Pages

 

Thursday, June 14, 2012

HII NDIO BARUA YA ORLANDO PIRATES YA KUMUITA OKWI

0 comments
 Klabu ya Orlando Pirates ya Afrika Kusni imetuma  barua ya kumtaka mchezaji wa Simba Sports Club ya Tanzania, Emmanuel Okwi kwenda nchini Afrika Kusni kwa ajili ya kufanya majaribio ili kuona kama anaweza kujiunga na timu hiyo
Barua hiyo  inatoa maelekezo kwamba Okwi atapewa majaribio ya wiki mbili na Orlando Pirates, huku akipewa huduma kuanzia malazi, matibabu, usafiri pamoja na gharama nyingine zitakazojitokeza  wakati akiwa huko.

Ni misimu miwili sasa Orlando wamekuwa wakimfuatilia Okwi ambaye klabu yake ya sasa, Simba, imeimesema ana thamani ya Tshs Billioni 2.Simba ilifikia hatua ya kutangaza thamani ya mchezaji wao huyo tegemeo,baada ya kuzuka habari mwanzoni mwa mwezi Juni kuwa Yanga wamemsajili mshambuliaji huyo raia wa Uganda.

0 comments:

Post a Comment

 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797