Kiungo wa kimataifa wa Tanzania, Nizar Khalfan aliyekuwa anacheza soka la
kulipwa katika timu ya soka ya Vancouver Whitecaps ya Canada inayoshiriki ligi ya Marekani, amejiunga rasmi na Mabingwa Watarajiwa’ wa Ligi Kuu ya
Tanzania Bara msimu huu, Simba, ambapo habari kutoka ndani ya klabu hiyo ambazo
bongostaz.blogspot.com imezipata, zinasema kuwa usajili wa mchezaji huyo
umefanikishwa na mmoja wa wafadhili wa zamani wa klabu hiyo, Azim Dewji.
Dewji mwenyewe alipotafutwa kuzungumzia hilo alikiri na kusema kuwa,
aliombwa na uongozi wa Simba kufanikisha usajili wa mchezaji huyo na kwamba
baada ya kufanikiwa, ameshamkabidhi Nizar kwa uongozi wa klabu abapo
aliongeza kuwa mchezaji huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar na Moro United
atakuwa na nafasi ya kuanza kuichezea Simba katika michuano ya kimataifa mwaka
huu endapo itaingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.Nizar baadae atakabidhiwa rasmi jezi atakayoitumia akiwa Simba.
Baada ya kuzing’oa Kiyovu
ya Rwanda na Setif ya Algeria, wiki hii Simba itaishukia Al Ahly Shandy ya
Sudan na kama ikifanikiwa kuvuka kiunzi hicho, itaingia katika raundi nyingine
itakayoamua timu za kucheza Nane Bora Afrika
Nizar alijiunga na Vancouver Agosti 22 2009 na kuichezea mechi 9 msimu huo wa 2209 na akasaini mkataba mwingine wa kuichezea timu hiyo msimu wa 2010.Juni 12 2010 aliifungia Vancouver goli lake la kwanza katika mechi dhidi ya Austin Aztex na tarehe 9 Februari 2011 alisaini mkataba mpya wa mwaka mmoja wa kuichezea timu hiyo katika ligi ya MLS
0 comments:
Post a Comment