Pages

 

Wednesday, June 13, 2012

WATU MATAJIRI ZAIDI TANZANIA

3 comments
Watanzania matajiri zaidi ni akina nani?Au kwa lugha nyingine,watu wanaomiliki mali nyingi zaidi Tanzania ni akina  nani?Bila shaka hayo ni maswali ambayo watanzania wamekuwa wakijiuliza na wenginne hata kubishana kuhusu matajiri katika jitihada za kutaka kujua nani ni tajiri zaidi ya mwingine na ana utajiri wa aina gani


Kwa hakika Tanzania ina matajiri wengi tu na makala hii ina lengo la kuwalinganisha ili kuwajua.Hapa chini ni orodha ya baadhi ya watanzania matajiri na utajiri wanaomiliki.1. Said Salim Awadh Bakhresa.Huyu ni mwanzilishi na mwenyekiti wa makampuni ya Bakhresa Tanzania.Mbali na kuwa mmiliki wa viwanda na mjasiliamali,Bakhresa pia ni mtoaji mkubwa wa misaada ya kijamii Tanzania ambae ameunda himaya kubwa ya kibiashara yenye mafanikio,inayojumuisha viwanda kadhaa,ndani ya miaka. 30

Kwa hiyo hakuna shaka kuwa Bakhresa ni mmoja wa matajiri wakubwa nchini TanzaniaHimaya yake ya kibiashara ni kubwa,iliyosambaa sehemu mbali mbali za Tanzania hadi Msumbiji,Uganda na Malawi.Baadhi ya utajiri alikuwa nao Bakhresa ni pamoja na:

 • Kiwamda cha kusaga nafaka
 • Vyombo vya usafiri wa kwenye maji
 • Uuzaji na usambazaji wa bidhaa za plastic
 • Biashara kubwa ya vyakula na vinywaji
2. Aziz Aboud.Huyu ni tajiri mwingine wa Tanzania.Tajiri huyu amewekeza kwenye sekta nyingi za kiuchumi kama vile vyombo vya kusafirisha abiria,vyombo vya habari na mawasiliano(ana miliki kituo cha redio na cha televisheni),viwanda vya vyakula na kampuni inayotengeneza magari makubwa ya mizigo.3.Nasoro.Tajiri huyu ana mlolongo mkubwa wa vitega uchumi.Unapozungumzia uchumi wa Tanzania,hautokuwa umeutendea haki iwapo hautotaja biashara za tajiri huyu.Biashara anazomiliki ni pamoja na
 • Ana miliki majengo kadhaa nchini kote
 • Mabasi ya abiria(mabasi ya Super star na Royal)
 • kusimamia uchukuzi wa mizigo(matrela ya Super Doll)
 • Pia ana hisa kubwa katika kampuni ya sukari Mtibwa.

 
 
4.Mohamed Dewji.Mohamed Dewji ni tajiri maarufu nchini Tanzania.Ana mlolongo mkubwa wa vitega uchumi na biashara,kuanzia viwanda,majengo ya kupangisha makazi na biashara na anamiliki hisa katika makampuni mengi makubwa ya Tanzania
5.Reginald Abraham Mengi .Ni Watanzania wachache sana ambao watakwambia hawamjui Reginald Mengi.Huyu ni mmiliki wa viwanda,mjasiliamali na kigogo wa vyombo kadhaa vya habari.Mengi ndiye anaemiliki makampuni ya IPP,moja kati ya miungano mikubwa ya makampuni inayomilikiwa na wat binafsi katika ukanda huu.Kampuni hii makao yake makuu yapo jijini Dar Es Salaam.Mbali ya makampuni ya IPP Mengi pia anahusika kwa kiasi kikubwa kwenye
 • Kampuni ya ushauri ya IPP
 • Kiwanda cha Coca-cola(Bonite na uzalishaji wa maji ya kunywa ya Kilimanjaro)
 • IPP Media ambayo ni mjumuiko wa vyombo kadhaa vya habari,ambayo inatoa magazeti ya The Guardian,Nipashe,vituo vya televisheni  vya ITV,EATV, na vituo vya redio SKY FM na East Africa Radio

 
6.Michael Ngaleku Shirima Inaaminika kuwa ana hisa nyingi katika makampuni makubwa mbalimbali ya Afrika Mashariki.Na pia ni mmoja wa wamilikim wa Precision Air amabayo ni kampuni ya ndege inayojishughulisha na kusafirisha abiria na mizigo katika Afrika Mashariki

 

7.Fida Hussein Rashid.Huyu naye ni mmoja wa matajiri wakubwa nchini Tanzania.Huyu ni mfanyabiashara mkubwa anaejihusha na
 • Kampuni ya kuunda mabodi ya magari(Africarriers)
 • Upangishaji wa majengo  kwa ajili ya makazi na biashara,ikwa ni pamoja na Raha Tower na Zahra Tower
 8.Yussuf Manji.Huyu naye,kama ilivyo kwa Bakhresa, Mengi na Dewji ni mmoja wa matajiri wanaojulikana sana na jamii kutokana na kujitokeza mara kwa mara kwenye shughuli za kijamii kama michezo na kadhalika.Yeye ni mmoja wa wahusika katika baadhi ya makampuni makubwa kabisa ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki, na pia anamiliki raslimali nyingi kama majengo kwa ajili ya makazi na shughuli za kibiashara,kampuni ya inayoshughulika na uunganishaji wa magari.Ni mmiliki wa makampuni ya Quality Group.

 9.Nazir Mustafa Karamagi.Huyu ndie anamalizia orodha ya watu matajiri zaidi nchini Tanzania huyu ni mfanyabiashara mwenye mafanikio anaemiliki kampuni kubwa maarufu nchini Tanzania inayojishughulisha na makontena.
  
Kwa kumalizia tu,zaidi ya hao waliotajwa hapo juu,kuna Watanzania wengine ambao wanaaminika kuwa ni miongoni mwa matajiri wakubwa nchini Tanzania,Hao ni....
 • Edward Ngoywai Lowasa
 • Mohamed Aboud
 • Abass Tarimba
 • Philemon Ndesamburo 
 CHANZO: HubPages
PICHA ZOTE:Kwa msaada wa mitandao mbalimbali

3 comments:

Mweyendezi Filbert said...

Mungu hawaongezee zaidi lakini pia watutoe watanzania na sio kutukandaniza kwa maslahi yao

eliussy edward said...

utatoka kwa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa sio kwa msaada wa mtu

Hussein Mnyaruge said...

kweli kuzaliwa maskini sio kosa,kosa ni kufa maskini

Post a Comment

 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797