Pages

 

Thursday, July 11, 2013

MAMA WA PROFESA J AFARIKI KWA AJALI,MWENYEWE AELEZEA.

0 comments
Profesa J akiwa aktika picha ya pamoja na wazazi wake siku  za nyuma
Mama mzazi wa mwanahip-hop nguli nchini Joseph Haule anaekwenda na jina la kisanii la Profesa J amefariki dunia baada ya kugongwa na gari huko Mbezi Juu nje kidogo ya jiji la Dar Es Salaam alikokuwa akiishi na mwanae


Taarifa zinasema kuwa Marehemu Bi Rosemary Majanjara Haule alipatwa na ajali hiyo alipokuwa akikatiza barabara kuelekea dukani majira ya saa mbili usiku na kuwa baada ya  kugongwa wasamaria wema walimsaidia kwa kumkimbiza Hospitali ya Tumbi Kibaha kwa kutumia usafiri wa Bajaj,ambako muda mfupi baadae alifariki dunia.Bado haijajulikana aina ya gari iliyomgonga.

 Vyanzo mbalimabli vya habari vimesema Profesa J mwenyewe amethibitisha kutokea kwa msiba huo na kuwa bado inamuwia vigumu kuamini kilichomtokea mama yake kwa kuwa muda mfupi baada ya kupatwa na ajali aliwasiliana nae kwa njia ya simu kumjulisha kuwa amepata ajali na yuko kituo cha Polisi (ilikupatiwa PF3 ambayo ingemuwezesha kutibiwa Hospitali) 
"Mama aliniambia mwanangu nimegongwa na gari njoo niko Polisi naandikisha...mwanangu nakufa..aliniambia mama na mara simu ikakatika.Kila nilipojaribu kupiga ikawa haipatikani."Alisema Profesa J kwa uchungu.
Profesa J alisema kuwa wakati anapigiwa simu na mamayake alikuwa katika mkahawa wa Nyumbani Lounge,maeneo ya Namanga,jijini Dar Es Salaam,amabko alikuwa na kikao na msanii mwenzie Lady Jay Dee na mumewe Gadna Habash ambao baada ya kuwafahamisha kilichotokea walimsindikiza hadi Hospitali ya Tumbi Kibaha.
"Tulipofika Hospitalini Tumbi sikuamini nilichokikuta,nilijua mama amelazwa,badala ya kupelekwa wodini nilipilekwa kwenye chumba cha maiti na kumkuta mama ameshafariki" Alisema Profesa J kwa majonzi
Said Nuhu Blog inatoa pole sana kwa Profesa J kwa kufikwa na mtihani huu.Mola Amlaze Pema Mama Rosemary Haule.Msiba upo nyumbani kwa Profesa J Mbezi Mwisho






Nyumbani kwa Profesa J








0 comments:

Post a Comment

 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797