Pages

 

Sunday, July 21, 2013

WAENDA JELA KWA KUPOST NYAMA YA NGURUWE NA KEJELI KWENYE FACEBOOK WAKATI WA MFUNGO

0 comments
Alvin Tan na Vivian Lee wakiwa chini ya ulinzi
Wamiliki wa Blog moja inayojihusisha na masuala ya ngono Alvin Tan na Vivian Lee wamefunguliwa mashtaka na kuwekwa ndani bila ya dhamana nchini Malaysia baada ya kuweka picha inayowakosea waumini wa kiislam kwenye Facebook.Wanakabiliwa na adhabu ya kifungo cha miaka minane jela.

Alvin na Vivian kwenye picha iliyowaponza ambayo ina ujumbe unaotafsirika kama"Futari njema furahi na nyama ya nguruwe,harufu nzuri, tamu, inayotia hamu ya kula"
Picha iliyowaponza  ilikuwa ikiwaonesha wakila nyama ya nguruwe ikiwa na ujumbe wa kuwatakia waislam ramadhan njema.Mamlaka inayosimamia sheria nchini humo imelichukulia tuko hilo kuwa ni kosa kubwa,ikizingatiwa kuwa nyama ya nguruwe ni haram (hairuhusiwi) kwa waumini wa kiislam.Ingawa watu hao walijitetea kuwa walilenga katika kuonesha ucheshi wao,imechukuliwa kuwa inawavunjia heshima baadhi ya watu katika jamii na pia kuzingatia na kazi wanayojihusisha nayo wakosaji pia si nzuri ambapo wamekuwa wakiweka video za ngono kwenye ukurasa wao wa Youtube uitwao `Sexcussions with Alvin` na pia wanamiliki blog inayoegemea kwenye masuala ya ngono.

Picha za ngono ni marufuku kwenye nchi za Malaysia na Singapore,hivyo tukio hilo limesababisha Tan mwanafunzi wa sheria Chuo Kikuu cha Malaysia kunyang`nywa hati za masomo ya juu (Scholarship) ya nchi za ASEAN,baada ya malalamiko ya wananchi dhidi ya blog yao.

Tan na Lee wameshakana mashtaka yao na wamewekwa ndani bila dhamana hadi kesi yao itakapoanza kusikilizwa Agosti 23 mwaka huu.Baada ya tukio hilo waliomba radhi kwenye ukurasa wao wa Youtube kwa kusema:
 "Tunarekodi video hii ili kuwaomba radhi waumini wa kiislam kwa kuwa tumewakosea kwenye mwezi huu mtukufu wa Ramadhan"


0 comments:

Post a Comment

 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797