Pages

 

Friday, June 15, 2012

50 CENT ATAKA `KOLABO` NA WAYNE ROONEY

0 comments
Mwanamuziki mkali katika miondoko ya Hip hop 50 Cent ameelezea nia yake ya kushirikiana na mwanandinga mahili wa Uingereza anaekipiga katika timu ya Manchester United,Wayne Rooney.

Akiongea na gazeti la kila siku la Uingereza THE DAILY STAR 50 Cent amesema,anaamini kabisa kuwa akifanya collaboration ya kibiashara na Wazza wanaweza kuingiza kipato kikubwa hadi kufikia paundi bilioni 1,hasa ikiwa watawekeza pamoja kwenye biashara za migahawa na mavazi

"Mimi ni shabiki mkubwa wa Wayne,ana jina kubwa,ningependa siku moja tuwe washirika wa kibiashara
Soka la Ulaya kwa sasa ni biashara kubwa.Unaweza kuingiza pesa nyingi kwenye biashara ikwa utatumia majina ya wachezaji wenye majina makubwa"

"Nilishawahi kukutana na Wayne,ni mtu mzuri,ni mmoja wa wachezaji mahiri wa soka duniani,pia ana miaka mingi mbele katika kazi yake."

"Mimi wakati wote ni mtu wa mipango ya pesa na ninajua kuwa hata mtu wangu Wayne yuko hivyo.Nafasi za kutengeneza pesa hazina mipaka.Unawekeza kwenye migahawa Ulaya,maduka ya nguo,klabu za usiku.Kuingiza mamilioni ni poa, lakini kuingiza mabilioni ni jambo zuri zaidi na Wayne anafahamu hilo"

"Nimeshamualika Wayne, mashindano ya EURO 2012 yakiisha ningependa aje kunitembelea home Miami,yeye na familia yake.Hakuna atakaewasumbua wala kuwapiga picha,watu wangu wata hakikisha hilo halitokei"




0 comments:

Post a Comment

 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797