Pages

 

Wednesday, April 25, 2012

UKATILI GANI HUU!BINTI WA MIAKA 8 ABAKWA NA KUNYOFOLEWA JICHO

0 comments
Kuna habari kuwa binti mmoja mwenye  umri wa miaka 8 amebakwa ,kung`atwa ng`atwa shingoni na hatimae kung`olewa jicho lake
moja nchini Afrika Kusini katika jimbo la Kwazulu -Natal.

Polisi wa mji huo wamesema leo kuwa tukio hilo lilitokea juzi Jumatatu ambapo mbakaji huyo alimburuza msichana huyo mdogo hadi kwenye shamba la miwa lililopo karibu na nyumbani kwao anakoishi na bibi yake. Muda huo bibi yake alikuwa akimsubiri binti huyo arejee kutoka shule

Msemaji wa polisi mjini humo Captain Zulane Zwane alisema leo kuwa baada ya tukio hilo binti huyo alishindwa hata kutembea sawa sawa na kwamba alichoweza kufanya ni kujikokota hadi kwenye uwanja ulio karibu na nyumba yao ambapo alianguka na kupoteza fahamu.Alikuwa yuko kwenye mavazi ya shule huku nguo alizovaa na nywele zake zikiwa zimevurugika na kuchafuka.Baada ya hapo msichana huyo alikimbizwa kwenye zahanati iliyo karibu na baadae hospitali

Capt. Zwane akiendelea kuelezea mkasa alisema mbakaji alinyofoa jicho la binti huyo kutoka kwenye shimo la jicho lake la kushoto na alijaribu bila ya mafanikio kulitoa la kulia ambalo lilibaki limevimba sana.Binti huyo alikuwa akitokwa nadamu kwa wingi kutoka kwenye macho yake yote mawili.Mtuhumiwa pia alimng`ata binti huyo shingoni,alimbaka na kisha kumtelekeza.Uchunguzi umeonesha kuwa kulikuwa pia na jaribio la kumnyonga msichana huyo

Polisi wamesema kuwa mvulana mmoja mwenye umri wa miaka 15 amekamatwa kuhusiana na tukio hilo na atafikishwa mahakamani hivi karibuni

Msemaji wa Wizara ya Afya Kwazulu- Natal, Bw. Chris Maxon, amesema kuwa msichana huyo mwanzo alikimbizwa katika hospitali ya Eshowe kabla ya kuhamishiwa hospitali ya Ngwelezane ambako alikuwa akifanyiwa upasuaji leo mchana.Bado haijajulikana hali ya msichana huyo ikoje na kama madaktari waliweza kuokoa uwezo wake wa kuona

0 comments:

Post a Comment

 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797