Pages

 

Wednesday, June 27, 2012

KIONGOZI WA MGOMO WA MADAKTARI AOKOTWA AKIWA HAJITAMBUI

0 comments
Mwenyekiti wa Jumuiya ya madaktari  nchini, Dk Stephen Ulimboka amelazwa katika hospital ya Taifa ya Muhimbili baada ya kuokotwa katika pori la Pande nje kidogo ya jiji akiwa taaban.Inasemekana Dk Ulimboka alitekwa jana na watu wasiojulikana.
  
Helen Kijo-Bisimba wa LHRC amenukuliwa katika East Africa Redio,ambaye amekariri maelezo ya Dkt. Ulimboka ambayo pia yamesikika yakitamkwa na mwenyewe (Dkt. Ulimboka Steven), kupitia kituo cha redio cha CloudsFM, kwamba walikuja watu watatu waliovalia kiraia na kujitambulisha kuwa wao ni askari. Watu hao walimchukua na kumuingiza katika gari lisilokuwa na namba na kuanza kuelekea barabara ya Bagamoyo. Huko walimfunga kitambaa usoni, kamba mikononi na miguuni kisha wakampiga huku wakimwambia amekuwa akiwasumbua kwa muda mrefu na kama wangekuwa na sindano ya sumu wangemmaliza kabisa.

Dkt. Ulimboka alifikishwa katika hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa huduma. Hali yake ni mbaya ila "stable".

 Baadhi ya watu wa shirika la Tanzania Legal Human Rights Center (LHRC) walifanya juhudi za kumtafuta kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dkt. Ulimboka Steven aliyekuwa ametoweka jana usiku.

 Taarifa iliyotoka kwa mmoja wa wanaharakati hao inasema, walifanikiwa kumpata Dkt. Ulimboka katika eneo la Mwabepande, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam,  akiwa amefungwa kamba miguuni na mikononi, hajitambui  na asiyeweza kuzungumza.



Taarifa hiyo inaongeza kuwa, Dkt. Ulimboka alikuwa amepigwa vibaya sana katika sehemu mbalimbali za mwili wake na anahitaji matibabu ya haraka
  
Juhudi zinafanywa kumpatia msaada unaohitajika Dkt. Ulimboka.

 HABARI INAYOHUSIANA:

 

0 comments:

Post a Comment

 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797