Pages

 

Sunday, April 15, 2012

MUVI ZA KANUMBA ZAANZA KURUSHWA NA DSTV MWEZI MZIMA KUANZIA JANA

0 comments

 Kuanzia jana Jumamosi kampuni ya televisheni ya kulipia kwa njia ya satellite, DSTV,kupitia chaneli yao ya Africa Magic Swahili, imeanza kurusha filam zilizochezwa na msanii maarufu wa tasnia ya filam nchini Tanzania, Marehemu Steven Kanumba aliyefariki ghafla nyumbani kwake Sinza usiku wa  kuamkia Jumamosi ya tarehe 7 Aprili
 Ikiwa ni sehemu ya kumuenzi Kanumba chaneli hiyo jana ilirusha filam ya UNCLE JJ kuanzia saa 1.30  usiku na leo jumapili kuanzia saa 2.00 usiku chaneli hiyo itarusha filam ya iitwayo THIS IS IT (Part1 na 2)

Jumamosi ijayo tarehe 21 April watarusha filam  MORE THAN PAIN kuanzia saa1.30 usiku ikifuatiwa na YOUNG BILLIONAIRE  (Part 1 na 2)itakayorushwa Jumapili kuanzia saa 2.00 usiku nautratibu huo utakamilishwa Jumamosi ya terehe 28 kwa filam BLACK SUNDAY ambayo itakuwa kwenye skrini saa 3.20 usiku wa siku hiyo

Mkurugenzi mwendeshaji wa M-Net Africa Bi Biola Abi alimwelezea msanii huyo kuwa alikuwa ni mwenye kipaji, uwezo na malengo.
"Ni lazima tumfurahie kijana huyu mwenye mambo makubwa, ambaye alizichangamsha skrini zetu na kukonga nyoyo za wengi.Kifo chake ni pigo kubwa kwenye tasnia ya burudani Afrika,tunapenda kuwapa pole nyingi familia marafiki na wote waliompenda"

Marehemu Steven Kanumba akitaka kujua wasanii wa Afrika Mashariki watanufaika vipi na mpango wa DSTV wa kurusha filam zao.Hii ilikuwa siku ya uzinduzi wa chaneli ya Africa Magic Swahili

0 comments:

Post a Comment

 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797