Pages

 

Saturday, May 5, 2012

SAGNA AVUNJIKA TENA MGUU,ATAIKOSA MICHUANO YA EURO 2012

0 comments
Beki wa kulia wa timu ya taifa ya Ufaransa anaechezea klabu ya Arsenal amevunjika mguu katika  mechi ya sare ya 3-3 dhidi ya Norwich City na atazikosa fainali zaKombe la Mataifa ya Ulaya yanayoanza tarehe 8 mwezi ujao.Sagna mwenye umri wa miaka 29 alivunjika mguu huo huo mwezi Oktoba na kuwa nje kwa miezi mitatu.

"Amevunjika mfupa wa nyuma ya ugoko.kwemye mguu ule ule ..ni lazima atakuwa amepigwa daruga sio hivi hivi tu.Kuna mchezaji amemwangusha na kisha akaukanyaga mguu wake...sijui ni bahati mbaya au vipi"Kocha wa Arsenal amewaambia waandishi wa habari.

 Yalikuwa ni matarajio ya wengi Sagna angejumuishwa katika kikosi kitakachokwenda kwenye fainali za Euro zitakazofanyika  kwenye nchi za Ukraine na Poland.Sagna hajachezea `Les Bleus` tangu mechi waliyotoka sare ya bila ya kufungana dhidi ya Romania mwezi Septemba wakati wa mchujo wa mashindano hayo makubwa  kabisa ya kimataifa barani ulaya.

Lakini kocha Laurent Blanc ana uchaguzi mpana wa mchezaji atakaeziba pengo la Sagna .Anthony Reveillere wa Olympique Lyon uwezo wa kucheza pande zote,kulia au kushoto na Mathieu Debuchy alionyesha kiwango kikubwa kwenye mechi dhidi ya Ujerumani mjini Bremen mwezi February.Blanc anatarajiwa kutaja vikosi viwili vya awali kabla hajachagua watakaounda timu. itakayoenda Euro.

Katika kikosi atakachokitangaza Jumatano hii,kitajumuisha wachezaji wanaocheza nje ya Ufaransa tu na Mei 15 atatangaza kikosi chenye wachezaji wanaocheza kwenye ligi za nyumbani

Blanc tayari alishamkosa beki wake wa kushoto Eric Abidal ambaye alifanyiwa upasuaji wa kubadilisha ini na pia kiungo Abou Duiaby naye ameumia nyama ya kiazi cha mguu

Ufaransa imepangwa kundi D pamoja na Uingereza,wenyeji Ukraine na Sweden

0 comments:

Post a Comment

 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797