Pages

 

Monday, July 8, 2013

BAYERN YATANGAZA RASMI MARIO GOMEZ KUJIUNGA NA FIORENTINA

0 comments
Mabingwa Soka Barani Ulaya kwa ngazi ya vilabu,Bayern Munich imetangaza rasmi kuachana na mshambuliaji Mario Gomez na kwamaba wamefikia makubaliano na timu ya Forentina ya Italia ambao wamekuwa wakimfuatilia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kwa muda sasa.Mchezaji huyo alipokonywa nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza cha Mabingwa hao wa Ujerumani na mshambuliaji mwingine Mario Mandzukic.

Wiki iliyopita Bayern walisema kuwa mpango wa Gomez kwenda Fiorentina umekufa huku ikiripotiwa kuwa Fiorentina hawakuwa tayari kutoa kitita cha euro milioni 20 walizotaka Bayern.

Mkurugenzi wa mawasiliano wa Bayern amesema uhamisho wa mchezaji huyuamabao unatajwa kuwa utakuwa hadi 2017, utasainiwa katika wiki moja au mbili zijazo na katika mkataba wake Gomez anatarajiwa kuvuna kitita cha euro milioni 4 kila msimu Gazeti moja la Italia Gazetta Dello Sport limandika kuwa Fiorentina watatoa euro milioni 15 kumnyakua mchezaji huyo

Mkataba wa Gomez na Bayern ulikuwa unaenda hadi 2016,lakini katika kile kilichoelezwa kukasirishwa kwa fowadi huyo na kitendo cha kutopangwa mechi nyingi za msimu uliopita.Kocha Jupp Heynckes alikuwa akimtumia Mandzukic mara kwa mara.Aliomba auzwe timu nyingine ili apate nafasi ya kucheza na kujihakikishia nafasi ya kwenda Kombe La Dunia Brazil 2014 .

Ingawaje hakupngwa mechi nyingi Gomez alifanikiwa kufikisha idadi ya magoli 19 msimu ulioisha yakiwamo mawili aliyofunga kwenye fainali ya Kombe la Ujerumani

Mchezaji huyo amebatizwa jina la Super Mario,linalotokana na kikaragosi cha kwenye mchezo wa kompyuta.Alijiunga na Bayern Miunich mwaka 2009 akitokea VfB Stuttgart kwa ada ya uhamisha ya euro milioni 35.Ameifungia timu ya taifa ya Ujerumani magoli 25 katika mechi 58 alizocheza.

0 comments:

Post a Comment

 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797