Pages

 

Wednesday, May 23, 2012

MLINZI ALIEKUWA ANATETEA MCHORO WA ZUMA USIHARIBIWE AKAMATWA NA KUFUNGULIWA MASHTAKA

0 comments

Picha za televisheni zikionedsha Lowie Mabozela akishambuliwa
Mlinzi aliekuwa akitetea mchoro wa Rais wa Afrika Kusini,Jacob Zuma usiharibiwe  kwenye jumba la maonesho ya picha jijini Johannesburg amekamatwa na kuwekwa mahabusu


Kanali Vishnu Naidoo msemaji wa polisi alieleza:
"Amekamatwa muda mfupi uliopita "
Picha za televisheni zilimuonesha mlinzi huyo akimpiga kichwa na kumbinua sakafuni mtuhumiwa Lowie Mabokela kijana mdogo aliekuwa akichafua mchoro kwa rangi nyeusi jana Jumanne


Naidoo amesema Mabokela alifungua kesi ya kushambuliwa jana usiku

Mabozela akivuruga rangi nyeusi kwenye mchoro wa Zuma
Barend la Grange akiweka alama ya X juu ya mchoro
Kijana Lowie Mabozela

Unyama aliofanyiwa Mabokelo umezua mjadala na hasira zingine nchini Afrika Kusini


Mtuhumiwa wa pilialieharibu mchoro,Barend la Grange ambae ni profesa hakuonekana kufanyiwa unyama wakati anakamatwa


Jumba la maonesho liliendelea kuwa limefungwa leo Jumatano.Mtuhumiwa mwengine wa tatu alikamatwa akichora ukutani nje ya jengo la maonesho maneno yasemayo`RESPECT`
Barend la Grange

Watuhumiwa wote watatu wamepewa dhamana baada ya kusomewa mashtaka na mahakama ya Hillbrow


Habari zingine zinasema wenye maonesho wameamua kufunga na kuondoa mchoro wa Zuma na kuupeleka sehemu salama baada ya vitisho kuzidi

0 comments:

Post a Comment

 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797