Pages

 

Tuesday, July 9, 2013

LAURYN HILL AFUNGWA JELA

0 comments
Aliekuwa mwanamuziki mashuhuri wa nchini Marekani na duniani ambae pia aliwahi kubeba tuzo ya Grammy,Lauryn Hill, ameanza kutumikia adhabu yake ya kukaa jela miezi mitatu kwa kosa la kukwepa kulipa kodi
Hill anaanza kutumikia adhabu hiyo kwenye gereza la Danbury katika jimbo la Connecticutt huko kwao nchini Marekani


Wafungwa kwenye gereza hilo ambalo ulinzi wake si mkali,wanaishi katika vyumba vilivyokuwa  katika mabweni na wajibu wao ni kufanya kazi mbalimbali

Hill ambae alianza fani yake na kundi la Fugees akiwa bado msichana mdogo katika miaka ya 1990 kabla ya kutoa albam yake ya Miseducation of Lauryn Hill  mwaka 1998,alikubali kosa lake mwaka jana,la kutokulipa kodi katika kiasi cha dola milioni 1.7 alizoingiza kuanzia 2005 hadi 2007

Pia imejumuishwa kodi aliyoikwepa mwaka 2008-2009.Mwanasheria wake aliiomba mahakama isimfunge,ila awekwe chini ya uangalizi kwa vile Hill amekuwa kitoa sana misaada kwa jamii,hali ya familia yake ambayo imekuwa kubwa na pia kutokana na ukweli kuwa deni alilodaiwa ameshalilipa

Wakati akisomewa hukumu mwezi Mei Hill aliezea jinsi alivyoshindwa kulipa kodi alipoamua kuachana na mambo ya muziki ili kujiweka mbali na matatizo ambayo yangeweza kumtokea,yeye na watoto wake.Ana watoto sita sasa.

Alielezea kuwa mabo aliyokuwa akitendewa alipokuwa katika fani ya muziki ndio yaliyomsukuma kuachana na biashara hiyo

Naibu mwanasheria mkuu wa Marekani Bi Sandra Moser aliutambua na kkuelezea kipaji cha ubunifu alichokuwa nacho Hill na moyo wake wa kuwakumbuka watoto masikini ,lakini akasema sababu alizotoa Lauryn Hill ni visingizio tu vilivyojengwa na na hisia zake na wala haviwezi kumfanya akwepe kuwajibika

Akitoka kifungoni  atatakiwa awe chini ya uangalizi kwa muda wa mwaka mzima na  atakuwa kwenye kifungo cha nyumbani katika miezi mitatu ya kwanza

0 comments:

Post a Comment

 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797