Pages

 

Thursday, June 28, 2012

CHADEMA YATOA TAMKO KUHUSU MKASA WA DK.ULIMBOKA

0 comments
Benson Kigaila, Mkurugenzi wa mafunzo na organization Chama Cha Demokrasia na Maendeleo. akitoa tamko la chama hicho juu ya kutekwa na kuteswa mwenyekiti wa madaktari dk Ulimboka steven, katika makao makuu ya CHADEMA Mtaa wa Ufipa Kinondoni, leo mchana
Mkurugenzi wa Mafunzo na Oganaizesheni ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo,CHADEMA,Bw.Benson Kigaila leo mchana ametoa tamko la chama hicho juu ya utekwaji nyara wa Kiongozi wa Jumuia ya Madaktari Tanzania,Dk.Ulimboka Steven,ambae usiku wa kuamkia jana alitekwa nyara na watu wasiojulikana,kujeruhiwa na kutelekezwa katika maeneo ya Pandemabwe nje kidogo ya jiji la Dar Es Salaam.
Mbele ya waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu ya chama hicho Mtaa wa Ufipa,Kinondoni ,jijini Dar Es Salaam,Bw.Kigaila amesema: 
"Suala hili la kutekwa Dk ulimboka linatukumbusha miaka ya sabini wakati wagombea haki walivyokuwa wakipotea katika hali za kutatanisha. Matukio mengi ya kuuwawa wagombea haki nchini yanatuonyesha ni namna gani serikali yetu ni dhaifu na bunge lina meno ya plastic. 

Chadema tunadhani na ni ukweli ulio wazi kuwa tukio hili lina mkono wa serikali, IGP Mwema mtaalamu wa kuoteshwa kutokea vurugu katika maandamano ya chadema iwapi inteligensia yake katika hili?

Serikali haina nia thabiti ya kumaliza tatizo la madaktari maana imeamua kuongeza mishahara kwa baadhi ya watendaji wa serikali mpaka kufikia milioni kumi kwa mwezi, mfano ikulu inakarabatiwa kila mwaka kwa kutumia bilioni 6, hii ni hatari. Halafu wanatuambia serikali haina fedha za kumaliza tatizo la madaktari.. "
PICHA NA HABARI KWA HISANI YA HAFIDH KIDO (JEMBE)

0 comments:

Post a Comment

 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797