Pages

 

Wednesday, July 10, 2013

BABA MZAZI WA JOHN TERRY NAE ASHITAKIWA KWA UBAGUZI

0 comments
Gazeti la Daily Mirror leo limebeba habari kuwa baba wa nyota wa timu ya soka ya Chelsea ya Uingereza John Terry amefikishwa mahakamani kwa kile kilichoelezwa kuwa `shambulio lililotokana na ubaguzi` na pia ameshtakiwa kwa kutishia kumuumshambulia mtu mwingine kutokana na hisia za kibaguzi.Makosa yote hayo aliyafanya kwenye tukio moja,ugomvi uliotokea katika mtaa mmoja jijini London.



Mzee Terry mwenye umri wa miaka 59,alitiwa mbaroni Machi 22 mwaka huu baada ya kutokea ugomvi aktika mtaa mmoja uitwao Frenchurch ndani ya jiji la London,nchini Uingereza.

Alisomewa mashtaka yake leo asubuhi katika kituo cha Polisi cha Bishopsgate wakati akiripoti kwenye dhamana aliyopewa.Watu wengine wawili,Tudor Musteata,47, na Stephen Niland  wanahusishwa katika kesi hiyo na watafikishwa mahakamani kujibu kesi tarehe 23 mwezi huu katika mahakama ya jiji la London.
Polisi wamethibitisha kuwepo kwa kesi hiyo lakini hawakutoa maelezo zaidi.

Kesi hiyo ya Terry mkubwa imekuja ikiwa ni mwaka tu tangu mtoto wamzee Terry John afutiwe mashtaka mahakamani kutokana na kesi iliyomkabili ya kumtolea lugha ya kibaguzi mchezaji wa Queen`s Park Rangers Anton Ferdinand mdogo wa Rio Ferdinand wa Manchester United


John Terry alikanusha kumtolea lugha hiyo Anton Ferdinand wakati wa mechi kati ya Chelsea na QPR mwaka juzi

Lakini Chama cha Soka cha Soka cha Uingereza kilipingana na maamuzi ya mahakama ya kumtoa hatiani John Terry na kudai kuwa utetezi wa Terry ulikuwa ni wa `kutunga na usioendana na tukio`,wakamfungia mechi nne.Terry hakukata rufaa FA na aliomba radhi kwa kosa lake la kutumia lugha isiyofaa.

Lakini alishutumiwa kwa kutomtaka radhi Anton Ferdinand mwenyewe na Chelsea nao walilaumiwa kwa kuendelea kumuachia Terry unahodha wa timu.

Katika miaka ya nyuma ,2002,John Terry akiwa na wachezaji wengine wawili,alifunguliwa mashataka ya kuvunja amani baada ya kuibua zogo dhidi ya baunsa kwenye klabu ya starehe usiku.Aliondolewa mashtaka baadae.

0 comments:

Post a Comment

 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797