Pages

 

Wednesday, July 10, 2013

TUHUMA ZA KUAIBISHA ZAMUANDAMA ODAMA

0 comments
Mtandao wa bongo movies umetumiwa madai, kumhusu mwanadada muigizaji wa Filamu aliyepata tuzo hivi karibuni, Jennifer Kyaka anakwenda na jina la kisanii la Odama kuhusu safari zake za kwenda nje ya nchi.
Habari au tuhuma hizi , zinasema kuwa mwanadada huyo huwa haendi nje ya nchi kama anavyowaambia washabiki wake kupitia blog yake ya odama1.blogspot.com kuwa anasafiri kwenda nje kikazi zaidi, na badala yake imesemwa kuwa huwa anabaki hapa hapa nchini akijifanya yupo nje ya nchi,akiwa na lengo la kulazimisha umaarufu

Mdau aliyepeleka tuhuma hizo amesema kuwa ana ushahidi wa kutosha wa picha mbalimbali toka kwenye mtandao mmoja wa kijamii ambao staa huyo  anautumia kudanganya ,zikimuonesha akiwa maeneo mbalimbali ya “duniani huko” ambayo kwa kuangalia picha hizo anasema kuwa ni feki na zimetengenezwa kwa kutumia teknolojia tu ya kuhariri picha maarufu kama PHOTOSHOPMtandao wa Bongo Movies umewaomba wadau wenye majibu na utaalamu wa picha wasaidie kwa kutazama picha hizi ili kuthibitisha kama tuhuma hii ina ukweli wowote.

0 comments:

Post a Comment

 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797