Robin van Persie |
Tuzo hizo ni kwa kutambua mchango wake binafsi kwa timu yake msimu huu,ambayo ameifungia magoli 34 na kuisaidia kuingia kwenye mashindano ya Klabu Bingwa Ulaya.Scott Parker ndiye alitwaa tuzo hiyo msimu uliopita,tuzo ambazo hutokana na kura za waandishi wa habari za michezo wapatao 400 na washiriki wengine katika mchakato wa kupiga kura
Minong`ono ilienea kuwa Van Persie angetwaa tuzo hiyo na katika upigaji kura mdachi huyo alikuwa mbele akiwaacha wapinzani wake Wayne Rooney,Paul Scholes na mmarekani Clint Dempsey ambaye amesimama nafasi ya nne.Van Persie anakuwa mchezaji wa kwanza wa Arsenal kuchukua tuzo hiyo tangu Thierry Henry alipoitwaa mwaka msimu wa 2005 - 2006 na anakuwa mdachi wa pili tangu mchezaji mwengine wa Arsenal Denis Bergkamp alipoitwaa msimu wa 1997 - 1998 baada ya kuisaidia Arsenal kutwaa mataji mawili,la ligi kuu na la F.A
0 comments:
Post a Comment