Pages

 

Monday, August 11, 2014

HASIRA ZAMFANYA VAN GAAL KURUDI UHOLANZI

0 comments
Baada ya Kocha wa Manchester United Louis Van Gaal  kuchukizwa na kitendo cha kukosa windo lake alilokuwa amelitolea macho muda mrefu,anajiandaa kufunga safari kuelekea Uholanzi kutafuta njia mpya ya kujifariji kwa kuvamia Klabu ya Ajax nchini humo

Manchester United wanajiandaa kutoa ofa ya kitita cha pauni 15 milioni kumnasa beki Daley Blind,baada ya kutoka kapa kwenye mbio za kumuwania Thomas Vermaelen,gazeti la Mirror nchini Uingereza limeripoti leo.
LVG anasemekana kumuwekea kipaumbele Varmaelen katika muda huu mchache uliobaki wa dirisha la usajili,lakini jana wababe wa Catalan waliitangazia dunia kuwa wameshamnasa beki huyo raia wa Ubelgiji aliyetimka kutoka Arsenal.

Akiwa anachukizwa na vigingi anavyokutana navyo kwenye usajili,Van Gaal bado hajakata tamaa,kiasi kwamba yuko tayari kufanya uvamizi kwenye klabu ya Ajax,kumnasa Blind

.Daley Danny Blind ambaye ni mtoto wa Danny Blind, kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Uholanzi,alijizolea sifa wakati wa michuano ya Kombe la Dunia nchini Brazil kwa uwezo wake wa kuzuia na kusaidia mashambulizi tangu mechi yao ya kwanza dhidi ya Spain,alipotoa krosi murua ilyozaa bao safi la kusawazisha la Van Persie Blind ana uwezo wa kucheza nafasi  tofauti ,hasa beki wa kati au kiungo wa kati. ingawaje anajisikia poa kukaba upande wa kushoto

Kiasi cha pauni milioni 15 zitawekwa mezani siku chache zijazo kwa ajili ya nyota huyo wa Kiholanzi mwenye umri wa miaka 24 na imedokezwa kuwa Ajax,wamesalimu amri kumpoteza mchezaji wao huyo muhimu,baada ya Blind mwenyewe kuonesha nia ya kutaka kuondoka.

Aliwahi kusema"Unategemea nifanye nini Van Gaal atakaponihitaji Manchester United?Inabidi nitafakari.
Kombe la Dunia limeniongezea heshima kama mchezaji na nilishaweka bayana kuwa kama kuna watu watakuja na ofa nzuri nitawasikiliza."




Read more...
 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797