Pages

 

Thursday, June 21, 2012

WOLPER AANGUSHA KILIO AKIJITETEA KUHUSU GARI `ALILONYANG`ANYWA`

0 comments
Hivi karibuni kulikuwa na uvumi kuwa nyota wa filamu za  Bongo, Jacqueline Wolper Masawe amenyang’anywa lile gari alilokuwa akitanua nalo hivi karibuni aina ya BMW X6, lenye namba za usajili T 574 BXF na kwamba, sasa nyota huyo anatembelea gari lake la zamani Toyota Noah.Taarifa zinazsema
chanzo cha kuenea kwa tetesi hizo kilianzia kwenye mitandao ya kijamii na blog  ambapo wadau mbalimbali waliandika kuwa Wolper alinyang’anywa gari hilo na mwanaume aliyemnunulia.Wengine  wakitaja hata jina la Frank ambaye ni mtoto wa mfanyabiashara maarufu jijini Dar kuwa ndiye mmiliki wa gari hilo kwa sasa.Kwa mujibu wa mwandishi wa tabloids za Global Publishers ambae alikutana na Wolper Jumatatu ya wiki hii ,Wolper mwenyewe alikiri kusikia taarifa hizo huku akikanusha kuwa si za kweli.


“Na mimi nimesikia lakini si kweli jamani. Hivi mtu anaweza kunyang’anywa nguo yake ya ndani au shati lake? Si itakuwa kichekesho, gari ni mali yangu na hakuna mwenye uwezo wa kuja kuninyang’anya kwani nalimiliki kihalali,” alinukuliwa Wolper akisema.
Wolper alisema amelifungia gari hilo nyumbani kwake, Mbezi Beach, Dar  Es Salaam kwa sababu "lina matatizo kidogo".
Ili kujiridhishana hatimaye kuifahamisha dunia ukweli Wolper aliombwa kuongozana na waandishi  kwenda Mbezi kuliona gari hilo kama lipo kweli auikbidi alifuate na kulifikisha ofisi za Global Publishers.
: “Nisikuongopee kuwa naweza kuja nalo hapo ofisini wakati tatizo lake nalifahamu mimi, nakuja kuwachukua twendeni nyumbani mkalione.” Ndio jibu alilolitoa Wolper baada ya kutakiwa kulileta gari kwa uthibitisho


Saa 2:16 usiku, Wolper aliongozana na waandishi hadi nyumbani kwake na walilikuta gari hilo likiwa ndani ya geti.
Anaonesha kadi ya umiliki

Huku akilionesha  gari hilo Wolper aliangusha kilio na kusema:
“Watu wananionea sana, wananichafua. Sijui lengo lao ni nini hasa? Kila kukicha nasingiziwa jambo, mara Jack kafanya hivi, mara vile.Mbaya zaidi, hata waigizaji wenzangu wapo wanaonichukia, au kwa kuwa nimepata maendeleo kidogo? Walitaka niporomoke kimaisha?”


Kuhakikisha kuwa Wolper hajanyang’anywa gari hilo, pia alionesha kadi yake ya umiliki.
SOURCE:GLOBAL PUBLISHERS

  ZINAZO HUSIANA NA HII:
 

0 comments:

Post a Comment

 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797