Pages

 

Wednesday, July 17, 2013

MKONGWE GEORGE MASATU ALILIA KURUDI SIMBA

0 comments
Waliosimama kutoka kushoto.ni Rashid Msemakweli(Dokta)Abdallah Kibadeni,Often Martin,Razak Yusuf,George Lucas,Iddi Seleman,Damian Kimti,Abdul Mashine,George Masatu,Entienne Eshete,Mzee Abdulrahman Muchacho.

Waliochuchumaa kutoka kushoto ni.Kasongo Athuman,Selemani Pembe,Edward Chumila,Dua Said,Fikiri Magoso,Malota Soma na Mohamed Mwameja.
Hii ilikuwa ni mechi ya Simba na Yanga (Simba ilishinda 1-0 mfungaji Dua Said.)Nahodha wa Simba siku hii alikuwa ni Rashid Abdallah Magongo ambae hayupo  pichani, alikuwa na waamuzi pamoja na Nahodha wa Yanga Keneth Mkapa.

ALIYEKUWA  mchezaji wa Simba miaka kumi na tano iliyopita George Magere Masatu, amesema kuwa kwa sasa yuko tayari kurejea kwenye timu hiyo.
 

Masatu hivi sasa amerejea nchini akiwa tayari amestaafu soka lakini ana kadi ya uanachama wa timu hiyo yenye maskani yake Msimbazi jijini Dar es Salaam.

Masatu amesema kuwa yuko tayari kurejea kama kocha na siyo mchezaji tena kama ilivyokuwa awali Masatu alisema kuwa, ana uwezo na uzoefu kufundisha aliyoupatia katika shule ya soka ya Arsenal huko Indonesia alikokuwa akicheza soka la kulipwa kwa zaidi ya miaka mitano.
 

“Kweli nimerudi nyumbani kuendelea na maisha, lakini ukisema kuhusu Simba mimi ni mwanachama.Na kama wakisema nifanye nao kazi,niko tayari haina shida
 

“Nimekuwa kocha kwenye shule ya watoto ya Arsenal kule Indonesia kwa zaidi ya miaka mitatu. Ninajua kazi inavyofanyika na wakisema wanataka tufanye kazi, basi tutafanya hivyo,” alisema Masatu aliyekuwa beki kisiki wakati wa enzi zake.
 

Masatu alianza kufanya vizuri akiwa na Pamba ya Mwanza kabla ya kujiunga na Simba mwanzoni mwa miaka ya 1990.
Pamoja na kuwa na umbo dogo, Masatu alikuwa ndiye beki nyota na imara zaidi wa kati nchini na jina lake halijawahi kushuka chati pamoja na kuwa nje ya Tanzania kwa muda mrefu.

0 comments:

Post a Comment

 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797