Pages

 

Friday, April 20, 2012

WOLPER ABADILI DINI

0 comments
Katika picha ni Jacqueline Wolper na aina ya usafiri anaotembelea sasa
Staa wa kike anaekamata kwenye kiwanda cha muvi za kibongo Jacqueline Wolper ametajwa kuwa amebadili dini kutoka kwenye ukristo na kuhamia kwenye uislam.Staa huyo amenukuliwa na gazeti moja akikiri kuwa amefanya zoezi hilo wiki mbili zilizopita katika Masjid Kichangani pale Magomeni Mapipa na kuwa hivi sasa anakwenda kwa jina la Ilham.
Inadaiwa kuwa Wolper amechukuwa hatua hiyo baada ya kupata mchumba wa kiislam ambae kwa mujibu wa habari inadaiwa kuwa anatarajiwa kufunga nae ndoa karibu.Mchumba wake huyo ambaye ametajwa kuwa anakwenda kwa jina la Dulla au Dallas inadaiwa ameshajitambulisha kwa wazazi wa Wolper na kuwa Wolper mwenyewe alishaonana na wazazi wa Dallas
"Nimekuwa nikimchunguza Dallas kwa muda sasa na nimeridhika na nia yake ya kuishi na mimi kama mke na mume"
 Msanii huyo amesema kuwa sasa anajulikana kwa majina ya Ilham Wolper Dallas.Habari zinaendelea kusema kuwa baada ya Wolper kukubali kufunga ndoa na kuslim,mchumba wake huyo alitoa zawadi kwa mkewe mtarajiwa ambayo ni gari ya bei mbaya aina ya BMW X6 kama inayoonekana pichani

0 comments:

Post a Comment

 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797