Kwa mujibu wa habari nilizozinyaka kitu ambacho watumiaji
wengi wa kompyuta duniani hawakuwa wanakijua kuwa wezi wa kimataifa wanaotutumia
mitandao ya kompyuta (international hackers)waliingiza tangazo feki kwenye
mitandao duniani kwa lengo la kudhibiti mienendo ya kompyuta dunia nzima.Baada
ya hujuma hiyo, kwa kasi ya kushangaza, Shirika la Upelelezi la Marekani, FBI,
kwa kutumia kompyuta za serikali ya nchi hiyo, lilijanzisha mfumo salama wa
mtandao wa dharura kuzinusuru kompyuta zilizoshambuliwa duniani kote zisijifunge…lakini
ifikapo Julai mfumo huo utalazimika kuzimwa.
ifikapo Julai mfumo huo utalazimika kuzimwa.
FBI wanawashauri watumiaji wa kompyuta kutembelea tovuti ya http://www.dcwg.org, tovuti ambayo ni ya washirika wao katika mambo
ya usalama wa kompyuta,nao watawafahamisha watumiaji iwapo kompyuta zao
zimeshambuliwa au la na jinsi ya kupambana na tatizo hilo. Inasemekana kuwa
wale wote ambao kompyuta zao zimeshambuliwa hawatakuwa hewani baada ya Julai 9
Watumiaji wengi
hawajui kuwa kompyuta zao zimeshashambuliwa,ingawaje
virus hatari vimeshaanza kupunguza kasi ya kuperuzi mitandao na pia kuharibu
kinga (antivirus) kwenye kompyuta zao,na
hivyo kuwa hatarini kupatwa na matatizo
Mwezi Novemba mwaka
jana FBI kwa kushirikiana na mamlaka zingine za usalama,walikuwa wanajiandaa
kuusambaratisha mzingo mkubwa wa wezi wa mitandaoni ambao ulikuwa unaendesha
wizi kwa kutumia matangazo ya internet(internet ad) wakitumia lundo la kompyuta
zenye virus.
“Tuligundua kuwa
tunaweza kuja kupata matatizo kidogo kwa sababu tungesema tukamate mtandao
mzima wa hawa waharifu na kuwasweka jela…baadhi watumiaji wangekosa huduma ya
internet”alisema Bw. Tom Grasso msimamizi maalum kutoka FBI.”Mtumiaji wa
kawaida angeweza kufungua Internet Explorer na kukuta `page not found` na
kudhani kuwa ni matatizo tu ya network”
Usiku ule walipovamia
na kuwakamata,shirika hilo la upelelezi lilimleta Paul Vixie Mwenyekiti na
mwanzilishi wa Kituo Kinachounganisha Mifumo ya Internet(Internet Systems
Consortium) ili aunde server mbili za internet kuchukua nafasi ya server ambazo
zilikuwa zinashambulia kompyuta za watumiaji duniani ambazo tayari zilikamatwa
na kujazwa katika lori
Maafisa wa serikali
mwanzoni walikubaliana kuziacha server za serikali kuendelea kusaidia hadi mwezi Machi ili kuwapa muda watumiaji
kusafisha kompyuta zao, lakini ilionekana kuwa muda huo ni mfupi.Jaji wa New
York aliamuru server hizo za serikali
ziendelee kutoa huduma hadi mwezi Julai.
“Sasa tunawaachia
uwanja watu wa habari muwafahamishe watu juu ya tatizo lililopo…na ni juu ya
watumiaji iwapo watapenda kuzikagua
kompyuta zao”alisema Grasso
HIVI NDIVYO ILIVOTOKEA
Wezi hao wa kwenye mtandao wa kompyuta wameshambulia
kompyuta zipatazo 570 000 dunia nzima.Kutokana na udhaifu wa mfumo wa
uendeshaji wa Microsoft Windows(Microsoft Windows operating sytem) waliweza
kupenyeza virus kwenye kompyuta za watumiaji.Kitendo hicho kiliondoa uwezo wa programme za kuboresha kinga(antivirus updates)
na hatimaye kubadili mwenendo wa kompyuta zinavyofasiri anuani ndani kwa ndani,
kwenye mfumo wa internet unaotafsiri majina (Domain Name System)
Mfumo huu wa DNS ni mjumuiko wa server ambazo kazi yake ni
kutafsiri anuani za mtandao kwa mfano http://saidnuhu.blogspot.com/
na kadhalika.Iwapo kompyuta yako ilishambuliwa, jua kuwa wezi hao walipenyeza programme
zao na kuiongoza kuelekea kwenye kitafsirio (DNS) kilicho kwenye server zaoHii
imewawawezesha wezi hao kuzielekeza kompyuta
kwenye aina yoyote ya website za uhalifu.
Watu hao wamevuna mapato kutokana na matangazo ya biashara
(advertisements) mbalimbali ambayo yanatokea kwenye website za kizushi ambazo
watumiaji wamekuwa wakishawishiwa kuzitembelea.Wameingiza kiasi cha dola za
kimarekani milioni 14 kulingana na maelezo ya FBI na pia wamewafanya maelfu ya
watumiaji kutumia internet kwa kuzitegemea server za wahalifu hao bila kujua
Siku ambayo FBI na mamlaka zingine za usalama zilipowakamata
watu sita wenye asili ya Estonia mwezi
November, shirika hilo liliamua kutumia server
salama za Bw. Vixie ili kuziba nafasi za server za wahalifu.Kufunga na
kuziendesha sever mbili kwa miezi minane kumeighali serikali ya Marekani kiasi
cha dola 87 000
Ni vigumu kujua idadi
sahihi ya kompyuta zilizoathirika ,lakini FBI wanaamini kuwa hadi siku
walipowakamata waliohusika na uhalifu huo, kiasi cha anuani 568 000 za
mitandao ya kompyuta zilikuwa zikitumia server za wahalifu hao
Ikiwa ni miezi mitano sasa
imeshapita FBI wanakisia kuwa kiwango cha watumiaji walioathirika kimeshuka
hadi 360 000,huku Marekani yenyewe ikiwa na idadi kubwa ya watumiaji
85 000.Nchi zingine kila moja zina watumiaji waliathirika wasiopungua 25
000 ikwemo Italia,India,,Uingereza, na Ujerumani.Kiasi kidogo cha watumiaji
walioathirika kipo Hispania,Ufaransa,Canada,China na Mexico
Vixie amesema ni dhahiri kuwa
wengi wa watumiaji walioathirika na hili tatizo ni wale wa majumbani na sio
makampuni,kwa kuwa yana wataalam wao wanaokagua kompyuta kila mara
Maofisa wa FBI wamesema kuwa
wameunda mfumo wa kompyuta usiokuwa wa kawaida ili kuepusha mtandao wa kompyuta za serikali usiingiliane
na mtandao wa internet au kompyuta za watumiaji binafsi na ingawaje ni mara ya
kwanza FBI kuutumia mfumo huo,haitakuwa mara ya mwisho kuutumia.
“Hii ndio hatua tutakayochukua hata
hapo baadae”,Eric Strom, mkuu wa kitengo cha FBI cha mambo ya kompyuta alisema.”Labda kuwe na mabadiliko ya kisheria
ndani na nje ya Marekani,lakini ili tushughulikie matatizo kama haya kwa haraka
zaidi ni lazima tutumie njia hizi,kufuatilia na kuangalia njia zote,katika
upelelezi wa mambo kama haya”
Alisema sasa hivi kila mara FBI
wanapokaribia kumaliza kesi inayohusiana na kompyuta “inafikia hatua fulani
tunajiuliza sasa tufanyaje,tufanye nini ili tuusafishe mfumo wote bila ya kuzua
tatizo lingine kubwa zaidi ya hili”
TAFSIRI ISIYO RASMI KUTOKA
news24: http://www.news24.com/SciTech/News/Thousands-may-lose-internet-in-July-20120420
0 comments:
Post a Comment