Pages

 

Monday, April 23, 2012

MASHUJAA MUSICA YAIKWANGUA `TWANGA`

0 comments




 
Lilian `INTERNET`


Chalz Baba
Sudi Mohamed `MCD`
Saulo John `FERGUSON`








Bendi ya muziki wa dansi ya Mashujaa Musica imemnyakua mpiga tumba mahiri wa bendi hiyo, Sudi Mohamed ‘MCD’.

Hivi karibuni, bendi huyo ilimyangua muimbaji mahiri wa Twanga Charls Gabriel, ‘Chalz baba’ kabla ya kumchukua mnenguaji machachari Lilian Internet na sasa imekwenda kwa mpiga tumba tegemeo MCD.

Mbali na kumchukua MCD, Mashujaa pia imenyakua rapa wa Extra bongo, Saulo John ‘Ferguson’.

Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa Mashujaa Musica King Dodoo alisema
wameamua kuwachukua wanamuziki hao ili kuimarisha bendi yao katika ushindani wa muziki
ambapo wasanii hao wamejiunga kwa mkataba wa miaka miwili.

Alisema pamoja na kuongeza nguvu katika bendi hiyo, wamewachukua wanamuziki hao
kwa ajili ya kuendeleza vipaji vyao, ambapo Ijumaa hii wanatarajiwa kutambulishwa rasmi katika onesho litakalofanyika kwenye ukumbi wa Business Park, Kijitonyama Dar es Salaam.

Kwa upande wa wasanii hao kila mmoja alisema ameamua kujiunga na bendi hiyo kwa ajili ya
kuendeleza kipaji alichonacho sambamba na maslahi mazuri ambayo wamepewa na watakayopewa pindi watakapokuwa wakiitumikia bendi hiyo.

“Kikubwa ni maslahi ndiyo yamenipeleka Mashujaa Musica kwani siku hizi kila mtu anaangalia
maslahi yake kwanza, pia nataka kuendeleza umahiri wangu katika upigaji tumba,” alisema MCD ambaye ameitumikia Twanga Pepeta kwa miaka 12.

Naye Ferguson tayari ametunga vibao vitatu kwa ajili ya mashabiki huku pia akitarajia kutambulisha mtindo mpya uitwao ‘Kibega’.

0 comments:

Post a Comment

 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797