Pages

 

Monday, June 11, 2012

KITUKO:WAZIRI MKUU WA UINGEREZA ,DAVID CAMERON AMSAHAU BINTI YAKE WA MIAKA 8 PUB JANA JUMAPILI

0 comments
Ilikuwa ni mshike mshike David Cameron alipofika nyumbani na kugundua kumbe Nancy,binti yake mwenye umri wa miaka 8 hayupo kwenye msafara, amemuacha pub

Alipiga simu pub na kuhakikishiwa kuwa Nancy yupo pale na yuko salama

Akachomoka sekunde ile ile na kufunga safari ya maili 2 kurejea kwenye pub inayoitwa Plough Inn ambayo yeye na familia yake walikwenda kupata msosi wa mchana jana Jumapili

Inasemekana Mtoto huyo alikuwa yuko maeneo ya choo cha wanawake kwenye pub hiyo wakati msafara wa Cameron na mkewe unaondoka kurudi nyumbani,na hakuna aliyehisi chochote hadi walipofika myumbani.


Cameron, mkewe Samantha na watoto wao Nancy,Arthur (6)na Florence mwenye umri wa miezi 22, walikuwa wamejumuika na familia zingine mbili kupata chakula cha mchana katika mkahawa wa Plough Inn jana Jumapili.Mkahawa huo ulioanzishwa katika karne ya 16 upo maili mbili kutoka katika nyumba ya mapumziko ya Cameron iliyo maeneo ya vijijini.Baada ya chakula,Cameron na familia yake wakiwa wamezungukwa na walinzi,waliingia kwenye gari kurejea nyumbani,huku Cameron akiwa na dhana kwamba Nancy yumo ndani ya gari jingine alilopanda mkewe na watoto.Huku mkewe akidhani kuwa Nancy yumo kwenye gari alilopanda baba yake.

Waziri mkuu huyo aliporejea kwenye eneo la pub alimkuta binti yake huyo kajichanganya na wafanyakazi wa pub akiwasaidia kazi huku akiwa na furaha.




Plough Inn
Wahusika wa pub hiyo wanasema mara walipomgundua Nancy chooni hawakujua wafanye nini.Mmoja wa wafanyakazi hao alisema"Unaweza kujiuliza kwanini wasihesabu vichwa wakati wanaondoka.Wafanyakazi wa hapa walipomgundua mtoto chooni,hakuna aliepata wazo haraka,kwa sababu ni vigumu kupata namba ya simu ya waziri mkuu kwenye kitabu cha orodha ili kumfahamisha kuwa wamesahau mtoto nyuma"
SOURCE: The Sun

0 comments:

Post a Comment

 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797