni mmiliki wa timu ya Wigan Athletic,Dave Whelan,Ferguson anafikria kuachana na ukocha baada ya kupata matatizo ya kiafya Ijumaa iliyopita,amabapo alipatwa ghafla na ugonjwa wa kutoka damu puani mfululizo bila kuacha na kusababisha akimbizwe Hospitali ya Glasgow
Whelan alikuwa alikiambia kituo cha televisheni cha ESPN:

"Baada ya msimu ujao,Sir Alex atabwaga manyanga.Msukumo wa mambo unataka iwe hivyo,hasa unapokuwa uko juu kwa muda mrefu.Umri unapokuwa umeshakwenda inakuwa ngumu kupambana namsukumo wa majukumu,na ipo siku lazima itakuathiri.Sir Alex ni mgumu kukubali kushindwa na najua atataka aendelee na hadi siku atakayodondoka na pia naheshimu mafanikio aliyofikia kama wengine wanavyoheshimu.Najua lengo lake lilikuwa kuendelea kwa miaka miwili au mitatu zaidi,pengine zaidi ya hapo,lakini alipata matatizo kidogo ya kiafya wiki iliyopita,hiyo inaniambia kuwa lazima afikirie kwa kina maamuzi yake na atagundua kuwa hakuna ulazima wa kuendelea kwa miaka mingine mitano na kujiweka katika hatari.Ningependa niseme yeye ni kocha bora kabisa kupata kutokea.Kama ataamua kweli kufunga virago, basi litakuwa ni pigo kubwa katika mchezo wa soka.Nina hakika.Jinsi mafanikio yake yasivyo lingana na ya mtu (kocha) yeyote,jinsi anavyochagua wachezaji kwa usahihi na kupata mavuno zaidi kutoka kwao,inamfanya awe kocha bora kabisa,bora zaidi ya tuliowahi kuwaona"
0 comments:
Post a Comment