Pages

 

Wednesday, July 10, 2013

FAMILIA YA MAREHEMU OMARY SYKES KUWASILI MAREKANI

0 comments
Familia ya  mwanafunzi mtanzania aliyeuwa mjini washington DC, marehemu Omary Sykes inatarajiwa kuingia nchini Marekani leo hii, swahili TV inaripoti. Kwa mujibu wa vyanzo vyetu faimilia hiyo itaongozwa na baba wa marehemu bwana Adamu Sykes na baba mkubwa  wake bwana Ilyasa Sykes.



Marehemu ambaye alikuwa na  miaka 22,  ni mjukuu wa mpigania uhuru maarufu wa Tanzania mzee Kleist Abdulwakili sykes na  pia ni ndugu wa  msanii star wa bongo Flava Dully Sykes.



Omar  aliuawa kwa shambulio la risasi karibu na maeneo ya chuo anachosoma cha Howard University usiku wa alhamisi julai 4, 2013 akiwa na mwenziwe katika mtaa wa Fairmont North West, kwa mujibu wa Polisi Washington DC (MPDC)  na Polisi wa chuo hicho (HPD), watu wawili ndio wanaoshukiwa kuhusika na mauaji hayo.Wahusika bado hawajatiwa mbaroni.



Kwa mujibu wa habari za ndani za jeshi hilo la Polisi, kitengo maalum cha uchunguzi wa mauaji kilichaanza upelelezi mkali ukiongozwa na Bwana Gabriel Truby wa MPDC na wameieleza Swahili TV*, licha ya upepelezi wanaoendelea nao  pia wanaomba ushirikiano wa wananchi kwajili ya kufanikisha uchunguzi wao. zawadi ya dola 25,000 itatolewa kwa yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa wauaji hao. 



Maripota wa Swahili TV wamefanikiwa kufanya mawasiliano na kitengo cha mauaji cha MPDC, Howard University Polisi  pamoja na familia ya marehemu Omar Sykes, kwa mujibu wa maelezo yao  mwili wa marehemu bado upo hospitalini kwa ajili ya uchunguzi na swahili TV inaahidi kuwaletea habari zote zinazohusiana na upelelezi huu. 

0 comments:

Post a Comment

 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797