Pages

 

Wednesday, July 17, 2013

BREAKING NEWS:LUKUMAY WA KLABU MASAI AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI

0 comments
LUKUMAY  (kulia)enzi za uhai wake
Habari nilizozipata muda mchache uliopita ambazo zimethibitishwa na ndugu na jamaa wa karibu zinasema Benedict Charles Lukumay amefariki kwa ajali ya gari eneo la Mikumi mkoani Morogoro usiku huu.
 
Chanzo cha kifo chake kimeelezwa kuwa ni ajali ya gari iliyotokea eneo la Mikumi mkoani Morogoro majira ya saa mbili usiku. Meneja mkuu wa Meridian Hotel LTD Mzee Mponda amethibitisha juu ya kifo hicho, huku huku akisema kuwa ilitokana na ajali ya gari.

 "Wakiwa na mwenzake aliyefahamika kwa jina la Adrian na gari binafsi wakielekea mkoani Iringa gari aliyokuwamo marehemu iligonga nyuma ya roli lililokuwa limesimama njiani." alisema Mzee Mponda.

 Adrian ambaye ndiye aliyekuwa anaendesha gari alinusurika kwenye ajali hiyo.

 Benedict alikuwa ni mmoja kati ya Wakurugenzi watendaji wa kampuni ya Meridian Hotel LTD inayomiliki na kuendesha kumbi za burudani zikiwemo Masai Kinondoni, Masai Ilala na Masai Galapo Ilala.
Kifo chake kimeacha pengo kubwa si tu kwa familia bali hata wapenda burudani, akifahamika kimchango katika kusimamia na kuendeleza burudani na yakiwemo maonyesho mbalimbali ya wanamuziki wa bongo fleva na fani nyinginezo.

Mungu alaze Pema ROHO ya Marehemu Ben..

0 comments:

Post a Comment

 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797