Pages

 

Monday, April 16, 2012

EL HADJI DIOUF AKAMATWA NA POLISI

0 comments
Mwanasoka raia wa Senegal anaecheza mpira wa kulipwa nchini Uingereza katika klabu ya Blackburn Rovers El Hadji Diouf amekamatwa na polisi wa jiji la Manchester jana kwa tuhuma za kuhusika na fujo zilizotokea kwenye klabu moja ya usiku jijini humo
Katika fujo hizo ambazo zilitokea alfajiri ya kuamkia jana jumapili mtu mmoja anaetajwa kuwa na umri wamiaka 33 alijeruhiwa kichwani na shingoni
Diouf na watu wengine watano walikamatwa kwa tuhuma za kuhusika na fujo hizo na waliachiwa baadae kwa dhamana hadi kesi yao itakaposomwa hapo Mei 23 mwaka huu wakati uchunguzi juu ya tukio hilo unaendelea
Miaka 14 ya maisha ya soka la kulipwa ya Diouf imegubikwa na na matukioo ya utata kutokana natabia yake ya ukorofi.Hivi sasa mchezaji huyo amefungiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Senegal kucheza soka kwa muda wa miaka 5 baada ya kubwatuka mbele ya waandishi wa habari kuwa maafisa washirikisho hilo wanaendesha shughuli za shirikisho kama nyani

0 comments:

Post a Comment

 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797