Pages

 

Sunday, July 14, 2013

MUNGU KAINGILIA KATI?MALAIKA JIBRIL(GABRIEL)`AONEKANA KWENYE MAANDAMANO` MISRI

0 comments

Waandamanaji wanaomuunga mkono Rais Morsi,wamedai kuwa wameona mwanga wa aina yake..

Kwa mujibu wa gazeti la Al Arabia,taarifa hizi zimetolewa na muhubiri mmoja anayeegemea upande wa Morsi,wakati akiwahutubia wafuasi wa Morsi katika viwanja vya Rabia all-Adawiya jijini Kairo,

Katika hotuba hiyo iliyorushwa na vituo kadhaa vya televisheni vya Misri,muhubiri huyo amesema kuwa malaika Jibril ameonekana miongoni mwa wafuasi wa Morsi wanaoandamana

Muhubiri huyo Sheikh Ahmad Abdel Hadi kutoka kikundi cha Muslim Brotherhood amesisitiza kuwa watu wanaoheshimika kutoka Madina Al-Munawara, Saudi Arabia, wamemueleza kuhusu ndoto malaika Jibril alivyotokea na kuingia kwenye msikiti wa Rabia aL-Adawiya na kuwataka watu wanaoswali wakae kama walivyo.

Vile vile kuna taswira nyingine ilyotokea ya Mtume Muhammad(SAW)amejumuika na Bw Morsi na watu kadhaa.Katika taswira hiyo anasema muda wa swala ulipofika,watu walimuomba Muhammad(SAW)aongoze swala lakini Mtume alimteua Morsi aongoze swala

Muhubiri huyo amesema mtu mwingine wa kuaminika ametokewa na taswira inayoonesha ngamia wapatao 50,pamoja na vijana nawatoto kadhaa wakiwa jangwani.Baada ya muda wale ngamia,vijana na watoto wakaanza kusikia kiu kali.Walianzakuswali kumuomba Mungu awasaidie na papo hapo ardhi aligawanyika na che chem ya maji ikatokea.Baada ya kumaliza kiu yao,sauti ikasikika ikiwaambia vijana `watunzeni ngamia wa Rais Mohammed Morsi`


Wakati huo huo Sheikh Mosad Anwar wa Misri amemfananisha Morsi na Nabii Yusuf,kwa kuwa wote wametawala baada ya kupitia misukosuko kwa miaka mingi ikiwa pamoja na kuwekwa kizuizini mara kwa mara

Katika hatua nyingine Sheikh Shawki Abdel Latif mwakilishi wa Wizara ya Awqaf(Kusimamia Msaada ya Kijamii)ameibeza kauli ya muhubiri Abdel Hadi kwa kusema kuwa "..ndoto kama hizo zimelenga katika kuhalalisha vitu visivyofaa vionekane kuwa vinafaa,Wanaweka sumu kwenye asali kwa  kuongea uongo juu ya Mtume Muhammad,amani iwe juu yake"
Shekh huyo alipoulizwa zaidi na gazeti la Al Arabiya kuhusu uwezekano wa malaika Jibril kutokea katika msikiti wa Rabia al-Alawiya alijibu:"Huo ni uongo pia,Jibril ni Malaika na hutokea mbele ya Mtume wa Mungu tu"

"Maneno kama hayo ni njia ya kujaribu kutumia dini kwa manufaa ya kisiasa na kutaka kuhalalisha utawala wa Rais Morsi" Aliongeza Sheikh Abdel Latif
Sheikh Abdel Latif hakuishia hapo,alipendekeza kukamatwa kwa watu wanaoeneza habari kuhusu ndoto ya Mtume Muhammad akimwambia Morsi aongoze swala kwani kauli hiyo ni `tusi` kwa Uislam na Mtume mwenyewe

Makumi Elfu ya waandamanaji wanaomuunga mkono Rais Morsi walimiminika mitaani kwa wingi kuanzia juzi Ijumaa,wakiapa kupambana ili BwMorsi arejeshwe madarakani huku watu wanaounga mkono kupinduliwa kwa Rais Morsi wakiendelea na maandamano na kuweka pabaya mustakabali wa kisiasa wa Misri.

Chama cha Muslim Brotherhood,alikotokea Rais Morsi kinazidi kusambaratika kufuatia kukamatwa kwa viongozi waandamizi kadhaa na wengine kukimbilia kusikojulikana kufuatia mapinduzi ya Julai 3,ambayo chama hicho na wafuasi wake kimeyaita ni ya kijeshi.

Milio ya risasi katika eneo la jeshi jumatatu ya mwanzoni mwa wiki inayokwisha,imewaacha  makumi ya watu wakipoteza maisha yao na wengine makumi kujeruhiwa kulingana na takwimu za Wizara ya Afya ya nchi hiyo
 

0 comments:

Post a Comment

 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797