Pages

 

Tuesday, April 24, 2012

ZOGO LAANZA KUGOMBEA KAMPUNI YA KANUMBA

0 comments
Hisani `TINO` Muya
MWIGIZAJI Nyota wa filamu na mtayarishaji wa filamu Swahiliwood, Hisani Muya` Tino`, amemshukia mchekeshaji na mwigizaji wa filamu Steven Mangere `Steve Nyerere` kwa kusema kuwa ni tatizo na mgombanishi wa wasanii wakubwa.
  
"Huyu Steve Nyerere ni mtu mbaya sana kwa sasa katika tasnia ya filamu, siku za nyuma wasanii walikuwa na ushirikiano wa kweli bila kuwa na makundi ambayo yapo sasa, na kila tatizo ukifuatilia utaambiwa Steve".

"Nimeshangaa sana hata msiba wa Kanumba haujakwisha tayari ameshatengeneza zengwe akidai kuwa mimi nimekaa na mama wa marehemu eti kumponda mdogo wake Seth asipewe kampuni ya Kanumba, hawezi kuongoza nipewe mimi", anasema Tino.

Tino alisema kuwa Steve Nyerere alimpigia simu kwa kumlaumu kuwa Bongo Movie wapo Leaders wakiwa katika kikao cha kumjadili yeye kwa kuingilia suala la marehemu wakati wao walikuwa wanataka kuisimamia kampuni hiyo kwa kumtumia Seth, lakini Tino anakuwa kikwazo jambo ambalo linawakera, lakini pia alisema anashangaa Steve kujiweka mbele wakati marehemu alijitoa katika kundi hilo.

Steven` NYERERE` Mangere
"Huyu anatakiwa kujua kuwa mimi sijajuana na marehemu juzi, nimekuwa nikifanya naye kazi mbalimbali hata kabla ya kufariki aliniita akaniambia anahitaji tuendeleze mradi wa kuinua vipaji vya wasanii wachanga na kusema nizifuate (tape) mikanda tuliyorekodi kwa ajili ya usaili wa wasanii tuliowafanyia siku za nyuma", alisema Tino.
 Steve Nyerere alipoulizwa kuhusu madai ya `TINO` alisema kuwa mambo hayo yalishapita na Tino waliongea naye yakaisha, sasa anashangaa kuyasikia tena yakiendelea bila sababu za msingi wakati yeye anaamini kuwa hayana faida yoyote.

"Jamani hayo mambo yamepita, tumwache marehemu apumzike kwa amani hakuna sababu ya kuendelea na malumbano yasiyotuingizia fedha na tusitafute umaarufu kupitia marehemu, tufanye kazi maisha yaendelee, kama kuna kosa kila mtu kajifunza kwa wakati wake", alisema Steve.

Kufuatia kifo cha Steven Kanumba kumekuwa na maneno yanayoashiria shari na kuibuka makundi kwa wasanii na kuzua vikao kila kukicha, huku wakishindwa kupanga mikakati imara ya maendeleo yao.


CHANZO: Mwanaspoti

0 comments:

Post a Comment

 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797