Pages

 

Wednesday, July 10, 2013

LEO VODACOM TANZANIA INAZIFUNGIA LAINI 450,000 ZISIZOSAJILIWA

0 comments
Kampuni inayotoa huduma ya mawasiliano ya simu za mkononi Vodacom kitengo cha Tanzania,leo kinaziondoa hewani kadi za simu 450 000 ambazo hazijasajiliwa hadi sasa,Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni hiyo Rene Meza amesema.

Bw Rene Meza
Bw.Meza aliyasema hayo jana alipokuwa akihojiwa na mtandao wa taasisi inayohusika na taarifa za mawasiliano Tele Geography.Alisema Vodacom Kitengo cha Tanzania wanawajibika kwenda sambamba na sheria za Tanzania za Mawasiliano kwa njia ya Umeme na Vifurushi (APOCA) ya mwaka 2010,ambayo inazitaka kampuni zote za simu nchini kusajili namba za simu za wateja wao.

Na kwa sababu hiyo,kampuni imeamua kuzifungia laini 450,000 kwa sababu kuu mbili,ambazo ni kutimiza matakwa ya sheria ya mawasiliano na vile vile kuhakikisha rekodi za mawasiliano za wateja zinaendana na wakati tulionao

Kutokana na hali hiyo,afisa huyo wa Vodacom Tanzania amesema kampuni imeshaanza kuingiza teknolojia inayoweza kufunga laini tangu tarehe 1 mwezi uliopita.Amedokeza kuwa,ili mteja aweze kufunguliwa kadi yake ya simu ya Vodacom,atalazimika kufuata utaratibu wa kujaza nyaraka maalum za usajili.

Ufungaji wa kadi za simu unafanyika ili kuendana na sheria mpya iliyowekwa na Mamlaka inayosimamia mawasiliano nchini TCRA.

TCRA ilitoa siku 40 kuanzia Juni 1 hadi Julai 10 2013, kampuni zote zinazotoa huduma ya mawasiliano ya simu za mkononi nchini kuzifunga laini zote zisizosajiliwa

0 comments:

Post a Comment

 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797