Mtoto mwenye miguu sita amezaliwa mjini Sukkur nchini Pakistan wiki iliyopita na amelazwa kwa uangalizi kwenye Taasisi ya Taifa Inayoshughulika na Afya ya Watoto ya nchi hiyo,NICH,jijini Karachi.
Mkurugenzi wa taasisi hiyo Dr. Jamal Raza,amefafanua kuwa katika hali isiyokuwa ya kawaida ya mtoto huyo kuwa na miguu sita,mtoto huyo si mmoja kama anavyoonekana,bali ni watoto wawili katika mwili mmoja na kati yao mmoja bado hajakomaa.Amesema kuwa hali hii husababishwa na matatizo ya vinasaba(genetic desease) na kuwa matatizo hayo huwapata binadamu kwa uwiano wa kihesabu wa mtoto 1 kati ya watoto milioni 0.1.Amesema jopo la wataalam wa upasuaji watamfanyia uchunguzi wa kina mtoto huyo ili kuangalia namna ya kumsaidia na kwamba madaktari bingwa kutoka nchi mbalimbali ikibidi wataitwa ili kusaidia
Thursday, April 19, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment