Pages

 

Thursday, July 11, 2013

DEREVA WA DALADALA ABWAGIWA MAITI YA KICHANGA NA MZAZI MWENZIE

0 comments
Vitendo vya ukatili dhidi ya  watoto na wanawake  jijini mbeya vimeendelea chukua sura mpya  baada ya dereva wa daladala jijini humo kumzalisha mwanafunzi wa Masomo ya jioni kituo cha Juhudi kilichopo  Ilomba.
.
Hii daladala ilibeba maiti kutoka Uyole
 Tukio hilo limetokea hivi karibuni  eneo la mama John Mtaa wa Ihanga Kata ya Ilomba ambapo dereva wa daladala aliyefahamika kwa jina la Aswile Mwalukoba (45 ) kubwagiwa kichanga wa miezi saba ambaye alikwishafariki baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Akizungumzia tukio hilo Mwenyekiti Mtaa huo Ndugu Emanuel Mwasibata amesema kuwa mgogoro huo umetokana  na dereva huyo kugoma kuuzika mwili huo kwa kile alichodai kuwa hivi sasa haishi na binti huyo kwa muda mrefu sasa.
Kwa upande wake binti huyo aliyefahamika kwa jina la Calorina Kyando amedai kuwa uamuzi wa yeye kuuchukua mwili wa mtoto huyo hadi kwa baba yake unatokana kutelekezwa na bwana huyo kisha kupigwa marakwa mara na kusababishiwa ulemavu wa sikio la kushoto baada ya kung’atwa na mwanaume huyo.

Mwili wa mtoto ukiwa umewekwa kwenye sofa nyumbani kwa Bw.Aswile
Mwanamke huyo amefafanua kuwa mara baada ya mtoto huyo kufariki wakati akipatiwa matibabu katika Hospital ya Igawilo jijini humo aliamua kumpigia simu mzazi mwenzie kwa lengo la kumpa taarifa za msiba huo.
Amesema mara baada ya kutoa taarifa hiyo, mwanaume huyo alikubali na kumueleza mwanamke huyo kuwa yuko tayari kumzika mtoto huyo na kwamba anafanya taratibu za kuwasiliana na ndugu zake walioko Tukuyu Wilayani Rungwe

Carolina Kyando (kushoto)akiwa na dada yake wakiwa nyumbani kwa  Bw.Aswile
Amesema katika siku iliyofuata mwanaume huyo hakupatikana kwa simu ya kiganjani na wala hakuwepo nyumbani kwake anapoishi eneo la Mama John, hali iliyopelelekea baadhi ya majirani pamoja na mwanamke huyo kutoka Uyole kusaidiana na kuutoa mwili huo Hospitalini hapo kwa lengo la kufanya taratibu nyingine .
Baada ya kushauriana mwanamke huyo na majirani hao waliamua kuchukua maiti hadi nyumbani kwa Mwalukoba ambapo waliiweka kwenye kiti ndani ya nyumba yake huku wakiendelea kumsubiri mwalukoba arudi aliko  ambapo baadaye alirudi nyumbani hapo akisindikiazwa na Mdogo wake aliyefahamika kwa jina Gabriel Mwalukoba hadi nyumbani hapo.

Wakazi wa Uyole wakijadiliana baada ya kumkosa Bw.Aswile

Kitendo hicho cha kurejea kwa mwanaume huyo kilifanya mwenyekiti wa mtaa huo Ndugu Emanuel Mwasibata kuhoji juu ya  kutoweka kwa nyumbani kwakwe kwa muda wa siku mbili huku kukiwa hakuna mawasiliano yoyote.

 
Bw.Aswile (aliyeshoka gongo)baada ya kurudi nyumbani


 Baada ya kikao cha muda mrefu kati ya pande zote mbili mwanaume huyo alikubali kuupokea mwili huo na hivyo kuanza kufanya taratibu za mazishi ambapo mazishi hayo yalifanyika katika makaburi ya Iyela mida saa 12 jioni na kuhudhuriwa na familia zote mbili pamoja na majirani wengine kutoka Uyole na Mama John

Majirani kutoka pande zote mbili wakisubiri muafaka wa kikao

0 comments:

Post a Comment

 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797